Maana Kwa taarifa zilizopo ni kama wameifanya nchi ya Syria bila nguvu za kijeshi kwa mwashumbulizi yake waliyoyafanya ndani ya Syria.
Na huko Gaza anashusha tu mabomu anavyotaka. Ile kauli ya Irani kuwa watashughulika na Israel imekuwaje tena?
Muogope Mungu na Teknolojia .
Wale watu wana Teknolojia nzuri sawa na Mataifa makubwa Duniani japo ni nchi ndogo.
Lakini pia katika Ulimwengu wa Roho Israel ni Taifa linalofanya Dunia imtaje Mungu aliyeumba vitu vyote ,yaani Mungu Mwenye nguvu nyingi kuliko Miungu yote.
Dunia inataja miungu mingi sana lakini Kuna Mungu aliyetajwa sana na taifa la Israel ,huyo ndiye anayesadikiwa kubwa aliumba vitu vyote na miungu yote pia imeumbwa na yeye. Ni asili ya vitu vyote .
Ili kuifanya dunia istarabike basi ni Lazima wetu waishi kwa amani na Israel. Vinginevyo dunia inakosa amani.
Waarabu pesa wanazotumia kufadhili ugaidi wa kuishambulia Israel wangezitumia kuwawezesha wananchi wa Palestina na kukaa chini na Isarel ili wakubali kuweka mipaka upya na kukubaliana bila kulipua mabomu leo hii wapelestina wangekua kama watu wa Katari.
Mfano Marekani inatoa pesa nyingi kuisadia Isarel kujenga uchumi na maisha ya watu ikiwemo kujenga viwanda na miundo mbinu .
Kwa sababu Waarabu kujaribu kuwatoa Waisaraeli pale ni sawa na waafrika kuungana na kuwasadia Wasauzi Afrika ili wawatoe wazungu Pale Afrika Kusini na kuwarudisha Ulaya . Mtiti wake utakua sio wa dunia hii. Ulaya yote wataungana na Wazungu wa Afrika kusini kwa sababu hawatakubali warudi Ulaya maana hawana sehemu yao kule Ulaya tena .
Ni Akili tu ya Kawaida huwezi kuwafukuza Waisraeli Pale Mashariki ya Kati tena. Hata Ikitokea vita ya tatu ya dunia. Watauana mapaka mwisho . Kwa hiyo waarabu walitakiwa waondoe chuki za kidini wakubaliane na ukweli kuwa Israel hawawezi tena kukimbia nchi yao kwa vitisho vyao magadi au hata vita.
Kama ni ngumi zinapigwa mpaka raundi 12 hakuna kukimbia jukwaa.
ILakini pia ni vita inayoigawa dunia pande mbili. na ni wazi kuwa Upande wa Isarel ndio wenye nguvu. Hata China ,India ,Japan ,Urusi Korea bado hawaoni sababu ya kuishambulia Israel inapopambana na magaidi.