Al Mukheef
JF-Expert Member
- Dec 7, 2025
- 315
- 479
Yeye ndiye ametaka mabaya yawepo na ndiye ametaka hukumu iwepoKwa nini hukumu iwepo?
Mungu angeumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kuwapo hukumu ingekuwapo?
Kwa nini Mungu kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana kuwapo wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
Hujajibu swali hili.
Sifikiri hata kama unalielewa swali.
Kwa majibu unayotoa, hujalielewa swali bado.
🙂🙂 Sijui ni nyie Waislamu wa Africa au Tanzania tu ndio mnakuwa wanafki, hili ni la kujiuliza kweli?!Muanzilishi wa serikali ya kidini au iliyokuwa na uhusiona na mbinguni alikuwa Mtume Muhammad (S.A.W)na hiyo serikali ilihasisiwa kwenye mji wa Madina ambapo aliishi na baadhi ya wayahudi lakini hakuwalazimisha kuingia kwenye Uisilamu ila walikubaliana katika swala la ulinzi endapo atavamiwa na madui,na hata Irani kuna baadhi ya watu wa madhehebu tofauti umeshawahi kusikia wanalazimishwa?
Lakini Israeli imepitisha sheria ya mtu yoyote yule atakayeabudu kwa jina la Yesu kwenda gerezani,umeshawahi kusikia Uisilamu umefanya hivyo
Sawa ametaka. Kwamba ametaka au hakutaka si hoja.Yeye ndiye ametaka mabaya yawepo na ndiye ametaka hukumu iwepo
Acheni hizo bana dini yenu historia inaonyesha uchinjaji wa kulazimisha watu.Hiyari yake
Uislam ni mmoja tu ulimwengu mzima hauna DHEHEBU, Shia sio Waislam.Kwani Uislamu ni nini? na madhehebu yake makuu ni yapi?
Ukiweza kujibu hilo, basi hapo tutajua kama Shia ni Islam au sio Islam.
Kwa nini ulazimishwe kuvaa mavazi kwa namna ya Kiislamu??Tofautisha unapokuwa katika inchi ya kidini hawatakulazimisha kuswali ila utalazimishwa uvae mavazi ya kujistiri,chukulia mfano unaweza kwenda beach na mama yako hata kama kavaa vitenge halafu mkawa mnaona wanawake wengine wamevaa vichupi hivi mtatizamana vipi na mama yako au mwanao?
Upo sahihi kabisa kiongozi, dini ni biashara za watu, dini ni utumwa mambo leo, nashukuru wengi tunaanza kujielewa na kujikomboa.Ukishaona mgawanyiko kwenye dini tu, ujue hapo hakuna Mungu hizo ni siasa za watu tu, ni kama CCM na CHADEMA wanashindana.
Dini ni siasa ya kale iliyovishwa joho la utakatifu wa Mungu asiyethibitishika.
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwapo, wote tungemjua, tungemjua bila utata, na kusingekuwa na dini wala madhehebu tofauti.
Hizi habari za hawa Shia, hawa Sunni, hawa Katoliki, hawa Protestant, hawa Buddhist, hawa Hindu, zinaonesha hizi dini zote ni hadithi za kutungwa na watu tu, watu wanapambana na hali zao, wanataka kutawalana, na huyo Mungu hayupo.
Ukimwambia mtu kwamba mavazi ya kiisilamu anafikiri labda ni kanzu na baibui,hapana tumefundishwa na Mwenyezi Mungu kupitia mtume wake mwanaume avae nguo itakayofunika kuanzia chini ya magoti yake mpaka juu ya kitovu chake,na mwanamke afunike kichwa nguo isimbane ikachora mwili wake na iichie chini ya kongo zake za miguu,sasa ubaya uko wqpi?Kwa nini ulazimishwe kuvaa mavazi kwa namna ya Kiislamu??
Kwa nini wasitenge beach kwa ajili wanawake wanaovaa vitenge na niqab tu na beach ambazo wanawake wanaruhusiwa kuvaa vyovyote??
Tatizo hamjui nini maana ya Uisilamu mnaochukulia juju tu ukitaka usome uelewe hauko kama dini zingine🙂🙂 Sijui ni nyie Waislamu wa Africa au Tanzania tu ndio mnakuwa wanafki, hili ni la kujiuliza kweli?!
Ukiwa raia wa dola za kiislamu ukipata ukweli mpya ukaacha uislamu jela au kifo ni hukumu yako.
Hamjui historia na ikiwa hata wazi mnasema ni ya uongo😛.
Unaweza kujenga kanisa au hekalu la kihindi Saudi, UAE, Oman au Iran jibu ni HAPANA.
Unaweza kujenga msikiti katika mataifa ya ulaya na Marekani jibu ni NDIO, sababu waliamua kuwa secular, dini ibaki kuwa ya mtu. Kwa kuwa kuna wazungu wanataka kuwa Waislamu, kwanini uwanyime suala hilo?
mnavyojua kutaja namba za wenzenu,na Israeli wamekufa wangapi toka mashambulizi ya Irani yaanze?Serikali ya Iran ili ua waandamanaji zaidi ya 6000, Mange na watz wapenda Haki hatusapoti ukiua waandamanaji
Laana ya kua waandamanaji itaitafuna Iran na Tz Karma is real
Hivi kuna dini iliyochinja watu wengi kwa kulazimisha waiamini dini yao kama Romani?Acheni hizo bana dini yenu historia inaonyesha uchinjaji wa kulazimisha watu.
