Kwa mujibu wa Biblia, unaweza kujikuta wewe ni mmoja ya watu ambao Mungu aliwakataa hata kabla hawajazaliwa

Kwa mujibu wa Biblia, unaweza kujikuta wewe ni mmoja ya watu ambao Mungu aliwakataa hata kabla hawajazaliwa

Mkuu kwa upande wangu naona inaweza kuwa alimaanisha ya kuwa anajua matendo ya wale ambao angewachagua watatenda,kwa hiyo Mungu anawachagua walio wake kulingana na matendo yao. kumbuka sis wanadamu ni free moral agents tuko huru kuchagua..
Na ndo sababu mhubiri 7:1,2..inasema "SIKU YA KUFA NI BORA KULIKO SIKU YA KUZALIWA", unapokufa unakuwa umejiwekea rekodi ya kuwa ww n mtu wa aina gani.
Biblia iko zigzag. Mungu ana wateule wake, tangu mwanzo anajua wewe ni wa kundi gani. Mwandishi mwingine anasema unapo kufa ndio unajua umejiwekea historia gani!
 
Bwana anawafahamu walio wake, kwa hiyo kuna wengine ambao sio wake toka kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu ambao hawafahamu na hata siku akiwaona atashangaa maana hawafahamu, they never existed kwenye akili yake.

Kwa hiyo dini ni utapeli tu wa kupotezeana muda kwani mungu anawajua walio wake kitambo.
... kinyume chake ndio ingekuwa ajabu; Mungu asiwafahamu walio wake!? Zingatia; kabla ya kuumbwa ulimwengu alishaumba viumbe wengine na waliomtii anawafahamu toka enzi hizo (kabla ulimwengu kuumbwa) hadi sasa. Hao ndio walio wake.
 
Ili kuwasaidia wale wanaoweza kupotoshwa na bandiko lako,..

Walio wa Mungu ni wale waliouacha uovu, kama ukisoma mstari mzima 2Timotheo 2:19, imeandikwa "Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake, Na tena kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu"
Kila mwanadamu amepewa nafasi ya kuwa wa Mungu, hakuna ubaguzi, Yohana 3:16, " Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanae wa pekee ili KILA amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele"
Tena Yohana 1:12" Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu" Neno KILA na WOTE hayaonyeshi ubaguzi.

Kuna watu wanaojipambanua kuwa ni wa Mungu, lakini Mungu ana muhuri wake wa kumtambulisha mtu kuwa ni wake, nao ni utakatifu, ndiyo maana akasema anawajua walio wake, na siku ile ya hukumu atawaambia wale watumishi wanaohubiri na kuombea watu wakati wao ni walevi, wazinzi, waongo, n.k kuwa "Sikuwajua ninyi kamwe, ondokeni kwangu ninyi mtendao mauvu..." Mathayo 7:23.

Hapo anawafukuza kwa kutokuwajua kwa sababu gani? kwa sababu ya kutenda uovu.
Maandiko haya yatakusaidia pia Yohana 10:26-27.
 
Hoja yako ina ukweli kwa asilimia kubwa mno,ni hivi nilisoma utafiti wa kisayansi uliondikwa na David Acke,huyu ni muingereza anasema hapa Dunia kuna viumbe waliofafana na wanadamu lakini sio wanadamu.Anadai miaka millions zilizopita kulikuwa na viumbe ambao wanaitwa wanafelis ambao walifanya interbreed na wanadamu wenye asili ya Mungu,kwa lengo la kufanya shiftingshape..lengo lao nikuwa miongoni mwa wanadamu ili waweza kuwa control wanadamu kwa kugain political power.

Na kwa mujibu wa David Acke anasema hawa wanaasili ya Reptilians,nahisi kama sio DNA zao basi itakuwa RNA zai zinasoma kule kwa Reptilians.

Ili uweze kuwagundua kitabia
Wana Lower blood pressure
Wana unexplainable scars kwenye mili yao
Pia ni Evil sana kitabia
Pia wanauweo wa kuona mbali pasipo kutumia miwani
Hii nilimsoma katika The Children of the matrix yule father ata lecture zake kama kichwa umekaza huwezi kumuelewa kabisa.
 
