Kwa hili la Ommy Dimpoz na Babake wee uliye biological mother/father ukimkataa/kumtelekeza mtoto wako ujue umemuumiza sana kisaikolojia na makuzi yake

Kwa hili la Ommy Dimpoz na Babake wee uliye biological mother/father ukimkataa/kumtelekeza mtoto wako ujue umemuumiza sana kisaikolojia na makuzi yake

Kuna braza mmoja anaitwa Godson(fake name). Alizaliwa kwa mwanamke flani ila baba wa Godson akatengana na huyu mama, G akiwa na miaka 2 na baada ya miaka 4 akaja kuoa mke mwingine na akamchukua God kulelewa na huyu mama mpya. Hapo God alikua kafikisha miaka 10. Bimkubwa mpya alimlea ila ndo obvious watu wanaona huyu mtoto si wa huyu mama wa kumzaa.

Baba hana muda yeye yuko busy anatafuta maisha. Braza G akawa busy analisha mbwa, kwenda kutafuta vyakula vya mbwa saa zingine mbali kweli kweli. kupika hapo ndani ni yeye. (mama alikuwa mfanya kazi). Kuna uonevu ulikuwepo kimtindo na majirani wakawa hawampendi yule mama. Kosa kidogo G atapigwa kinyama ila wadogo zake wawili fresh tu.

G maisha akaenda nayo adoado akaja kuhama kujitegemea maana alikua mkubwa kidogo. Mshua akafariki. Mama akajitenga na G kabisa. G akastruggle kama mwanaume. Hamadi mama nae akaja kufariki huku wale watoto wawili bado hawajaweza kujitegemea. Familia ya marehemu mume hawakutaka kujihusisha na chochote maana kipindi mume yuko hai, bimkubwa alikuwa anamjaza sumu sana mzee kiasi kwamba akawa kama amejitenga na nduguze. Na vile habari zilifika kwa aliokuwa anamfanyia G mpaka G kuondoka akiwa mdogo basi ndo ndugu hawana muda.

G kuona vile akawachukua wadogo zake. Mkubwa wa kiume wa mwisho wa kike. Akawasomesha mpaka wote wamemaliza chuo na leo wana maisha yao mazuri kiasi. G yuko na familia yake. Kila mtu anamshangaa G jinsi alivyokua na moyo mzuri.

My take: Humjui nani ni nani atakaekuja kuwa msaada kesho. Baba zetu nauliza tu..sawa mama anaweza kuwa alikuwa mkorofi na kisanga lakini hata kuwajulia hali watoto ulishindwa?? Au hata pesa za matumizi??
My brothers una watoto.somewhere nje huko...provide aisee. Haijalishi mama mtoto ni chenga kiasi gani. Penda uzao wako. Uthamini. Labda bado mdogo ngoja niendelee kukua.

Na ewe dada uliezaa na mwanaume flani and he is not your husband labda, acha kumfeed mtoto maneno ya uongo kisa una kisasi na baba yake. Unajua fika jinsi baba anavyojitahidi kumsogeza mwanae karibu. Akimchukia utakuja kujibu mbele za Mungu maana ukute wewe ndo bakahehe. Na wengine tunatumia watoto kama kitega uchumi afu kutwa kuwananga wanaume mitandaoni. Be rational in your actions everybody.
 
Upendo wa mtoto unajengwa na wazazi. Sasa kama wewe hukumfundisha mwanao upendo halafu unataka kupendwa utasubiri sana

Tunawaona watoto ambao wanafanikiwa na kuwasaidia wazazi wao na kuelezea vile wazazi walivyowapenda na kuwalae hata katika hali za umaskini wao

Huyu mzee faraj ni Kati wa wababajina, na wanaume katili
Asante kwa mchango wenye mashiko
 
Mama yake alifariki akiwa la pili alimezeshwa lini hizo sumu acheni kutteea upuuzi
Omy hajakosea popote
Umemsikia anachokisema ommy mwenyewe lakini au umekuja kujibu tu hoja bila kufuatilia...
Haya ni sawa alikufa akiwa la pili je hayo anayoyasema aliyajuaje kama alikuwa mtoto mdogo asiyeelewa na hajui lolote...be Sirius....
 
