Kwa kauli hii ya Rais Samia, Jaji Biswalo anapaswa kujiuzulu haraka

Kwa kauli hii ya Rais Samia, Jaji Biswalo anapaswa kujiuzulu haraka

Leo Januari 31, 2023 Rais Samia amezungumzia suala la Plea Bargain, utaratibu wa Makubaliano ya Kumaliza Kesi kwa Kulipa Fedha kwa Serikali ambao ulitumika wakati wa Utawala wa Hayati Rais Magufuli chini ya DPP Biswalo Mganga aliyeondolewa na kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu, huku akieleza kuwa Suala hilo limekuwa na utata ikiwemo baadhi ya pesa zilizolipwa kwenye akaunti zimeoneka kupelekwa Nchini China.

Ukiachana na hilo Jaji Biswalo amekuwa kwenye kashfa nyingi ikiwemo kuchukua mali za washtakiwa bila utaratibu wenye uwazi, bila uwepo wa sheria na akaunti maalumu ya Serikali inayokusanya fedha hizo.

Sasa kwa hili la leo, Jaji Biswalo anasubiri nini kuachia nafasi hiyo kuonesha Uwajibikaji? Lakini Pia, Rais Samia anasubiri nini kuunda Tume ya Majaji watatu wanaotakiwa kuchunguza suala hilo na kutoa uamuzi wa nini Rais afanye?

Anyway Taifa linasubiria ripoti ya matumizi ya fedha zaidi ya Tsh. Bilioni 50 zilizotokana na makubaliano ya washtakiwa na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS), Rais Samia Suluhu Hassan amesema ofisi hiyo ilipitia kipindi ambacho kuna michezo ilikuwa inafanyika ambayo iliharibu taswira ya taasisi hiyo.
Hawez kujiuzulu kwasababu aliyemteua walikuwa pamoja
 
Kabla ya ripoti ya uchunguzi kutoka mnatoaje hukumu kwamba pesa iliibwa?

NCHI hii imeanza Kuwa ya mihemko na mauzushi.

Wananchi wenye hasira Kali wameanza kuibuka wanaua mpaka watu wasio na hatia
Bar mad mmoja kapiga kelele za Mwizi Kwa mteja aliyeshindwa kulipa wamemuua hivi kosa la Kushindwa kulipa bill ya bia ADHABU yake ni KIFO?

Wananchi wamesambaziana uongo kwamba Kuna Bibi amekamatwa na misukule Wananchi wamevamia Kituo cha Polisi wanataka kuua.!

Hii sijui ndiyo Uhuru wa kufanya mikusanyiko na maandamano iliyokuwa inasubiriwa Kwa hamu!

Bibi mwingine amekamatwa na watoto watatu ambao kunakila dalili kwamba alikuwa anawatesa wakati utaratibu wa kisheria unaendelea Wananchi wanamtaka huyo Bibi ili wamuue!

Haitofautiani Sana hizi TUHUMA hivi kweli Yule Marehemu angeruhusu pesa iende China wakati Kwanza hakuwa na muda wa kujikomba Kwa wazungu
na mataifa yote ya kigeni ikiwemo China.

Miamala yote ya fedha aliiweka kiganjani watu walivyokuwa wanamuogopa wasingethubutu kucheza na pesa ya NCHI Chini ya mwendazake pamoja na mambo mengi ambayo wengine walichukilia kama ukatili Kwa kadri walivyoona lakini kwenye eneo la udhibiti wa pesa ya Umma Yule Mzee tumuache apumzike Kwa Amani.
Plea bargaining Ilikuwa inafanywa na Mahakama DPP alikuwa ni mwendesha mashtaka tu MAAMUZI yote ni ya Mahakama na Jambo lolote ambalo Mahakama itakuwa imeamua na kama hukuridhika DAWA yake ni kukata rufaa na si vinginevyo.
 
Nimemsikiliza sana mama na kwa maelekezo ya mama lile ni agizo inatakiwa TAKUKURU na Jeshi la Polisi wamkamate dpp aliyemaliza muda wake ndugu biswalo, awe chini ya ulinzi huyu mtu aliwaumiza watu wengi sana kupitia ofisi yake.

