Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

dogo una utani wewe. laki tatu ukanunue nguo mbeya mjini ili ukauze sumbawanga vijijini. mbona hiyo ni nauli tu.
 
Yani hiyo hela ni ndogo sana kwa biashara yako yakusafiri nakushauri ukanunue chenji uuze bara barani

ungekua Dar....hiyo pesa ninyingi sana kwani kuna Machinga pale wanaanza na msigi 50!000! Baada ya mda anampa msingi nduguye pale kuna biashara za Kurenga Tende.Maji Uhai NK lakini sio Nguo.
 
dogo una utani wewe. laki tatu ukanunue nguo mbeya mjini ili ukauze sumbawanga vijijini. mbona hiyo ni nauli tu.

nauli ninayo hiyo laki 3 kwa ajili ya kununua mzigo tu,nitajaribu kuwa mchumi zaidi,hata yeboyebo nitajumua tu nikauze
 
Nakushauri ujiunge na NETWORK MARKETING COMPANY hasa Forever living company ni sehemu pekee ambayo inaweza kukutoa na kuwa mfanya biashara mkubwa, ni biashara isiyo ofisi, isiyo hitaji kuajiri mtu wala leseni ya biashara. Ni inbox kama unahitaji kweli kufanikiwa kibiashara kwa mtaji mdogo
 
Laki tatu itakutoa kama una njia nyingine za kusustain maisha yako. Kama hela ya mboga na chumvi inatoka hapohapo, huwezi kutoka, utasurvive tu...
 
vijiji vya sumbawanga sivifahamu,chochote kile nitakachofika kama unavifahamu naomba unipe data ya vijiji ambavyo angalau nitauza

Kaka kwa ninavyokufahamu huko utafanya biashara katika mazingira magumu sana. Jaribu kupata ushauri kwa jamaa wanaofanya biashara ya namna hiyo huko.
 
Itakutoa tu. Ila usijiunge na maForever Living maGLND na madudu mengine ya network marketing. Jambo la muhimu kwa sasa uwe makini sana na matumizi yako. Kwa kipindi hiki cha mavuno ukifanya juhudi utauza sana. Ila kumbuka mwanzo ni mgumu usiwe mwepesi kwa kukata tamaa ukiona mambo hayaendi.
 
Fanya utafiti kwanza kama hitaji hilo la nguo lipo? Watu wengi wanashindwa biashara kwa kufikiria watauza tu bila kufanya utafiti. Hiyo sehemu unayotaka kufanya biashara watu wanahitaji hizo nguo, na je fedha wanazo? Hayo ni maswali ambayo lazima yajibiwe kabla hujaenda kujumua huo mzigo. Nakushauri ufanye utafiti wa kina kwanza. Ukiweza kugundua hitaji linalofaa hata mtaji wa elfu hamsini unamtoa mtu kama discipline ya biashara anayo!1
jf naomba mnipe mawazo kama kichwa cha habari kinavyojieleza,nina laki 3 nataka nijumue nguo za dukani then nipeleke vijijini nikauze kwa rejareja,

Kwa wale wazoefu wa biashara hasa za minadani hiyo pesa inaweza kunitoa kimaisha? mimi nipo sumbawanga mjini nataka kwenda mbeya mjini kujumua huo mzigo kwa hiyo pesa,naomba msaada wa mawazo
 
Ndugu hiyo inakutoa saana.Jaribu kwenda maeneo ya katandala, mazwi,bangwe ambako kuna population density kubwa.fungua banda dogo la kuuza chips,au machungwa kwa msimu huu,au tafuta gunia nne za mpunga na koboa uza rejereja kila gunia ni tshs 15,000 mara nne ni 60,000 per trip ingawa biashara hii huku kwetu ni kina mama zaidi.vilele sikuungi mkono biashara ya nguo kwani sasa hivi haina faida kama zamani.Anzisha biashara ndogo ndogo ila uwe mvumilivu saaana mwanzo ni mgumu ila utatoka tu.mawazo yangu tu
 
Piga mzigo kwa Sumbawanga laki 3 nyingi sana na ni mtaji tosha kabisa. Nimewahi ishi huko kipindi f'lani na nilijaribu kufanya research,vijana wengi wanaanza maisha kwa mtaji mdogo zaidi ya huo ulionao na baada ya muda wanatoka kimaisha. Muhimu kudhibiti matumizi yako na kuwa na nidhamu na kidogo ukipatacho.
 
haswa ni pesa nyng sana kwan wengne huanza na elfu 10 na kaa ukijua maisha ppte ila jitambue kwan utaweza.
 
unajua kuwa kila jambo ni mipango kama unaweza kujibana utafanikiwa maana co kila k2 uanze na pesa nyingi ila ni vizuri kama ukapata mtu ataye kuwa unamwagiza mzigo dar au hata mbeya kwa sehemu unaweza ila kama utasema utoke huko na uje dar utakuwa hujafanya kitu anzia kwanza kufanya mzunguko wa hiyo pesa ukiwa hukohuko
 
Nakushauri ujiunge na NETWORK MARKETING COMPANY hasa Forever living company ni sehemu pekee ambayo inaweza kukutoa na kuwa mfanya biashara mkubwa, ni biashara isiyo ofisi, isiyo hitaji kuajiri mtu wala leseni ya biashara. Ni inbox kama unahitaji kweli kufanikiwa kibiashara kwa mtaji mdogo

Acha kumdanganya mwezio...Hii biashara unasema unataka akate hiyo laki 3..Hapa Dar hiyo biashara inawashinda watu sasa huko sumbawanga si ndo itakuwa balaa?Atapata wapi huo mtandao wa watu wenye hela za kutosha kuzungusha hizo bidhaa?
 
Back
Top Bottom