Kwa kauli hii ya Rais Samia, Jaji Biswalo anapaswa kujiuzulu haraka

Si wengibe wanapewa teuzi au?
Kwa maoni yangu, mtu akiteuliwa na Raisi ina maana ni 'mtakatifu' wa zama husika.
 
Alishawateua kabla hajajua, kajua baada ya kuwateua. Na ndo maana anataka unda hata Tume ya kufatilia Mambo ya nje kuona kama hao watu hufaa au hawafai
 
Umeandika kwa hisia sana, solution ya haya yote ni utajiri tu. Unafikir kuna tajiri atakaa analialia hapa Kama wewe? Ongeza bidii za kutafuta pesa dogo ukikutana na wajinga wapige, dunia haina huruma
Ushauri mzuri mkuu wacha nifate ushauri wako ingawaje unaweza ukawa wa kitura pia..
 
Ushauri mzuri mkuu wacha nifate ushauri wako ingawaje unaweza ukawa wa kitura pia..
Huo ushauri ndio muhimu kuliko hivi vilio vyenu. Umeanza kulialia toka epa, ukaja Richmond, Mara dowans, Mara escrow, na Sasa unalia plea bargaining, tukiuliza hivyo vilio vyote umepata nini? Wenzako wanaaccumulate wealth ili Watoto na wajukuu wasije kuwa watumwa baadae.

Kosa alilofanya baba yako na wewe unataka kulifanya. Tafuta pesa
 
Ajiuzulu aende wapi

Hawezi kujiuzulu huyo

Ova
 
Ukiwa tajiri ukazungukwa na maskini 10 ni rahisi na wewe kuwa maskini.

Lakini maskini mmoja ukizungukwa na matajili 10 ni rahisi na wewe kuwa tajiri.

Ukitaka mafanikio ya kweli Tanzania usiishi na jamii yako au sehemu uliyozaliwa na kukuulia, hili ni tangu enzi za mitume ni lazima Utoke.
 
Yule zimwi magu alikuwa mwizi sana na alitisha, SAMIA angefanyaje pale
Samia alisharesign, wazee ndio wakaingilia kati, alishashindwa kufanya kazi na mgonjwa wa akili na kufokewa kama mtoto Mdogo wakati kwenye uchaguzi mmeomba wote kura.
 
Yaani hilo jitu linafaa lipelekwe Ukrain afu awekwe front line walahi [emoji35]
 
Hata Magufuli aliamini ana kinga anaweza kuuwa watu atakavyo.

Sasa leo mwenye kinga analiwa na funza Tundu Lisu yuko mzima wa afya.
Ndio maana walikimbilia jiwekea Kinga
Kuanzia Spika hadi Jaji
 
Kama ushahidi upo, wahusika wote wanatakiwa wakamatwe, wafungwe.

tatizo la Tanzania, wengine wenye ubavu wakiiba hawafanywi kitu, wezi wadogo wadogo wa kuku na bata mzinga, wanakamatwa, wanamwagiwa mafuta ya taa na kupigwa kibiriti.
 
Mzigo wote mtupie msukuma ndio inadhihirika lawama we rusha kwa mfu tu wote wataitikia anhaa ndio maana, anayeelekezewa tuhuma hawezi kujibu.
Ila kipo kiama
Nimekuelewa saana,mama bado tu hajarizika na kifo cha jpm,sijui anataka mpk amfanyaje,!?
 
Hii nchi kuna siku inakuja,patachimbika,Huyu mama anafikir taifa hili ni la wajinga woote,
 
Kwa shutuma za wizi wa fedha za plea bargaining zilizotolewa na amiri jeshi mkuu mheshimiwa Samia, sikutegemea Biswalo hadi leo awe hajatoka hadharani na kutangaza kujivua nyadhifa zake zote.

Lakn kwa kuwa watanzania na viongozi wetu wamejenga utamaduni wa kusifia wezi na mafisadi Biswalo anaonekana mjanja na ndiyo maana bado yupo ofisini mpk Sasa.

Biswalo jisikie aibu na uachie ngazi tafadhali.
 
Sasa Biswalo atajiuzulu vipi wakati aliyemteua kuwa jaji ni huyo huyo Samia?

Ina maana Samia alivyomteua alikuwa hajui haya madudu?

Samia ana nia ya kweli ya kufanya mabadiliko?

Au ameanza kampeni za 2025 mapema tu?
 
Nani alimpa ujaji?
 
Sasa Biswalo atajiuzulu vipi wakati aliyemteua kuwa jaji ni huyo huyo Samia?

Ina maana Samia alivyomteua alikuwa hajui haya madudu?

Samia ana nia ya kweli ya kufanya mabadiliko?

Au ameanza kampeni za 2025 mapema tu?
Tatizo huko juu kila mtu mchafu...

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…