Ipo wazi kabisa Wayahudi Jerusalem ni yao, uislam uli force pale, wakaja waroma waka force kuwaondoa waislam akaja Ottoman na fujo zake.
Watu wakajua Jews wamekata moto, kumbe wapo wanaangalia namna ya kuji restore 1948
Wakristo, Waislamu na Mataifa mengine wawaachie wayahudi haki yao kwao. Mfano Ilipo Masjid Al Aqsa ndio ilipokuwa Temple Mountain ya Wayahudi. Wailamu wanasema Al Aqsa ilijiengwa na nabii Adam, ikajengwa tena na nabii Ibrahim na baadae King Suleiman.
Kisha Al-Aq Umayyad Caliphate karne ya 8 wakajenga ambayo kimsingi ndio structure mpya iiliyoendelea, na mtume hakusali humu. Alisali katika hayo ya zamani likiwa ni eneo takatifu.
Ukirudi katika fact Wayahudi walikuwa kisali eneo lile kabla ya 'Waislamu wa Mtume Mohammed'.
Nimeita "Waislamu wa Mtume Muhammmed" kukwepa dhana ya kuambiwa manabii wote walikuwa waislamukwa kuwa walimuamini Mungu mmoja.
Kama King Seleiman hadi quran inamtambua ni Bani Israel na alijenga pale, basi tayari iko wazi pale ni pao na kwao.
WAKRISTO,WAISLAMU NA MATAIFA KAMA IRAN WAACHE KUWASUMBUA WATU WALE
Kwani nini maana ya dhehebu?Uislam ni mmoja tu ulimwengu mzima hauna DHEHEBU, Shia sio Waislam.
Ni kweli unachosema sipingi kuhusu Roman nao pia waliwaua Jews kwao, kuna sehemu nimegusia kuwa tuwaache Jews ktk haki zao, watu waliwafata kwao. Mfano unakuta mtu anasema wauwawe na asilimia takribani 18 ya Jews ni waislamu piaHivi kuna dini iliyochinja watu wengi kwa kulazimisha waiamini dini yao kama Romani?
Wewe unaweza ukajibu kwa nini huyo mtu afanye maovu na wengine wasifanyaje?Sawa ametaka. Kwamba ametaka au hakutaka si hoja.
Sijauliza Mungu ametaka au hajataka hivyo.
Unajibu swali ambalo sijakuuliza, wakati swali ambalo nimekuuliza hujajibu.
Kama unamuelewa Mungu wako, inatakiwa uelewe kwa nini alitaka kuumba ulimwengu ambao unaweza kuwa na mabaya, wakati alikuwa na uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao hauna mabaya na hauwezekani kuwa na mabaya.
Ukishindwa kujibu swali hili, ukitupa majibu ya "yeye alitaka", majibu ambayo yanajibu swali la "alitaka au hakutaka" ambalo si nililouliza mimi, na majibu ambayo hayajibu swali la "kwa nini alitaka hivyo?", unatuonesha kuwa humuelewi Mungu wako na pia hujaelewa swali langu.
Kama huelewi swali langu, utalijibu vipi?
Na kama humuelewi Mungu wako kiasi cha kuweza kujibu swali hili, utajuaje kuwa Mungu huyo yupo kweli?
Huoni kuwa kama unashindwa kujibu maswali kama haya unaweza kuwa unamuamini Mungu ambaye hayupo?
Nani hafanyi maovu?Wewe unaweza ukajibu kwa nini huyo mtu afanye maovu na wengine wasifanyaje
Kuna kufanya maovu madogo au machache ambayo hayawezi kukufanya ukahukumiwa na wale wanaofanya maovu makubwa na mengi?Nani hafanyi maovu?
Unaweza kutoa mfano wa mtu mmoja ambaye hafanyi maovu?
Na kwa nini unaona maovu ni kitu cha kufanya tu?
Unaelewa hata maovu ni nini?
Mungu angeumba ulimwengu ambao maovu hayawezi kufanyika, kuna mtu angeweza kufanya maovu?
Kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao maovu yanaweza kufanyika, wakati alijua na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao maovu hayawezi kutokea kabisa?Kuna kufanya maovu madogo au machache ambayo hayawezi kukufanya ukahukumiwa na wale wanaofanya maovu makubwa na mengi?
Mimi nawaulizia wale wanaofanya maovu mpaka wakastahili kuhukumiwa kwa nini wafanye maovu?
Hili si suala la mimi ninavyotaka aumbe, ni suala la kuhoji logical consistency ya maelezo yenu ya kuwapo Mungu.Unauliza kwa nini alitaka kuumba hivyo?
Wewe ulitaka aumbe vipi?
Ndiyo maana nikakuuliza kwani Allah alikuambia kuwa ataumba ulimwengu usio na maovu mpaka uhoji kwa nini ameumba ulimwengu wenye maovu?Ukisema utaenda kulia, halafu ukaenda kushoto, nikikuhoji mbona ulisema utaenda kulia halafu ukaenda kushoto
Wewe mwenyewe hujajibu kwa nini huyo mtu afanye maovu na asifanye mema?Hujajibu swali.