maandamano
JF-Expert Member
- Nov 12, 2025
- 726
- 1,548
- Thread starter
-
- #121
Mtu wa kalibu kabisa wa Mtume alikuwa na Ali bin twalibu,mtu anapopewa utume yeye alikuwa na miaka 10 alizaliwa ndani ya Alkaba hakuabudu masanamu na ndiye mtu aliyekuwa na elimu ya Dini kuliko wote,na hata Mtume mwenyewe alidiriki kusema kama utume ungekuwa unaendelea basi yeye angekuwa sawa na Haruni ndugu yake Mussa,na ndiye Ally na famiria yake waliyemzika Mtume peke yake yao huku Maswahaba wengine wakigombania madaraka ya kurithi Uhalifa wa Waisilamu,na bado baada ya kupita fitina kubwa ya kumnyima uhalifa Waisilamu wenyewe walimuomba awe Halifa wao,lakini alipoona watu wa Madina hawamtii aliamua kuhamia kwenye mji wa Kufa na ndiyo alikozikwa huyu ndiye kioo cha Uisilamu ule wa Mtume mwenyeweKwa hiyo Uislam ulianzia Irani, Muhammad alikua mPersian? hahaha wewe utakua ulipata ufadhili wa masomo kutoka kwa Mashia ndio maana umekua kipofu, iko hivi WaIran ni Mashia na Mashia sio Waislam, imba hivyo kila baada ya dakika 2
Mungu alikuwa ameumba Ulimwengu usiokuwa na mabaya hapo mwanzo lakini kwa tamaa ya mwanadamu akadanganywa na shetaniSasa kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aliamua kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati angeweza kuumba ukimwengu ambao mabaya hayawezekani?
Angetaka ungekuwa ila kwa sasa ametaka maana ya ulimwengu uwe ni ule wenye mabaya kwa hiyo, hiyo ndiyo kanuni iliyopo
Wewe hata swali hujalielewa.Mungu alikuwa ameumba Ulimwengu usiokuwa na mabaya hapo mwanzo lakini kwa tamaa ya mwanadamu akadanganywa na shetani
Kwa sababu ya hekima yake ili atujaribu yadhihirike matendo yetuTunarudi kulekule.
Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote atake ulimwengu ambao mabaya yanawezekana, wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
Hujajibu swali.
Ukisema ulimwengu ndivyo ulivyo, hivyo ndivyo Mungu kataka, hayo si majibu.
Kwa sababu, hata mtu akikubali ulimwengu uko hivyo, na hivyo ndivyo Mungu kataka, bado hujajibu swali la kwa nini kataka hivyo na hakutaka kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.
Sasa, jibu swali.
Kwa nini Mungu kataka kuumba ulimwengu unaoweza kuwa na mabaya, wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
Atujaribu ili iweje wakati yeye anajua kila kitu?Kwa sababu ya hekima yake ili atujaribu yadhihirike matendo yetu
Ni kweli angeweza kuhukumu tu pale alipoumba tu lakini ametuleta duniani na kutupa majaribu ili tujionee wenyewe matendo yetu ili hata akituhukumu tukiri wenyewe kuwa tumestahili na sio atutupe tu motoni kwa kuwa Yeye anaujua mwisho wetuAtujaribu ili iweje wakati yeye anajua kila kitu?
Mwalimu wa shule anakujaribu kwa mitihani kwa sababu hajui yote, anataka kujua unajua nini.
Mungu anayejua yote, anayekupa uwezo na mipaka ya uwezo wako, anakujaribu ili iweje wakati yeye anajua yote?
Kwa nini unasema ni kweli angeweza kuhukumu pale tu alipoumba?Ni kweli angeweza kuhukumu tu pale alipoumba tu lakini ametuleta duniani na kutupa majaribu ili tujionee wenyewe matendo yetu ili hata akituhukumu tukiri wenyewe kuwa tumestahili na sio atutupe tu motoni kwa kuwa Yeye anaujua mwisho wetu
Kiranga sometimes huwa unanichekesha sana kwamba dini ni porojoUkishaona mgawanyiko kwenye dini tu, ujue hapo hakuna Mungu hizo ni siasa za watu tu, ni kama CCM na CHADEMA wanashindana.
Dini ni siasa ya kale iliyovishwa joho la utakatifu wa Mungu asiyethibitishika.
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwapo, wote tungemjua, tungemjua bila utata, na kusingekuwa na dini wala madhehebu tofauti.
Hizi habari za hawa Shia, hawa Sunni, hawa Katoliki, hawa Protestant, hawa Buddhist, hawa Hindu, zinaonesha hizi dini zote ni hadithi za kutungwa na watu tu, watu wanapambana na hali zao, wanataka kutawalana, na huyo Mungu hayupo.
Kwani uongo mkuu?Kiranga sometimes huwa unanichekesha sana kwamba dini ni porojo
Ooh naona sasa unataka kumpangiaKwa nini unasema ni kweli angeweza kuhukumu pale tu alipoumba?
