Kaka nadhani haujafatilia vizuri, sio mimi nilioomba ushauri, ni mtu mwingine kabisa alienzisha huu uzi, nadhani swali hili umuulize yeye, mimi nimempa mawazo tu ni kipi afanye. Ila kama wataka kujua kama nishawahi kufanya moja ya biashara nilizozitaja hapo juu, basi nasema nishawahi kufanya tena sio kipindi nimemaliza chuo au nipo chuo hapana, mie biashara ilikua akilini zamani sana tokea nipo primari napiga dili, ila hasa nimeanza kukomaa nlivoingia form one, chochote kilichokua mbele yangu kwangu mimi ni oppurtunity, kipindi nipo form one mwaka 2012 nlikua na jamaa wawili mmoja anauza kahawa mwingine anauza biskuti maji pipi na mazaga tofauti karanga anatembeza, kila mmoja nlikua napiga faidi buku mbili jelo kwahiyo wawili inakua buku tano kwa siku, enzi hizo. mimi nimejilea mwenyewe nimejisomesha mwenyewe mpaka chuo nimemaliza mwaka 2011 nimepiga mwenyewe, nakumbuka kipindi nipo chuo kila mtu ana business ya ku print page moja mia, lakini mm nkasema niwe tofauti najua ku type vzr km secretary kwa spidi nzuri nkasema nijiweke nondo zaidi mwez mmoja tu nkawa fiti nkaweka tangazo kuchapa na ku print mia 5 wkt stationary mia 7, watu walikua wanamiminika mpaka nakataa kazi, nlikua pekeangu, kwa cku napiga mpaka elfu 20. na pia nkasema nisikae bure nkajifundisha kutengeneza computa na simu, nkawa napiga hela mzee mpaka elfu 30 kwa siku ukijumlisha na ya ku printi mpaka 50 daily, nipo chuo hapo. ukishajitambua ww umetokea kwnye familia isioeleweka ki uchumi bac ni kupigana tu kitaa, mzunguka bure sio mkaa bure, asietafuta na asile, lazima upigike ukitaka sukari, mtaji sio isue, isue ni kutokata tamaa tu. kpnd cha likizo cha A'levo watu wanaenda kupiga tuition mie npo stand ya daladala natafuta madili, ukienda mitaa yng kote najulikana Alwatan sichagui kazi, watu walikua wanasema yule jamaa si anasoma chuo lkn yupo stand anakomaa lkn mie sijali sisomeshwi na mshua nitapiga simu ntatumiwa, nakomaa mwnywe kila kitu. kua bilionea sio idea au talent, kwangu mm ni kukomaa na kutokata tamaa.
Hapo juu kwenye 2012 ni type error, nimemaanisha 2002 maana najua kuna watu watakurupuka hapa wenye kushkiliwa akili na wavivu wa kufikiri wataanza maswali, 2012 form one halafu 2011 umemaliza chuo, kwahiyo ile ni 2002. Ni hayo tu