Kwa maelezo haya ya Dudu Baya ukiwa na hela bora ukatibiwe India

Nakusalimu kwa jina la Muungano wa Tanzania Waziri wetu wa AFYA kipenzi cha Watanzania katika mwezi huu mtukufu kabisa wa Ramadan.

Natumaini ujumbe wa Bw. Godfrey TUMAINI a.k.a. Dudubaya au a.k.a. Mamba Twenty Four utakuwa umekufikia huko ulipo kuhusu Mashine zetu za MRI na CT-SCAN Kwamba Serikali mnanunua Second Hand, zinapiga kelele Sana pale zinapohudumia mgonjwa na zinachukua muda mrefu Sana kumchunguza mgonjwa wakati za India hazina kelele na zinatumia dakika 15 tu kumuhudumia mgonjwa.

Pia Dudubaya amezungumzia kuhusu Mashine zetu kutotoa taarifa sahihi kwa lugha nyingine zinadanganya kutoa majibu ya mgonjwa badala ya kutambua tatizo halisi la mgonjwa zinashindwa kufanya hivyo, badala ya mgonjwa kuambiwa anaumwa kichwa ataambiwa anaumwa miguu, na operation itafanyika ya miguu badala ya kichwa - HII NI HATARI SANA KATIKA KARNE HII

Hivyobasi, badala ya kuhangaika na Afisa Kificho wa Teeth katika tasnia ya Sanaa ya Bongo Fleva, Bw. Dudubaya na kuanza kumletea figisu naona Kuna haja ya kufanya mabadiliko chanya pale MOI, maana amesema ni Hospital ya TAIFA ya MOI, piga chini kuanzia DG hadi mkuu wa kitengo cha Radiology Hawa wote wapeleke Nanjilinji hapo weka watu wapya watakaotusaidia sisi wananchi masikini na waliohusika kununua Mashine Mtumba hapo MOI basi TAKUKURU wafanye kazi yao na Mashine Mpya za kisasa muweke kwenye Bajeti ijayo ziweze kununuliwa.

Ni hayo tu
 
Pole mkuu na wengineo wote mliokumbwa na kadhia.
 
Ila inaumiza sana.. Sisi 2024 kama sio kujiongeza tungempoteza ndugu yetu.. Inauma sana.. Kapasuka bandama wao wanasema kateguka nyonga
TEC wanatengewa pesa nyingi na serekali ktk huduma ya afya. Hawana machine.za kisiasa?
 
Kuna foreigner Specialist (kapuni) alimkataa Dr kutoka Hospitali kubwa tu hapa Tz owa sababu anatembea na picha za wagonjwa kwa simu, alimuuliza kwa nini unafanya hivyo alisema " ninakuwa nazo kwenye simu ili nitumie kama reference kwa wagonjwa wakija na kuwaonyesha kuwa huyu kwenye tulimfanyia hivi na hivi na wewe hivyo tutakufanyia" πŸ˜‚
Huyu Dr ni mkubwa na anaaminiwa kweli na hiyo hospital kubwa hapa Tz kama jembe lao πŸ˜„
 
Polisi Tanzania yeye hajali kitu, yeye anapiga za vichwa kwa Gen Z, wakiandamana kwa masuala kama haya
 
Kuna vitu ukiwasikia hawa ma pro wetu unashika kichwa. Nilipata mtoto premature miaka miwili iliopita. Kuna siku madokta wanapita round Dr mmoja katika kumpima Pima mtoto huyo Dr akaropola NASIKIA SAUTI KAMA MOYO WA MTOTO UNA TUNDU! Wife alipaniki sana. Huyo Dr akasema ngoja nikamwite Dr mwenzangu.
Nikamwambia wife don't worry hilo Dr pumbavu. Hata mtoto angekuwa na hilo tatizo hakutakiwa kuropoka tu Kuna njia nzuri zaidi na alitakiwa ajiridhishe kabisa ndio atupe taarifa. Lwanza mtoro ana zaidi ya wiki hapa ina maana wengine wote na vipimo vyao hawakuona hilo tatizo? Baadae akaja na ma Dr wengine mwisho wakaondoka kimya kimya mtoto hana tatizo lolote.
 
Ngosha mwenzangu kanishtua sana yaan sasa hivi pale siendi tena bora nikaliwe hela private hosptal kuliko kwenda kuongeza tatizo
 
atapata tu fursa ya matibabu zaidi, ni vizuri awe na heshima kidogo
 
Sijajua huwa wana shida gani mkuu. Nachoka kabisa halafu wakiona wamekosea hata kuwajibishwa hakuna. Sasa fikiria huyo anaongea hata kujali privacy au sababu wanaona wote wanaokuja fata huduma ni vilaza.
Suala la kukataliwa vipimo vyetu nje ya nchini kubwa mno wao ndio sababu, na kuwafanya wagonjwa watibiwe tofauti na matatizo yao ndio zaidi sema wengi wao hawajui.

Hebu fikiria wangeshikilia hilo swala la mwanao mkuu? Hata hofu zaidi ungepata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…