Nani kasema hilo?
Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote atake kuhukumu wakati angeweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani na hakuna haja ya kuhukumu?
Hivi hata maswali yangu unayaelewa?
Si kumpangia, ni kutaka kuelewa.Ooh naona sasa unataka kumpangia
Yeye ameamua kutuumba sisi tuchague kati ya mabaya au mazuri hakutaka kutuumba kama malaika
Sasa naona wewe ulitaka atuumbe kama walivyo malaika
Mimi nilisema kuwa nitakata kona kulia ila nimekata kushoto ndio maana unanihojiSi kumpangia, ni kutaka kuelewa.
Wewe ukisema unakata kona kulia, halafu nikakuona umekata kona kushoto, nikakuuliza, kwa nini pale umekata kona kushoto, wakati ulisema utakata kulia, hapo nimekupangia au nimekuhoji tu kutokana na kauli yako mwenyewe?
Kwani Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao hauna malaika, na hauwezekani kuwa na mabaya?
Mpaka sasa hujaelewa kuwa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana, wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani, ni contradiction, ni jambo la kujichanganya, kimantiki haiyumkiniki?Mimi nilisema kuwa nitakata kona kulia ila nimekata kushoto ndio maana unanihoji
Kwani Allah alisema ataumba ulimwengu usiokuwa na mabaya?
Contradiction ipo wapi?Mpaka sasa hujaelewa kuwa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana, wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani, ni contradiction, ni jambo la kujichanganya, kimantiki haiyumkiniki?
Bado hujaelewa hili jambo tu?
Naona huwezi kutoa majibu, kwa sababu hujaelewa swali.
Sifa za uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote alizonazo huyo Mungu wenu haziendani na ulimwengu unaoweza kuwa na mabaya mnaousema kauumba.Contradiction ipo wapi?
Kwani kuna sehemu alisema kuwa anataka kuumba ulimwengu usio na mabaya mpaka iwe contradiction?Sifa za uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote alizonazo huyo Mungu wenu haziendani na ulimwengu unaoweza kuwa na mabaya mnaousema kauumba.
Mungu huyo mnasema ana.
1. Uwezo wote wa kuumba ulimwengu usiowezekana kuwa na mabaya.
2. Ujuzi wote wa kuumba ulimwengu usioweza kuwa na mabaya.
3. Upendo wote wa kuumba ulimwengu usioweza kuwa na mabaya.
Angeuumba ulimwengu huu uwe hauwezekani kuwa na mabaya, kusingekuwa na contradiction. Hilo ndilo tungetegemea kutoka kwake.
Lakini tunaona ulimwengu huu unaweza kuwa na mabaya.
Hii ni contradiction.
Ni kama vile uambiwe kuna baba anawapenda watoto wake, ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote wa kuwajengea nyumba iliyo salama kabisa, isiyo na mabomu.
Halafu kwa makusudi kaamua kujenga nyumba yenye mabomu yanalipuka ovyo ovyo, watoto wake walipukiwe na mabomu.
Tutajiuliza, kwa nini huyu baba, tunayesema ana uwezo, ujuzi na upendo wa kujenga nyumba isiyo na mabomu, kaamua kujenga nyumba yenye hatari ya mabomu kwa watoto wake anaowapenda?
Huoni kwamba hii habari ina walakini sehemu?
Sikutaka kucomment.. ila ulichokiandika nimeona nicomment ili tusaidiane kudadavua mambo.Wairani sio Waislam ni Mashia na Mashia sio Waislam, period.
Dhana ya kuwepo kwake ni utakatifu usio doa, kuumba ulimwengu unaoweza kuwa na mabaya tu tayari kunaiwekea swali dhana hiyo.Kwani kuna sehemu alisema kuwa anataka kuumba ulimwengu usio na mabaya mpaka iwe contradiction?
Kwa nini yeye asijue kusoma halafu wengine wajue wakati wapo kwenye mazingira sawa?Dhana ya kuwepo kwake ni utakatifu usio doa, kuumba ulimwengu unaoweza kuwa na mabaya tu tayari kunaiwekea swali dhana hiyo.
Mungu wa haki anawaumba vipi watu waje kuishi katika ulimwengu wenye mabaya mengi, tena bila ridhaa yao, wanajikuta tu wapo.
Yeye ndiye anawapa kila kitu, ukiwamo uwezo wa kutenda mazuri na mabaya.
Halafu wakifanya mabaya, kwa sababu ulimwengu aliouumba yeye Mungu unaruhusu mabaya, yeye anawahukumu kwa kutenda mabaya.
Yani mzazi unamnyima mtoto fursa ya kwenda shule kujifunza kusoma na kuandika, unamzaa na kumkuza sehemu ambayo hakuna shule, hawezi juepuka kutojua kusoma na kuandika, halafu asipojua kusoma na kuandika, unamuhukumu kwa kutojua kusoma na kuandika.
Huoni contradiction hapo?