Usiku ule tuliwaamini na wakatupa mgonjwa wetu tuondoke naye wakasema shida sio kubwaKwa hio mkaamua kuhamisha magoli si ndio mkuu?
Mjini hapa best..!Hivi dudubaya amepata wapi hela.ya kwenda India?
Aisee pole sana kamanda. Pole sana.Baada ya mke wangu kujifungua mtoto wa pili ziwa moja likaanza kumuuma anaponyonyesha,
Tukaenda kwenye hospitali moja ya serikali,
Wakampima na kumpa dawa azitumie kwa siku 30 kisha turudi tena
Lakini kutokana na maumivu ilibidi mke wangu asitishe kumnyonyesha mtoto, maana pia lile ziwa lilianza kuvimba,
Tukarudi hospitali na kuwaeleza, tukawaambia pia kuwa ziwa lina uvimbe,
Doctor akamcheki tena, akatuuliza bado unanyonyesha? Tukamwambia hapana,
Akasema hiyo ni hali ya kawaida ikiwa utasitisha unyonyeshaji ghafla, akatufafanulia kuwa kuna tezi za maziwa zinaweza kuvimba kwa sababu mtoto hanyonyi, tukapewa dawa na tukaambiwa turudi tena baada ya kumaliza dawa,
Ziwa likazidi kuvimba, tukaenda hospitali binafsi, wakampima upya, wakakata kinyama kwenye ziwa la mke wangu kwa ajili ya vipimo,
Tukaambiwa turudi baada ya wiki mbili,
Tuliporudi tukaambiwa mke wangu ana saratani ya ziwa stage 2 na inaelekea 3, tukaanza matibabu ya saratani haraka, tuliandikiwa tuende KCMC moshi, tukauguza hapo for almost 2 years, akapata nafuu tukarudi nyumbani,
Baada ya muda ikarudi tena, tukarudi kcmc, akatibiwa hapo kwa miezi nane na akafariki hapo , sijui wa kumlaumu hapo, japo moyo wangu haujawahi kupona kabisa, nadhani sekta ya afya kwa nchi hii ina shida kubwa, nakumbuka doctor aliyetupima kwenye hospitali ya serikali tulimkuta tena kwenye hospitali hiyo ya binafsi na akatuhudumia tena.
Duh kwani wengine mnapata wapi hela ya kwenda India?Hivi dudubaya amepata wapi hela.ya kwenda India?
Mkuu naomba majina ya hospital nzuri unazoenda kufanya vipimo vya mama kwa manufaa yetu ukiacha hizo gost hospital 🙏Kuna hospital nilipimwa nikaambiwa nina UTI ni ya serkali dawa nikapewa za ugonjwa huo. Vile nafika home ninywe ile dawa nikaona emexpire miezi2 iliyopita!
Daah nikasita kwa sababu nilipewa dawa zaidi ya 3 nikaziangalia zote zime expire asee isipokuwa panadol tu ndo ilikuwa ina expire mwaka ujao!
Nikafikiria hapa huenda hata siumwi UTI kama dawa tu zime expire vipi vipimo vyao hawa?
Nikaenda hospital ya Agakhan nikacheki kila kitu wakaniambia nina typhoid na minyoo. Nikapewa dawa nikatumia nikapona.
Issue ya dawa nilizipeleka zile dawa kwenye ile hospital aliyenipa akashituka kama kapigwa short ya umeme badae akaanza kuangalia nilichoona karibia dawa zote zilikuwa muda wake umeisha!
Mama anaumwa kisukari tulipewa dawa ambazo angemeza basi angekufa kama sio za kisukari basi pressure ingepanda na kufa.....yani kwa ugonjwa wake hakutakiwa atumie kabisa zile dawa bahati nzuri huwa nina kawaida ya kushare kila aina ya dawa tunayopewa kwa ajiri ya matibabu ya mama hasa nikiwa naye mimi kwenye matibabu.
Ndg yetu mmoja wa damu kwenye group yeye ni Dr akasema hizo dawa msimpe msimpe msimpe kabisa ni hatari na atakufa!
Kwa msisitizo huo nikazipiga picha nikamuuliza chatgpt akanifafanulia kwa uzuri mno.
Nikaona haitoshi kuna Dr mwingine nikamtumia nikimwambia "Mama leo tulienda nae clinic tumepea dawa hizi nikazipiga picha nikamtumia maana anajua ugonjwa wa mama" dk0 akanipigia akaniambi mmeshampa akatumia nikamwambia hapana akasema umsimpe tupa kabisa hizo dawa mama hazimfai!.