Kwa nini Wanaume wengi mnapenda kujitetea kwa kipengele hiki cha chuki kupandikizwa,mkuu umesikiliza Ommy alivyoelezea alipokuwa anamuuliza marehem Mama yake alimueleza kwamba baba yako amesafiri iko siku atarejea (hapa na mpongeza huyo mama alionesha ujasiri mkubwa) kitendo hiki kilisababisha Ommy ajiulize why baba yake hakutokea hata siku ya msiba.

Hakuna chuki hapo sio kila Mwanamke ni mjinga
Kuna mmoja kasema ommy alikuwa la pili ko hakuwa anajua lolote ko hizo sumu hakumezeshwa...na wewe nakuuliza ikiwa mama yake alimjibu hivyo ye anamchukia kwa nini sasa....its very simple....nilikuwa safarini ndio nimerudi so why hates
 
Tusishabikie utelekezaji wa watoto

Mama ommy alifariki ommy akiwa primary school. Fikiria wewe ni baba wa aina gani hata pamoja na mzazi mwenzio kufariki hushughuliki wala hujali kumtafuta na kumtunza mwanao katika umri huo mdogo!?

Haya mwanae kasema japo hawajawahi kuwa na ukaribu heshma yake kama baba inabaki palepale. Kuna nini cha ziada ya heshma?

Heshma yashinda mali na ommy anampa heshma; unaweza kuonewa kila kitu kwa kudharauliwa
Hii naona ishakuwa vita ya wazazi wa kike na kiume
Hata hivyo baba ommy hajaomba chochote kwa ommy na wala hana haja na chochote .kilichoibua huu mjadala ni media tu ili kutaka public attention....yuko bize anaendesha Bajaj zake na hana habari na mtu....ninachompenda huyu mzee hana maneno mengi lakini fahamu nyuma ya ukimya wake kuna mambo mengi kayazuia...kaongea ommy mmemuamini na je akiongea huyu mzee mtamuamini nani...
 
Ni kweli....na kwa kuongezea wale ambao hawajawahi ku experience hii situation watamuhukumu baba ommy moja kwa moja but kwa tulioishi ndani ya hali kama hii tunaelewa nini kinaendelea
 
Kuna mmoja kasema ommy alikuwa la pili ko hakuwa anajua lolote ko hizo sumu hakumezeshwa...na wewe nakuuliza ikiwa mama yake alimjibu hivyo ye anamchukia kwa nini sasa....its very simple....nilikuwa safarini ndio nimerudi so why hates
Ni video ipi Ommy ametamka ana mchukia baba yake mkuu?
 
Hii naona ishakuwa vita ya wazazi wa kike na kiume
Hata hivyo baba ommy hajaomba chochote kwa ommy na wala hana haja na chochote .kilichoibua huu mjadala ni media tu ili kutaka public attention....yuko bize anaendesha Bajaj zake na hana habari na mtu....ninachompenda huyu mzee hana maneno mengi lakini fahamu nyuma ya ukimya wake kuna mambo mengi kayazuia...kaongea ommy mmemuamini na je akiongea huyu mzee mtamuamini nani...

Hili ni kwa wazazi wote wa kike na wa kiume. Ukitelekeza mtoto wakati hajiwezi hajielewi anakuhitaji hakikisha na wewe unaendelea kujitelekeza akishakuwa akaweza kusimama, kujihudumia na kutambulika na dunia

Halafu wewe nawe Lazima uko kwenye chama cha wanaotelekeza mimba na watoto wewe

Ni kweli....na kwa kuongezea wale ambao hawajawahi ku experience hii situation watamuhukumu baba ommy moja kwa moja but kwa tulioishi ndani ya hali kama hii tunaelewa nini kinaendelea
Nakuona baba ommy unavyopambana kujitetea. Huu muda umeshaambiwa unaheshimiwa kama baba mshukuru Mungu mwanao hajakukana amekuheshimu kama sperm donor, sasa kaa kwa kutulia na kupambana na hali yako
 
Baba alifanya kwa starehe kama wengine wanavyofanya chukuria starehe,alimyetekeza mtoto coz akuwa na na ya mtoto so na yeye atelekezwe tu
hauleweki vizuri lakini una pointi ya muhimu sana

hahahhahaha
 
Mtt mwenyewe kama ndio huyo tetesi zinadai mke wa mtu huko Mombasa mm ningesema hewala
 
Mtt mwenyewe kama ndio huyo tetesi zinadai mke wa mtu huko Mombasa mm ningesema hewala

Kumbe ni TETESI tuu!?

