Kwa kauli hii ya Rais Samia, Jaji Biswalo anapaswa kujiuzulu haraka

Kwa kauli hii ya Rais Samia, Jaji Biswalo anapaswa kujiuzulu haraka

Mama huwezi jisafisha wakati naye alikuwa kwenye hilo hilo jahazi. Kiongozi makini alipaswa awe amesha jiuzulu zamani.

Yeye kuendelea kukaa hapo, na hao waliofanya haya madudu kuendelea kuwateua ni ishara kwamba yeye kiongozi anabariki hayo madudu.

Kulialia na kutafuta sympathy hakuta msaidia, ni heri akae kimya sio kusema halafu huwa uwezo wa kuchukua hatua. Watanzania sio wajinga.
Akijisafisha chawa wataishi vipi? Yeye anawapa WaTz jambo la kuwashughulisha tu, hana la zaidi.
 
Nimemsikiliza sana mama na kwa maelekezo ya mama lile ni agizo inatakiwa TAKUKURU na Jeshi la Polisi wamkamate dpp aliyemaliza muda wake ndugu biswalo, awe chini ya ulinzi huyu mtu aliwaumiza watu wengi sana kupitia ofisi yake.

Huyu mtu DPP alijigeuza Mungu kwenye Ile ofisi hata hizo pesa walizokuwa wanatozwa akina Seth, ili waachiwe yeye ndiye alikuwa kinara, aliweka wafanyabiashara mahabusu kwa kuwasingizia kesi za uhujumu bila sababu ili ajipatie pesa, kama kweli mama umeamua kuisafisha nchi huyu hatakiwi kabisa kuwa uraiani!
Upo sahihi sana.
Kama boss wa PCCB angekuwa yupo huru na ni mtu mweledi na mwenye hofu ya Mungu, kauli hiyo ya Mh. Rais SSH ilipaswa kuwa agizo kwake la kuhakikisha huyo Biswalo anakuwa kwenye mikono salama akifanyiwa uchunguzi.
 
Kabla ya ripoti ya uchunguzi kutoka mnatoaje hukumu kwamba pesa iliibwa?

NCHI hii imeanza Kuwa ya mihemko na mauzushi.

Wananchi wenye hasira Kali wameanza kuibuka wanaua mpaka watu wasio na hatia
Bar mad mmoja kapiga kelele za Mwizi Kwa mteja aliyeshindwa kulipa wamemuua hivi kosa la Kushindwa kulipa bill ya bia ADHABU yake ni KIFO?

Wananchi wamesambaziana uongo kwamba Kuna Bibi amekamatwa na misukule Wananchi wamevamia Kituo cha Polisi wanataka kuua.!

Hii sijui ndiyo Uhuru wa kufanya mikusanyiko na maandamano iliyokuwa inasubiriwa Kwa hamu!

Bibi mwingine amekamatwa na watoto watatu ambao kunakila dalili kwamba alikuwa anawatesa wakati utaratibu wa kisheria unaendelea Wananchi wanamtaka huyo Bibi ili wamuue!

Haitofautiani Sana hizi TUHUMA hivi kweli Yule Marehemu angeruhusu pesa iende China wakati Kwanza hakuwa na muda wa kujikomba Kwa wazungu
na mataifa yote ya kigeni ikiwemo China.

Miamala yote ya fedha aliiweka kiganjani watu walivyokuwa wanamuogopa wasingethubutu kucheza na pesa ya NCHI Chini ya mwendazake pamoja na mambo mengi ambayo wengine walichukilia kama ukatili Kwa kadri walivyoona lakini kwenye eneo la udhibiti wa pesa ya Umma Yule Mzee tumuache apumzike Kwa Amani.
Plea bargaining Ilikuwa inafanywa na Mahakama DPP alikuwa ni mwendesha mashtaka tu MAAMUZI yote ni ya Mahakama na Jambo lolote ambalo Mahakama itakuwa imeamua na kama hukuridhika DAWA yake ni kukata rufaa na si vinginevyo.
Maandishi yako yanasomeka kuwa hakuna pesa ya "p-b" iliyopelekwa China!!?

Alichosema Mh. Rais umekisikia kwa masikio yako na kukielewa kwa akili zako!!???

Unajua hitimisho la maandishi yako yanasomeka kuwa namba moja hakusema ukweli!!???
 
Na makamu wa kipindi hicho aliamua tu kuendelea kula mshahara na kusubiri Pension yake huku anajua yanayofanyika hayaendani na haki ?

Yaani na Kampeni akapiga kabisa ili watu waendelee kunyimwa haki....., mambo mengine ukiyaangalia vizuri unaona chembe chembe za unafiki....
Unafiki ndicho kitu pekee ambacho watanzania tunakifanya kwa uwezo mkubwa sana.

Makamu wa kipindi hicho ku "table" barua ya kuachia ngazi na kukataliwa na vitisho juu,ulitaka nini afanye mbele ya shetani yule!!??
 
Unafiki ndicho kitu pekee ambacho watanzania tunakifanya kwa uwezo mkubwa sana.

Makamu wa kipindi hicho ku "table" barua ya kuachia ngazi na kukataliwa na vitisho juu,ulitaka nini afanye mbele ya shetani yule!!??
Kwahio Commander in Chief wa sasa ni mwoga na kwa kuogopa vitisho anaweza akafanya na kukubali chochote kile ?

Kwahio vitisho vya sasa vya mataifa mbalimbali anafanyaje ? Tuache ku-defend the indefensible....
 
Kwa kauli hiyo ilitakiwa awe ashavuliwa viatu sio yupo nyuma ya Nondo akisaidia kutoa ushahidi..
 
Back
Top Bottom