[emoji2]boss nachukua mtumba wa watoto ilala ,kwa 221,000 unayoifahamu ,naweza pata nguo 493 mchanganyiko .
Siku ya kwanza na ya pili nauza 3000 kila nguo, siku ya tatu nauza 1500 ,siku ya nne nauza 1000 kila nguo ...akipatikana mteja wa jumla nguo za mwishoni namuuzia 500 kila moja (wauza mtumba wanaweza kuelewa hapa )
Faida kwa siku 5 waweza kusanya 125,000 unayoifahamu .Kwa washindia mihogo wenzangu natenga 25,000 (operational cost ) nyingine ni faida ya msakatonge,ukipata location nzuri unawezapata faida zaidi ya hapo,
Hii ni ushuhuda wa kijana tu wa tandale .Subiri muuza pweza aje kukupa mchanganuo wa kupata faida ya 20,000 kwa mtaji huohuo mdogo mnaomaliza kwenye bia kwa siku