2Timotheo 2:19Lakini msingi thabiti uliowekwa na Mungu uko imara, na juu yake yameandikwa maneno haya: “Bwana anawafahamu wale walio wake,” na “Kila asemaye yeye ni wa Bwana, ni lazima aachane na uovu.”
Wajibu wako ni kuachana na uovu kama wataka kuwa miongoni mwa wateule
Mathayo 22:14 inasema Wengi wamealikwa lakini wachache wameteuliwa. Hapo ni kwamba walio tii ndo wanateuliwa. Ukisoma kisa chote cha Mathayo 22 watu walialikwa na kupewa mavazi ya harusi lakini kuna mwamba kaingia bila vazi la harusi, huyo hakutii
Tii maagiza ya Mungu nawe utaitwa mteule
KWA ninavyojua MUNGU ana sifa ya OMNIPOTENCE mwenye nguvu zote, omnipresence aliyeko kila mahali, alafu kuna omniscience anayejua kila kitu. Anafahamu kabla hata ya kuwepo tumboni mwa mama yako. Kwanini tusiseme kwamba kuanzia adamu anatenda dhambi mpaka kufikia DUNIA ilipo MUNGU alikuwa anafahamu itakuwa hivi? Jaman mimi huwa najiuliza tu ila naamini katika uwepo wa MUNGU. Naomba mwenye jibu anisaidie tuelimishane
 
Nitajuaje Mungu ananitambua ili nimuabudu? Mtu unaweza kupasua Sala mchana na usiku kumbe hakutambui na wala hajui kama upo duniani. Atheists ndio wanaoishi kwa raha, wao hawaangalii makunyanzi.
 
Ukisoma Biblia , 2 Timotheo 2: 19 Mungu anasema yeye anawajua watu wake hata kabla hajaumba misingi ya ulimwengu.

Ukisoma tena Mathayo 22:14 Biblia inasema walioitwa ni wengi lakini wateule ni wachache.

Kwa msingi huo wewe unaweza ama inawezekana umeitwa tu, yaani umekuja tu Duniani lakini Mungu alishakukataa toka hujazaliwa, yaani kabla hata hajawaza kuumba Ulimwengu (Universe).

Kwa msingi huo ni kwamba unaweza kujikuta wewe ni reject from the beginning. Hata ufanyeje, wewe ni reject tu.

Kwa maneno hayo ya Biblia ni kwamba Mungu aliumba watu wengine kuja duniani kufurahisha na kupoteza muda, hawana chao mbinguni hata wafanyeje, yaani unaweza kujikuta unaomba na kulia machozi yote na hata kunena kwa lugha mungu akini hujibiwi maombi ni kwa sababu wewe ni reject muda mrefu maombi yako unapoteza muda bure

Wa maana nyingine unaweza kujikuta Mungu anakuangalia tu na kucheka na kusema huyu angejua anapoteza tu muda hapa, ananipigia kelele kwani tayari alishakukataa kabla hujaumbwa.

Unaweza kusema kwamba mungu aliumba hii dunia na watu kwa ghelesha tu lakini nia yake na mipango yake alishaipanga huko kabla Dunia haijaumbwa na huna cha kufanya kuibadilisha.

Kwa kuhitimisha ni kwamba hizi dini ni ghelesha tu, hazina maana yoyote kwani mungu alishafanya maamuzi yake kabla hata ya kuja hizi dini.

Sijataka kuongelea Quran maana ile ni worst case.
Hizi dini kuzifuata mkuu sharti uwe si mtu wa kuhoji na kutumia logic.
ngoja mfia dini aje hapa atudadavulie juu ya hayo mambo 3.
  1. Tumezaliwa na dhambi ya asili kwaiyo we are just unworthy piece of s##t from day we arrived on the planet.
  2. You can only be saved by believing in the savior , and that means doing what the priesthood tell you to do.
  3. If you don't do that , you will be condemned to the bowels of hell forever.
KIUKWELI UHITAJIKUWA NA IQ kubwa kutambua kuwa kunajanja janja inafanywa na jamii ya watu kuwahadaa waAFRICA.
 
Nitajuaje Mungu ananitambua ili nimuabudu? Mtu unaweza kupasua Sala mchana na usiku kumbe hakutambui na wala hajui kama upo duniani. Atheists ndio wanaoishi kwa raha, wao hawaangalii makunyanzi.
Dini ni mipango ya watu kupiga hela, kukuamulia jinsi ya kuishi, kufikiri na kuamua mambo.

Ukifuata dini unakua kama liloboti.
 
