Kwa hili la Ommy Dimpoz na Babake wee uliye biological mother/father ukimkataa/kumtelekeza mtoto wako ujue umemuumiza sana kisaikolojia na makuzi yake

Mzee Nyembo alikula maisha na pisi kali, hakujihusisha na maisha ya mwanae hata mama yake alipokufa akiwa angali mdogo. Kwa ukatiri alioonyesha sio kosa Ommy Dimpoz akiishi naye kwa umbali hivi hivi kwa sababu hizi:

1. Mzee alitarajia Ommy awe chokoraa, choka mbaya au kibaka ndio maana hakujali
2. Mzee aliona ni kawaida kuzaa kama mbuzi ukaenda zako, mbuzi akitungisha mimba huwa harudi kwa ndama kudai chochote. Naye aishi hivyo hivyo
3. Mzee alijua possibility ya mwanae kufanikiwa ila alijishauri kwamba ale bata atakuja kuomba msamaha
4. Kuna vijana maelfu wanaacha watoto wao, itakuwa ni inspiration kwao kuona kumbe unaweza fyatua tu ukadanga zako miaka ya baadaye mtoto atakutunza. Waliokimbia majukumu wakikaziwa hivi ni onyo kwa vijana wa ovyo ovyo
 
Una mtoto?
 
Asanteee
 
Ukikua utajua

Brother najua kuna vingi sana natakiwa kujifunza lakini siungi mkono kumlaumu ommy kwa kitu alichoamua kukifanya

Kwangu naamini baba ni zaidi ya kuwa sperm donor, ubaba ni jukumu

Hata kama umekosana na mwanamke na akakuzuia kumuona mtoto Ila ikifika stage mtoto akakutafuta na usioneshe umuhimu wake kwako hadi pale ulipoona kuna dalili ya mlo.

Naamini hustahili kuforce kupata nafasi kwenye maisha yake kwa sababu ya kutoa mbegu ambazo hukuona thamani yake mwanzoni.
 

Brother kuna watu wapo proud kabisa

"Nina watoto wanne Ila wanaojulikana wawili Ila hawa wengine sijui hata sarakaar wapi, wakishakua watanitafuta"

Hii kauli nimeisikia mara nyingi sana, yaani mzazi anakula bata na malaya bar Ila hana uhakika kama mtoto wake amepata hata mlo mmoja

Mtoto anaishi kwa kuteseka, anapambana hadi anatoka bila kutegemea thumni yako, Leo hii uzee umekufikia, marafiki na malaya ulionjoi nao hawapo tena, ndio unaamua kurudi kwa mtoto uliyemuweka kando shamelessly

Mimi naona wakaziwe maana sijawahi kuona mtu kaenda kulilia akubaliwe uzazi na teja, ni waliofanikiwa tu,
 
Amesema mama yake alifariki kama sikosei
Yeye mama ndie anaeujua ukweli

Mtoto hawezi kumjui baba yake bila mama kumwambia huyu ndio baba yako maana mama ndie mwenye kumjua baba halisi wa mtoto,

Km mama yake kabla hajafariki aliwahi kumwambia kua huyo ni baba yake akamtambulisha na yeye akamfahamu hapo sawa..

Ila km mama yake hakumwambia kua huyu ndio baba yako basi hapo bado kuna giza totoro (wasituletee maigizo)
 

Nimalize kwa kusema WANAWAKE WANAKERA SANA.kuna mwanamke nilizaa nae nilijuta.nikasema sitolaumu mwanaume anayekataa mtoto.ni kweli ommy kafanyiwa mabaya.hilo sikatai.kama Ana uwezo amsaidie tu na amwambie nakusaidia Kama mtu uliyenileta duniani na sio BABA.
 
Nawaona anawalaumu Clouds, ila akae akijua huo mwanzo tena hizi online media ndio zitamfanyia interviews baba yake kila siku.
 
Ni kweli brother lakini mtoto wako ni wako tu na hana hatia ,

ni sawa kujiweka pembeni kwa muda Ila kama mtoto akikutafuta au kukuonesha kukuhitaji kama ommy alivyofanya, siamini kama ni sahihi kumuonesha kuwa kwako watoto uliowapata nje ni kitu extra, sio vyema 🙏🙏
 
Mama wa ommy Dimpoz alifariki ommy ukiwa mdogo sana primary school. Huyu baba hakutokea msibani japo kumpa faraja mwanae, wala hakuwahi kumtafuta mwanae kujua anaishi au amekufa
Sorry! Naomba kuuliza Mama D! Wwe na Ommy ni ndugu au ni mtu na Mpenzi wake!!?
 
Kuna wakati una zaa na mwanamke.unajuta kuzaa nae.kuna sababu nyingi sana za mwanaume kukataa mtoto.
Hizi excuse tu, mtoto hakuwaomba umzae mlimzaa kwa starehe zenu sasa kwanini eti ugomvi baina yenu umtelekeze. Yaani, lets assume kulikuwa hakuna maelewano baina ya baba na mama, sasa kwanini hakumtafuta mwanae hata baada ya mama kufariki?
Wanaume tuache janja janja tulee watoto na nazungumza kutokana na experience maana mimi ni mmoja ya watu waliozaa na mtu halafu tukazinguana ila mpaka leo namlea mtoto kama baba na mama yake akiwa mbali na nimegundua ni jinsi gani malezi ni gharama na si jambo jepesi.
 
Kama ni Mzazi tapeli, mbona Ommy anatumia saa name yake toka kitambo tu!! Si ndiyo huyo Mzee Nyembo!!??
Jina jina tu hakuna cha zaidi linachompa. Mzee alitelekeza mtoto huku akijua yupo, basi na yeye atulie apitie kile ambacho alimpitisha mwanae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…