Je, ni-assume tu kwamba unaishi, let's say, Dar es salaam, tena umepanga chumba kimoja Uswahilini?!
Suala la wapi upo lina-matter sana kwa biashara nyingi!!
Mtu anaweza kukushauri uanzishe biashara ya kitimoto kumbe unaishi Chake, Pemba! Mwingine anaweza kukushauri ufuge kuku wa kienyeji kumbe unaishi chumba cha kupanga!
Anyway... mimi nita-assume upo Dar!
1. Kwavile huwezi kufanya kazi full time, basi tafuta kijana(m/f) aliye humble na asiye muoga kuingia maofisini!
2. Ji-connect na watu wa Visiwani hususani Mafia. Lakini unaweza ku-include Kilwa na Pangani au kokote kule ili ufanye Total Cost Analysis kwa kila eneo!
Kama humfahamu yeyote, tumia FB kutafuta ma-group ya watu wa huko!
3. Peleleza kujua bei ya samaki ipo vp huko!!
4. Ukiona bei ina maslahi; tafuta vitendea kazi hususani crate utakayotumia kusafirishia samaki to Dar!
5. Uwe unachukua samaki wa size maalumu tu... sio mara dagaa humo humo, mabaunsa humo humo!
6. Mzigo ukifika mjini, tembeza maofisini! Kama unapoishi sio Uswahilini sana, wakati dogo anaenda maofisini, anaweza kukuachia mzigo kidogo ambao utaweka tu meza safi nje na kuweka mzigo wako hapo lakini jitofautishe kwa kuzingatia usafi!
Mengine; jiongeze!