Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Ahsante sana kaka Slim5 bila shaka nitalifanyia kazi wazo hili...
Lakini umenifanya nicheke sana mkuu..!
 
nitafanyia kazi wazo lako
na vipi bei naweza nikapata kwa sh ngapi
 
kwa hili swali lako nakushauri usifanye biashara kabisa, fuga kuku
why nifuge kuku na mimi interest yangu ni biashara
nimeuliza bei za jumla ili nilinganishe kutokana na eneo nililopo kuwa nitapata faida au lah
mfano viatu vya kike kwa bei ya jumla hapo karume
but poa
 
Naomba mchango wa kima wazo, nina laki 5 nifanye issue gan?
Npo .....Dodoma (UDOM)
Age ..... 27
Plz tia neno...............
 
Gud idea
 
Mungu Awabariki sana uzi huu,hapa hata ukisema una shilingi hamsini unataka kufanya nini,hamna atakayekubeza,utapewa ushauri nini ufanye,mnawakomboa watu wengi sana ki fikra katika ujasiriamali,mnatoa ile dhana nzima kuwa mpaka uwe na mamilioni ndo ufanye biashara
 
Hii posti nimeikuta humu humu, kama imani yako inaruhusu na una mtaji wa kma laki 5 basi fanya research then anza hivi kama jamaa anavyotoa ushuhuda wake...


Ufugaji wa nguruwe ulivyonipa utajiri na kujitegemea

Habari wanaJF

Tafadhali kwa wale wasiopenda jina hilo hapo juu samahani sana.

Mimi nimefuga nguruwe, nilianza nikiwa niko chuo kikuu mwaka wa pili pale UDSM kwa mtaji wa shilingi 500,000/=

Nilianza kujenga zizi kwa shilingi laki tatu tu na nikanunua makinda ya nguruwe mawili jike na dume kila mmoja sh. @40,000 (mradi niliufungua nyumbani mkoani Kigoma). Fedha zilizobakia nilitafuta mfanyakazi wa kuwalisha hao nguruwe. Nilimlipa sh. 40000 kwa mwezi. Kati ya laki 5, zilibaki 80,000 ambazo nilianza kwa kunulia chakula cha nguruwe.

Baada ya hapo nguruwe niliwapandisha wakazaa watoto 10. Kati ya hao madume yalikuwa 4 na jike 6. Baada ya hayo makinda kukua sikuuza makinda ya jike. niliamua kupanua mradi hivyo nilipanua zizi! Hapo ilikuwa baada ya miezi tisa tu.

Baada ya kupanua mradi niliuza madume 3 nikanunua vyakula (maharage yaliyooza na mashudu) ya kulishia nguruwe waliobakia.

Baada ya miezi 18 nguruwe waliongezeka baada ya kuzaa tena (yale majike 6 na dume 1). Nikaendelea kupanua zizi maana nilijikuta nina nguruwe 30. Kumbuka nguruwe sita wote walizaa. Mmoja makinda 6, mwingine 5, mwingine 5 mwingine 4 mwingine 7 na mwingine 2, na lile dume 1. Jumla nguruwe 30.

Nazidi kupanua mradi na chuo nimeshamaliza kwa sasa nasimamia mwenyewe!

Hakika kwa sasa mimi ni tajiri!

Amini usiamini mimi sio masikini tena!

siku njema.
 
Heshima kwenu wakuu
Nina laki tano nataka kuanzisha Biashara..naogopa kukurupuka
Wazoefu nisaidieni je naweza kuanzisha Biashara gani ikalipa?
Naishi Mburahati
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…