Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

[emoji106]
 
Sisi vijana tuna uvivu flani hivi unsosababishwa na hivi vyeti vya chuo.ila hizi biashara ndogo ndogo hulali njaa kabisa.mfano ingia sokon mabibo au temeke sterio hapo wanauza tikiti buku hadi buku 2 ukilikata kwa ustadi unatoa vipande hata vya buku 4 kwa tikiti moja tafuta meza yako safi panga uza.Niamini mimi unatoka kwa siku hata tikiti 10 unauza.na kukunja 20k. Nenda hapo hapo sokon machungwa wanauza 70tsh wanuza kuanzia kumi.chukua machungwa yako kadhaaa kaaa na meza yako stend uza 150 usitake faida kubwa.Amini mungu utaonekana kawaida lakini maisha yako yanakuendea hakuna kwenda kwa mganga wala nini.! Mimi kama sio hivi vyeti vyangu ningeingia front kuuza matunda ila vyeti vimenifanya kuwa na aibh usoni ntaonekan vipi na watu wanaonijua ??? Ntadharaulika ntachekwa....
 
 
Nilihangaika kumjibu bure, kumbe ulikuwa ushamaliza.
 
Habari za mida hii wana JF,
Naomba kuuliza, kwa mtaji wa Tsh 200, 000 naweza kuanzisha biashara gani hapa Dar itakayoniwezesha kutengeneza faida ya Tsh 20, 000 kwa siku!!
Msaada wenu tafadhari!!
Kuuza shanga
 
Hahaaa...bado hayajakupiga rafiki..
Yakikupiga mbona utasahau kama ulishasomaga?
Ndo mana hawa hawa ambao hawajasoma wanatupiga gap wasomi WA Leo..
 

Huu ushauri unautoa uku una njaa!
 
[emoji2]boss nachukua mtumba wa watoto ilala ,kwa 221,000 unayoifahamu ,naweza pata nguo 493 mchanganyiko .
Siku ya kwanza na ya pili nauza 3000 kila nguo, siku ya tatu nauza 1500 ,siku ya nne nauza 1000 kila nguo ...akipatikana mteja wa jumla nguo za mwishoni namuuzia 500 kila moja (wauza mtumba wanaweza kuelewa hapa )

Faida kwa siku 5 waweza kusanya 125,000 unayoifahamu .Kwa washindia mihogo wenzangu natenga 25,000 (operational cost ) nyingine ni faida ya msakatonge,ukipata location nzuri unawezapata faida zaidi ya hapo,

Hii ni ushuhuda wa kijana tu wa tandale .Subiri muuza pweza aje kukupa mchanganuo wa kupata faida ya 20,000 kwa mtaji huohuo mdogo mnaomaliza kwenye bia kwa siku
 
Mkuu usimlazimishe kuamini ,wasakatonge tumekuelewa inatosha
 

ile meza ya muuza pweza ukijumlisha vitu vyake ....pilipili + kachumbali +ule mchuzi + pweza mwenyewe haiwezi zidi 18k akiuza vitu vyote maana Kuna siku anaweza asipate wateja na mzigo ukalala hawezi zidisha 30 k Sasa hio faida ya 20k mnayosema huku kwenye keyboard hivi mnatuona sisi wajinga et ....pita pale kivukoni jion uone maishe ya hao wauza pweza ndio uje uniambie kama ni mtu mwenye uhakika wa laki 6 kwa mwezi ...

Wewe endelea kujitekenya nakucheka mwenyewe huku ,uzuri mnajua moto wa biashara huku mtaani ,changamoto ni kibao Tena zaidi ya mnavoona .....kwanza nyie watu wa ofcin hamuwezi nambia kitu chochote kwenye biashara zaidi ya kuandika maneno ya kusadikika huku ukifikili huku mtaani yanaweza kufanya kazi ...!
 
Fungua kijiwe cha kahawa utauza asubuh na jion kila siku faida ni 40,000 maji dumu 2 za lita 20, kahawa ya elf 5, kashata za elf 5, mkaa elf 5 , vikombe elf 20, jiko la elf 5, sukar ya elf 10 na malimao ya buku
hahahahaha, mna fantasies nyingi sana hapa ila ukija 'field' mambo ni tofauti
kuandika, kuongea ni rahisi mno
 
boss na ilo wazo la kufungua nguo za watoto km una uzoefu san naomba nkuone unipe msaada
 
hey
 
Unafeli sana

Hua naingia k/koo najumua vipodoz kwa 253k

Revenue ni 1.45milion , kwa mwez naenda mara 3


Akili kumkichwa , kuingiza pesa yamaana hakuna uhusiano wowote na mjtaj

Hawa wauza ice cream wa Bakhresa, mule ndan hua kuna mzigo wa 15k , net profit yao hua ni 7k .. so mtu anajitad kwa siku atoe walau viwili vile

Again, akili kumkichwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…