Huyu mtu DPP alijigeuza Mungu kwenye Ile ofisi hata hizo pesa walizokuwa wanatozwa akina Seth, ili waachiwe yeye ndiye alikuwa kinara, aliweka wafanyabiashara mahabusu kwa kuwasingizia kesi za uhujumu bila sababu ili ajipatie pesa, kama kweli mama umeamua kuisafisha nchi huyu hatakiwi kabisa kuwa uraiani!
Watu wengi waliumizwa na kuporwa, kinachotakiwa ni tume ya Ukweli na maridhiano, vinara ni Kuna Bwisalo
 
Siyo kujiuzulu, anatakiwa atiwe pingu yeye pamoja na binamu wa Mrundi Dotto James
Umaskini ndio unakufanya unalialia hivi. Ungekua tajiri wala usingelia hivi. Tafuta pesa uondoe aibu
 
Na makamu wa kipindi hicho aliamua tu kuendelea kula mshahara na kusubiri Pension yake huku anajua yanayofanyika hayaendani na haki ?

Yaani na Kampeni akapiga kabisa ili watu waendelee kunyimwa haki....., mambo mengine ukiyaangalia vizuri unaona chembe chembe za unafiki....
 
Mama huwezi jisafisha wakati naye alikuwa kwenye hilo hilo jahazi. Kiongozi makini alipaswa awe amesha jiuzulu zamani.

Yeye kuendelea kukaa hapo, na hao waliofanya haya madudu kuendelea kuwateua ni ishara kwamba yeye kiongozi anabariki hayo madudu.

Kulialia na kutafuta sympathy hakuta msaidia, ni heri akae kimya sio kusema halafu huwa uwezo wa kuchukua hatua. Watanzania sio wajinga.
Asiposema sasa hivi, tutayasikia kwenye mikutano ya hadhala. Ndio mjue kwa kwa nini Magufuri aliikataa.
 
Huyu maza ngoja nimtetee Kwa hili , kipindi cha Marehemu gaidi huyu maza hakua na nguvu yeyote ndio maana kuna kipindi alitaka hata kujiuzulu ila alipigwa biti.

Wacha tu nae ateme nyongo.
Ila Kwa mitazamo wangu maza inabidi mambo mengine ya hovyo yaliyofanyika kipindi cha Mwenda zake awe anayafanyia kazi kimyakimya bila kutaarifu umma kwani ni kama analeta taharuki na kuongeza kinyongo Kwa wananchi.

Namshauri wote waliofanikisha madhambi hayo awawajibishe kimya kimya
Aseme ndio nafuu yake, akikaa kimya, ikaja kuvuja kwa Mwamba Lisu akaitoa itakuwaje. Angalau likiongelewa baadae linajulikana. Tutasikia mengi ndio faida ya vyama vingi huru. Magufuri aliziba midomo ili afanye yake!
 
Mama huwezi jisafisha wakati naye alikuwa kwenye hilo hilo jahazi. Kiongozi makini alipaswa awe amesha jiuzulu zamani.

Yeye kuendelea kukaa hapo, na hao waliofanya haya madudu kuendelea kuwateua ni ishara kwamba yeye kiongozi anabariki hayo madudu.

Kulialia na kutafuta sympathy hakuta msaidia, ni heri akae kimya sio kusema halafu huwa uwezo wa kuchukua hatua. Watanzania sio wajinga.

Wapemba hawana akili
 
Tanzania ni nchi maskini Ila wapo matajiri, jitahidi uwe mmoja wao.
Maisha sio utajiri masikini wengi wanaamini ukiwa tajiri ndio maisha kumbe ni kawaida tuu...ila wengi waliokulia kwenye umasikini wakabahatika kupata Elimu kidogo na kuendelea na poverty circle of life wanaamini wao washatoka kumbe bado wapo kwenye mfumo wa umasikini...
 
Kama unaumia chomowa.
Mimi naumia au wewe ndio unaumia? Mimi toka lini nikalialia kwa mtu mwenye pesa. Umaskini wako ndio unakufanya ulielie Sana, hii ni awamu ya 6 ni awamu ya kutafuta pesa sio ya kulalama.
 
Maisha sio utajiri masikini wengi wanaamini ukiwa tajiri ndio maisha kumbe ni kawaida tuu...ila wengi waliokulia kwenye umasikini wakabahatika kupata Elimu kidogo na kuendelea na poverty circle of life wanaamini wao washatoka kumbe bado wapo kwenye mfumo wa umasikini...
Umeandika kwa hisia sana, solution ya haya yote ni utajiri tu. Unafikir kuna tajiri atakaa analialia hapa Kama wewe? Ongeza bidii za kutafuta pesa dogo ukikutana na wajinga wapige, dunia haina huruma
 
Back
Top Bottom