Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

spleen,
Nimekusoma umetisha mkuu, nimeanza vutiwa na jambo moja la kigeni katika taifa letu.... Kuagiza vitu kwa bei nafuu mtandaoni na kuuza.
 
Hii Imetulia kaka ni wazo zuri ukizingatia naskia mboga mboga kuanzia week mbili Neema inaanza unaweza anza Vuna kama bustani itaenda vizur.
ndio mkuu ni kila week mbili unavuna.
Matembele ukishapanda ndio imetoka utaendelea kuvuna mpaka miezi 6. Muhimu kila yakivunwa ni kuweka mbolea tu na kung'olea magugu.
Mchicha ukivunwa unakwatua tuta then unapanda tena. Kilo moja ya mbegu nafikiri unaweza kupanda tuta 3-4

Shamba unahudumia asubuhi na jioni.

Me nilikuwa nasoma so, shamba langu nilikuwa nahudumia jioni tu. Na mambo yalikuwa yanaenda vyema.
 
Samahani troubomeka!umeandika mbegu 40000! Ni mbegu gan hizo za mboga mboga!?
mbegu ya mchicha, (inafikia 10k+ nafikiri kwa kg1), msusa (maboga)
Matembele anaweza pata bure tu kwa wakulima wengine hasa wale ambao wanang'oa yale matuta yaliochoka.
 
😀😀 we nae hustler mpaka huku ushapita.
Kilo dar inafikaga mpaka 12000.
Hapo nimepigia apate kilo mbili labda za mchicha na kg 2 za maboga.
Tuseme mchicha alime matuta 4, matemble matuta 4. Maboga nayo matuta 2 au 4.

Nilianza na mchicha mkuu 2015!lakini ss hv hii biashara mhhh!
 
Inaenda kabisa. hii unatega sehem ambayo ina walengwa unatoka. Mfano hata wale wanapiga vyombo (watumiaji wa vilevi)
pia hiyo hela waweza nunua mbuzi mzima ukamchemsha soup, soup ya mbuzi huuzwa 2000. Unatega sehemu nzuri unauza wakati wa kuanzia usiku.
Baadae mtaji ukikuwa unanunua na jiko unauza na mbuzi choma.
 
Nilianza na mchicha mkuu 2015!lakini ss hv hii biashara mhhh!
mimi ilikuwa 2011 kurudi nyuma.
Mbona unaguna wakati mimi wakati nalima mtaani fungu tulikuwa tunanunua 100 ikapanda kidogo kufikia 200, lakini sasa hivi 250-500 kwa fungu kutegemeana na eneo
 
Shida vitu vya online mfano Ae kufika ni kazi
1.Biashara ya Karanga za kukaanga/mbichi
2.biashara ya mama ntilie
3.biashara ya miwa
4.unaweza nunua baiskeli ukakodisha kijijini
5.unaweza chonga mkokoteni ukakodisha kwa saa 1,000/=.
6.unaweza nunua nguo ama viatu vya mtumba ukaenda kuuza mtaani kwa kutembeza
7.ukafungua genge simple lenye mazaga yote mtaani
8.unaweza tumia kama ada ya kujifunza skills flani,gereji,kushona viatu,computer
9.unaweza itumia kununua na kujenga banda la kuku,kanga kwa ajili ya ufugaji
10.unaweza limia heka mbili za ardhi ifakara kwa ajiri ya kilimo cha mpunga
11.unaweza agiza vitu online vya USD 0.5 ukaja kuviuza kwa USD 2.5
Acha wengine nao wajazie
NOTE:kuweza kufanya kitu hiyo pesa na utayari wa mfanyaji ni vitu viwili tofauti.
Hiyo laki 1 unaweza lipia lodge na huyo malaya asije au unaweza walipia pombe rafiki zako na nyumbani bado wakalala njaa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa uzoefu wangu Hapo kwenye Namba 9, haitoshi Laki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom