Kwa masharti na stress hizi utazopitia, Utajiri wa ndagu ni heri kuwa masikini tu

Kwa masharti na stress hizi utazopitia, Utajiri wa ndagu ni heri kuwa masikini tu

Coco kuna siku kwenye comment yako moja ulisema ukisoma story ya INSIDER MAN ule mtiririko wake unajifunza kiswahili vizuri! Kwani kiswahili kinakupa shida madam? I mean umeanza kujifunza ukubwani?

Hapana tangu mdogo
hakinipi shida nijuavyo, Ila sijui y ipo ilivyo. Miaka yote naambiwa hivi humu, najitahidi wapiii nionavyo.. Kilugha chetu kimenimeza 😊

cc: ERoni
 
Kuna mtoto wa staa wetu mkubwa hapo bongo juzi imerushwa video yake mtoto alizaa na Mkenya yuko chale haswa.
 
Hizo ni porojo tu, hakuna pesa zinazopatikana kwa aina hiyo.
Huyu ni mmoja wao anaemiliki pesa za hivo au ni mtoto wa tajiri mwenye pesa za hivo ye anatumbua tu kwahiyo hajui magumu babaake anayopitia
 
Aya mambo huwa yapo, katika harakati zangu za ujana nilijikuta nimeingia chimbo moja. Maelekezo waliyonipa, sitakiwi kuchepuka, sitakiwi kunywa pombe, sitakiwi kula kitimoto, kutoa sadaka kila mwaka (mnyama). kama ningekubali, wangenichana sehemu ya mwili na kupandikiza dawa iliyofungwa kwenye ngozi ya mnyama (jini). Mafanikio yangeonekana kwa kila ninachokifanya kinakuwa kinazaa mara dufu. Swali, unakuwa na hela ila uzifurahii ni nini maana ya hela?​
Aisee 🤔
 
Ninajitegemea kwa miaka 15, nimefika nchi 7 na mpaka sasa hivi sijawahi kuona hata dalili ya hizi porojo zenu za uchawi.
Uchawi na ushirikiano vipo Sana mkuu.
Mimi mwenyewe nimewahi kushuhudia haya mambo kwa macho yangu kbsa
 
Watu mna Siri usikute hizi pesa zipo sana ila mlivyo na Siri sasa
 
Umewahi kushuhudia tukio gani la uchawi kwa macho yako?
Hata akikuambia ni kazi Bure. Mnafikiri hii dunia ni kuangalia matako tu ya kina pipitida ...siku mkikua kiroho ndio mtaelewa.
 
Watu mna Siri usikute hizi pesa zipo sana ila mlivyo na Siri sasa
Bongo hii hata mtu kupewa chimbo la kununua bidhaa kwa bei rahisi mtu anakunyima itakua sembuse mambo mazito hayo....bongo ndio mana umaskin hauishi...tabaka la maskin na matajiri linaendelea kupanuka kama Kumah....
 
Biashara zile zilizokamatwa kwenye Gari la Abood ni uchawi ule?
Mirungi haiwezi kukupa utajiri, ni vicious circle tu maana watumiaji mirungi ni watu wa chini tu. Labda angeuza heroine nayo nje ya Tz. Tanzania mateja wanakula makapi ya cocaine tu
 
Aya mambo huwa yapo, katika harakati zangu za ujana nilijikuta nimeingia chimbo moja. Maelekezo waliyonipa, sitakiwi kuchepuka, sitakiwi kunywa pombe, sitakiwi kula kitimoto, kutoa sadaka kila mwaka (mnyama). kama ningekubali, wangenichana sehemu ya mwili na kupandikiza dawa iliyofungwa kwenye ngozi ya mnyama (jini). Mafanikio yangeonekana kwa kila ninachokifanya kinakuwa kinazaa mara dufu. Swali, unakuwa na hela ila uzifurahii ni nini maana ya hela?​
Hapo ningeshindwa sharti moja tu la kutokula kitimoto
 
Kilugha chenu ni kipi Coca?

Yaani kazi sijui nitaje ipi utaelewa.. Ni kutoka mikoa minne

Kwa Dingi kutoka kabila 2
Kwa Maza kutoka kabila 2

Wao wazee kila mmoja na mkoa wake.. Labda ndio maana sijuwi Kiswahili. 😅🤗
 
Back
Top Bottom