Kuna Binadamu na Watu.

BinAdam Ni uzao wa Adam ... Ila Wa-tu ..ndio wale waliokuwa upande wa pili mbali ambako Kaini alikwenda kuishi baada ya kulaaniwa na kutiwa alama kwa kosa la kumuua ndugu Yake!

Patamu hapo.. ..Ni kwamba huwezi jua au kutofautisha Kati ya Binadamu na Watu!inaweza kuwa hata Mimi na wewe sio binAdam!

Na hapo hapo Adam mwenyewe si bin Adam .Ni Adam!
Una weza kuwa binadamu ila sio mtu , mtu anatokana na utu , kama huna utu wewe sio mtu ila ni binadamu. Ili uwe mtu inakupasa uwe na utu , ila kuwa binadamu ni lazima bila hata kuwa mtu.
 
Shida yenu huwa mnaisoma Biblia na kuitafsiri vile vile na Mara nyingi huwa mnakosea katika tafsiri zenu.

Oyaa Biblia sio kitabu Cha kawaida Kama vitabu vya shuleni.Hicho Ni kitabu kitakatifu Sana na Mara nyingi huwa nashauri kabla hujaifungua Biblia na kuanza kuisoma, muombe Mungu akupe uwezo wa kuelewa kile utakachokisoma bila kupotosha maana iliyokusudiwa.
 
MKUU kabla ya kusoma biblia kuna prior knowledge itakupasa uwenazo.

nimegundua unakaFEAR flani ndani yako
 
Shida yenu huwa mnaisoma Biblia na kuitafsiri vile vile na Mara nyingi huwa mnakosea katika tafsiri zenu.

Oyaa Biblia sio kitabu Cha kawaida Kama vitabu vya shuleni.Hicho Ni kitabu kitakatifu Sana na Mara nyingi huwa nashauri kabla hujaifungua Biblia na kuanza kuisoma, muombe Mungu akupe uwezo wa kuelewa kile utakachokisoma bila kupotosha maana iliyokusudiwa.
ungesema tatizo hatuishi na kufuata maagizo tuliyopewa kwenye biblia ningekuunga mkono.
 
Saa nyingine ukisoma sana mambo ya dini unaweza kuchanganyikiwa. Kwa mfano Yesu alimwambia Petro utanikana.. sasa kama ilikuwa hivyo si angemuepusha tu Petro hilo lisitokee? Ukienda agano la kale wale waisrael walipotoka Misri hawakuwa na pa kufikia kwahiyo walikuwa wakikuta mji wanaushambulia na kuwaua wenyeji wote.. kiongozi wa yale mauaji ya kutisha alikuwa akiitwa Joshua. Na kwenye mchakato wa yale mauaji alikuwa na usaidizi wa karibu sana wa Mungu. Dini zetu za mizimu nadhani ni bora sana kwasababu hazina huu upuuzi wa kupanikisha watu.
 
Nahuko kuchanganyikiwa ni sehemu ya ajenda ya walioandika hicho kitabu.

don't take it too serious bro.
kinamafundisho mengi na mazuri sana pia kina burudani kibao drama za kutosha.

japo iliniuma mussa hakutoboa kufika nchi ya ahadi.
hahahahaha
 
Saa nyingine ukisoma sana mambo ya dini unaweza kuchanganyikiwa. Kwa mfano Yesu alimwambia Petro utanikana.. sasa kama ilikuwa hivyo si angemuepusha tu Petro hilo lisitokee? Ukienda agano la kale wale waisrael walipotoka Misri hawakuwa na pa kufikia kwahiyo walikuwa wakikuta mji wanaushambulia na kuwaua wenyeji wote.. kiongozi wa yale mauaji ya kutisha alikuwa akiitwa Joshua. Na kwenye mchakato wa yale mauaji alikuwa na usaidizi wa karibu sana wa Mungu. Dini zetu za mizimu nadhani ni bora sana kwasababu hazina huu upuuzi wa kupanikisha watu.
Agano la Kale ni Jino kwa Jino na Jicho kwa Jicho

Agano Jipya ni Upendo, ukipigwa kofi kushoto geuza kulia na usirudishe kofi, ukipokonywa koti mpe na shati, akikupora viatu mpe na soksi, akikuchojoa suruali msusie na boksa kabisa kisha baki uchi
 
Back
Top Bottom