Mama huyu huyu alichomwa mwiba akawa na kidonda ila kilikuja kupona kabisa miezi kama 3 pakaanza kuuma hapo alipochomwa ule mwiba tukaenda hospital moja ya serikal tukaambiwa tuende kwenye kipimo kiitwacho Dopler ultra sound (sijui kama nimepatia kwa usahihi)
Tukaenda kupima jamaa akatuambia mguu umeoza ukatwe tu. Mama akagoma mnoo sema sisi tiyri tulikuwa tumekubali kuwa akatwe mguu wake.
Na taratibu zingine zilikuwa zimeanza asee ili tumpeleke tu hata kwa nguvu maana alikuwa halali usiku analia kama mtoto japo alikuwa anasema afe tu na mguu wake kuliko kufa nusu nusu!.
Siku moja akaja jamaa mmoja akatuambia tuende kuna hospital moja hivi tukarudie vipimo hii ni baada tu kama ya siku3 kweli nikampeleka kweli alipopima jamaa akasema ..ule mwiba kipindi unamchoma uligusa kabisa kwenye mfupa na ukaacha kama ka ncha fln hivi hivyo akitembea kanagusa nyama na kuitonesha hivyo mama anunuliwe viatu fulani hivi vyenye sponge akatoa na maelekezo kwa kina sana.
Akatupa na dawa za kusaga ule mfupa nk ......hadi leo hii mama kuhusu hiyo shida kashapona kabisa hasemi mguu tena bado tu kisukari ndo tunapambana nacho.
Nilijiuliza kwa maumivu makubwa sana kuhusu huyu Dr aliyetuambia mguu ukatwe asee siku nikimuona basi tu huwa nawaza mengi sana juu yake asee.
Tuweni makini sana na Dr wa bongo na vifaa vyao. Huu uyuhunda ni wakweli kabisa.
Kidokezo: Ikiwa una uoga wa kukaa kwenye sehemu iliyofungwa (clastrophobia), ni vyema kumfahamisha daktari mapema. Wanaweza kukupa dawa ya kutuliza au kutumia mashine ya "Open MRI" ikiwa inapatikana.
Eti headphone kama DJ huyu jamaa kila nikimsikilizaga lazima nicheke staili yake ya kutoa madini.Inahuzunisha sana maelezo aliyotoa gwiji na mhasisi wa bongo fleva Godfrey Tumaini Dudu Baya vipimo alivyofanya Muhimbili kuwa siyo sahihi na uhalisia.
Anasema asingeenda India angepooza milele.
Katumia dollar elfu 20 kufuata matibabu India.
Msikilize zaidi hapo chini kwenye Video.
View attachment 3556025
Siku nyingine tutazima ujifieAnachoongea ni kweli...na ni hosp karibu zote TZ mashine used.
Mi yalinishinda...niliingizwa kwenye hyo mashine ya MRI baada ya dk 30 nikaanza kusumbua wakanito.,
Muwe na shukurani kwa kazi kubwa iliyofanywa na Serikali ya CCM tangia kupata uhuru wa Taifa letuNchini Tanganyika tunafanyiwa mambo ya kipumbavu sana. Watu wengi wanakufa kwa sababu ya matibabu mabovu kwa kutumia mashine zilizokufa na kutupwa huko Ulaya halafu zikaokotwa na kuletwa Tanganyika kwa ajili ya kuwaua raia wasiokuwa na hatia. Inauma na inahudhunisha sana. Hivi ni lini serikali hii ya wakoloni weusi (CCM) itaanza kujali maisha ya raia.
Cc MamaSamia2025 ChoiceVariable Tlaatlaah Ritz Lucas mwashamba Lucas Mwashambwa
Uzembe haunaga D wala A.Una recruit Watu wa D 3 unategemea nini?
Nimewahi andika Uzi wa kupinga huu ujinga ila wapuuzi wakanishambulia.
Haya ndio matokeo Sasa.
Kamanga na bugandoMkuu naomba majina ya hospital nzuri unazoenda kufanya vipimo vya mama kwa manufaa yetu ukiacha hizo gost hospital 🙏
Madaktari ni kama walimu, they don’t take things personally… Na akirudi wanamtibia kama hakijatokea kituMuhimbili hawato mmaind kweli !?