Halafu hata kama ni kweli bado huyo mzee atakua ndio sababu!

Acheni ommy aseme ataendelea kumheshimu ila ukaribu nae hana sababu hamjui madhara ya kutelekezwa kwake yamempeleke kupitia mswahibu gani tangu utotoni hadi sasa
 
Hili ni kwa wazazi wote wa kike na wa kiume. Ukitelekeza mtoto wakati hajiwezi hajielewi anakuhitaji hakikisha na wewe unaendelea kujitelekeza akishakuwa akaweza kusimama, kujihudumia na kutambulika na dunia

Halafu wewe nawe Lazima uko kwenye chama cha wanaotelekeza mimba na watoto wewe

Nakuona baba ommy unavyopambana kujitetea. Huu muda umeshaambiwa unaheshimiwa kama baba mshukuru Mungu mwanao hajakukana amekuheshimu kama sperm donor, sasa kaa kwa kutulia na kupambana na hali yako
Mtoto hawezi kuwa fimbo ya kunichapia kamwe,nina maana gani?kama mzazi mwenzangu anashindwa kuniheshimu na kila ninachotoa kinaonelana sio kitu na bado mtt analishwa maneno mabaya kuhusu mbaya zaid yote anayoelezwa sio ya kweli basi acha iwe hivyo wala sitahitaji msaada wa huyo mtt,mnatetea huyo Ommy dimpoz bila kusikiliza upande wa baba yake,Yaan nikonaga situation kama hii then nikimfikiria mzazi mwenzangu najisemea hawa hawaelewi tuu,ila uzuri nilishamwambia mtt huyo ni mama yako na ww ni mwanaume ukikua utajua kwanin niliamua kukaa mbali
 
Kumbe ni TETESI tuu!?

Halafu hata kama ni kweli bado huyo mzee atakua ndio sababu!

Acheni ommy aseme ataendelea kumheshimu ila ukaribu nae hana sababu hamjui madhara ya kutelekezwa kwake yamempeleke kupitia mswahibu gani tangu utotoni hadi sasa
Nyie ndio sababu ya wanaume kutelekeza watoto,acheni kuficha tabia zenu mbovu kwenye migongo ya watoto kwa kigezo cha baba hajawajibika
 
Mtoto hawezi kuwa fimbo ya kunichapia kamwe,nina maana gani?kama mzazi mwenzangu anashindwa kuniheshimu na kila ninachotoa kinaonelana sio kitu na bado mtt analishwa maneno mabaya kuhusu mbaya zaid yote anayoelezwa sio ya kweli basi acha iwe hivyo wala sitahitaji msaada wa huyo mtt,mnatetea huyo Ommy dimpoz bila kusikiliza upande wa baba yake,Yaan nikonaga situation kama hii then nikimfikiria mzazi mwenzangu najisemea hawa hawaelewi tuu,ila uzuri nilishamwambia mtt huyo ni mama yako na ww ni mwanaume ukikua utajua kwanin niliamua kukaa mbali

Na kwanini tangu mzazi mwenzio afe mtoto akiwa primary school standard2, hadi mtoto kawa mwanaume mtu mzima wewe kama baba hukumtumtunza!? Au ulikua unamtumia marehemu mama yake kama fimbo ya kumchapia mtoto?
 
Nyie ndio sababu ya wanaume kutelekeza watoto,acheni kuficha tabia zenu mbovu kwenye migongo ya watoto kwa kigezo cha baba hajawajibika

Wewe utaamua mwenyewe kusimama kwenye nafasi yako kama mwanaume na baba kwa mwanao. Au utaendelea na kurushiana maneno na watu😅😅 ila ujue mwisho wa siku utapata heshma yako kama sperm donor
 
Na kwanini tangu mzazi mwenzio afe mtoto akiwa primary school standard2, hadi mtoto kawa mwanaume mtu mzima wewe kama baba hukumtumtunza!? Au ulikua unamtumia marehemu mama yake kama fimbo ya kumchapia mtoto?
Hapo ss kama mama alifariki jamaa akiwa mtt mdogo mzee alifanya makosa kumsusa,hapo mzee alichemsha
 
Back
Top Bottom