Lete facts mkuu.
Kama umasikini hata Dar ni masikini sana. Dar ina umasikini kwanza ambao haujaisha ndio unataka Pwani ilingane na Dar kimaendeleo?
Haya Pwani wavivu, Singida, Rukwa, Kigoma nako ni nini kimewapata?
Halafu usiongee sana, Wasukuma wanahamia kwa wingi Pwani. Wanadhani wakazi ni wavivu. Wakifika mtu mmoja analima heka nyingi akidhani ni rahisi kutunza shamba. Wanagundua ardhi na majira ya Pwani si kama kwao usukumani. Pwani inapokea mvua nyingi, palizi ni nyingi, magugu yanaota after 2 weeks hata upulize dawa gani. Ndipo wanajifunza kulima kwa akili badala ya nguvu.
Haya tuambie, watu wa Mbeya wangefanya nini Pwani?