Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Uza matunda maofisini ukiwa umeweka kwenye vifungashio,.. Vinalipa saana.
 
Salamu kwenu wana jamii...
Kama heading inavyojieleza...
Ni biashara gani nayoweza kufanya kwa mtaji wa shilingi laki tano za kitanzania..?
Nahitaji mawazo yenu KAKA na DADA zangu wa jamii forums katika jambo hili..!​
 
Mimi nafanya biashara ya Mult level Marketing nilianza na mtaji wa laki 280 inanilipa nanaendelea vizuri kwa sasa. Nakushauri na wewe karibu laki tatu inaweza kuwa mtaji mkubwa sana kwa biashara hii. 0763797853 whatsap na live calls
Mult level marketing ni nn mkuu
 
mimi nikushauri kwanza nikupongeze kwa kuwa na wazo la uwekezaji katika biashara.

Niukweli usiopingika kwamba ukitaka kuwa tajiri na kuwa huru katika eneo la kifedha basi biashara ndiyo suluhisho.

Kwa mtaji wa laki 3 kwetu sisi wafanyabiashara ni pesa nyingi sana kama ukiweza kuwekeza kwenye fursa zinazokuzunguka na zisizo hitaji mtaji mkubwa.

Siku zote biashara zenye fedha nyingi ni biashara ndogo ndogo.

Ukiweza kununua Mayai kama trei 10 za kuku wa kisasa na ukazunguka kwenye vioski vya kukaanga chips na kuuza kwa jumla ndani ya muda mchache utakuwa umekuza mtaji wako.

Mfano ukanunua trei 1 kwa sh 6500 ukauza elf 7000 kwenye trei 10 utapata elf 10

ukipata wateja 10 kila siku wote wakachukua Trei 10 kila m1 utakuta unatengeneza laki moja kwa siku faida. Hapo hujatoka?

Tatizo la watu wengi hawataki kuanzia chini ndiyo maana wanadharau fedha na kubaki maskini.
 
Mapochi ya kina Dada ya mitumba, unanunua kwa jumla unasafisha vizuri, shona yawe kwenye hali nzuri, unayauza being nzuti maana ni leather na material yake mengine ni imara, yanahitaji muda was kuyarrkebisha tu, yatakulipa sana kwa hela hiyo
 
mimi nikushauri kwanza nikupongeze kwa kuwa na wazo la uwekezaji katika biashara.

Niukweli usiopingika kwamba ukitaka kuwa tajiri na kuwa huru katika eneo la kifedha basi biashara ndiyo suluhisho.

Kwa mtaji wa laki 3 kwetu sisi wafanyabiashara ni pesa nyingi sana kama ukiweza kuwekeza kwenye fursa zinazokuzunguka na zisizo hitaji mtaji mkubwa.

Siku zote biashara zenye fedha nyingi ni biashara ndogo ndogo.

Ukiweza kununua Mayai kama trei 10 za kuku wa kisasa na ukazunguka kwenye vioski vya kukaanga chips na kuuza kwa jumla ndani ya muda mchache utakuwa umekuza mtaji wako.

Mfano ukanunua trei 1 kwa sh 6500 ukauza elf 7000 kwenye trei 10 utapata elf 10

ukipata wateja 10 kila siku wote wakachukua Trei 10 kila m1 utakuta unatengeneza laki moja kwa siku faida. Hapo hujatoka?

Tatizo la watu wengi hawataki kuanzia chini ndiyo maana wanadharau fedha na kubaki maskini.
naomba kuweka hesabu sawa, maana humu kuna watu kazi yao kuvizia kutoa makosa.

Kwenye trei 10 utapata 5000, badala ya elf 10 nadhani hapo nimeweka Hesabu vizuri.

Pia kupata tenda kama hizi kunahitaji uwe na kauli zenye kushawishi. Yaani lugha nzuri na uchangamfu.

Katika vitu ambavyo vinawaangusha sana watanzania ni kuutumia ulimi wao vizuri.

Utakuta unakwenda dukani kununua kitu. Unamkuta mwenye duka kanuna na hatoi lugha za ushawishi wa kukuvuta mteja ununue bidhaa kwake na kukupa motisha ya kurudi tena.

Mimi wakati mwingine natoka ofcn nakwenda kujichanganya na wafanyakazi wangu kuhudumia wateja.

Na ukinikuta nahudumia utadhani natongoza Mwanamke.

Hizi mbinu nilijifunza kwa rafiki zangu wa kihindi. Hawa jamaa ni hatari sana kwenye biashara wanajua kuhudumia mteja.
 
Mkuu Nenda kabeti yaani nakuhakikishia unalala maskini kesho unaamka tajiriiii....
kama mimi ningekuwa Rais. Ningepiga marufuku michezo yote ya kamari.

Maana michezo hii inawafanya watu walemae na kutegemea miujiza ili wapate Pesa badala ya kufanya kazi.

Siku zote katika maisha hakuna mafanikio ya gafla bali mafanikio ni mipango thabiti.

Ndiyo maana hawa jamaa wa kubeti wamepiga kambi tanzania maana tanzania ndiyo shamba la bibi.

Watu hawataki kufanya kazi wanakimbilia kubet!
 
Kama upo eneo linalofaa kwa ufugaji Anzisha mradi wa kufuga kuku wa kisasa unaweza kuanza na kkuku 25 hyku kwa makadirio ya kuku 15000Tsh hapo utanunua majogoo 5 na mitetea 20 then unaanza MDOGO MDOGO

Mzee gharama ya banda hapo itatosha kweli kwa hiyo laki tatu yake?..hela ya chakula chanjo na madawa mengine?..au akinunua tu kuku unadhani inatosha?..atalala nao chumbani au atawalaza sebuleni?
 
Habari zenu wana JF. Nina sh laki moja na nataka kuingia kwenye biashara. Jen ni biashara gani itafaa nianzishe kwa hicho kiasi cha fedha? Tafadhali naombeni msaada wenu.
 
Back
Top Bottom