Kwa masharti na stress hizi utazopitia, Utajiri wa ndagu ni heri kuwa masikini tu

Kwa masharti na stress hizi utazopitia, Utajiri wa ndagu ni heri kuwa masikini tu

Aya mambo huwa yapo, katika harakati zangu za ujana nilijikuta nimeingia chimbo moja. Maelekezo waliyonipa, sitakiwi kuchepuka, sitakiwi kunywa pombe, sitakiwi kula kitimoto, kutoa sadaka kila mwaka (mnyama). kama ningekubali, wangenichana sehemu ya mwili na kupandikiza dawa iliyofungwa kwenye ngozi ya mnyama (jini). Mafanikio yangeonekana kwa kila ninachokifanya kinakuwa kinazaa mara dufu. Swali, unakuwa na hela ila uzifurahii ni nini maana ya hela?​
Ni kama kupata cheo cha ndani ya serikali za Afrika. Pesa na madaraka unayapata ila Raha hupati.

Unazuiwa usipig Mbunye usinywe pombe na usile K/moto. Hizo hela Bora uzikose tu
 
Kuna mwamba kwake kuna kaburi 7 amezisakafia zote.Amemalza familia kisa tamaa hana wazazi mke wala watoto.Ila anabiashara za kutosha na magari ya kifahar.Ila haish nafurah ili anajutia kuingia mikataba na kuzim.Asipotoa kafara majin yanamtokea yanamtesa.Bora kufa maskin kulk kuwa mtumwa wa shetan
Haya ni masimulizi tunya mitaani hayana ukweli
 
Kumchizisha ndugu yako awe ndondocha, kila siku unaporudi unajijua wewe ndio chanzo chake kuwa chizi

Kumuua mzazi wako, mtu aliekuleta duniani umemtoa duniani anatumika kama msukule.

Kumuua mtoto wako, damu yako umeitowesha duniani kwasababu ya tamaa yako ya pesa.

kukatazwa kusaidia ndugu, wazazi na marafiki, kusaidiaa ni ndani ya kikundi cha waliokubali masharti au watu wataotumika hapo baadae kwenye mambo ya kafara

Kukatazwa kushiriki mapenzi, hapa unapewa masharti ukitaka kushiriki mapenzi shiriki na mtoto wako wa kike, ndugu uliemgeuza kuwa ndondocha au kushiriki mapenzi ya jinsia moja, pisi kali unaishia kupiga nazo picha tu

kukatazwa kula vyakula vizuri kama nyama, wewe ni kushindia viazi, ugali figili, n.k. kwa kuwa pesa zipo ni rahisi kuonekana unakula diet ila chamoto lazima ukione, pesa ya kuku choma ipo lakini umekatazwa
Huo ndiyo utajiri wa yule Chief Goodlove anayetamba na magari ya thamani, lakini hajajenga nyumba popote iwe Kyela, Mbeya au Dar
 
Hizo ni porojo tu, hakuna pesa zinazopatikana kwa aina hiyo.
Karibu Mkoa wa Njombe, Mbeya, Ruvuma na Iringa. Hawa wapo sana na tunaishi nao. Sasa hivi wamehamia Kariakoo na wanamiliki magorofa

Wapo waliofulia baada ya kukiuka masharti, na wapo wanaotamba sasa kwa pesa nyingi bila biashara inayoendana na utajiri walionao
 
Karibu Mkoa wa Njombe, Mbeya, Ruvuma na Iringa. Hawa wapo sana na tunaishi nao. Sasa hivi wamehamia Kariakoo na wanamiliki magorofa

Wapo waliofulia baada ya kukiuka masharti, na wapo wanaotamba sasa kwa pesa nyingi bila biashara inayoendana na utajiri walionao
Sio kwamba wana biashara zisizoonekana?
 
Back
Top Bottom