Kwa nionavyo, mikoa inayoongoza kwa uvivu ni Lindi, Mtwara, Pwani na Tanga

Kwa nionavyo, mikoa inayoongoza kwa uvivu ni Lindi, Mtwara, Pwani na Tanga

Ukiwataja watu wa Lindi majority huko ni Waislamu mkuu kua makini Misikiti ni mingi kuliko makanisa 90% nyumba za Ibada ni Misikiti ikifuatiwa na Kilwa sijui ni Mkoa au ni Wilaya
Udini usiwekwe hapo mkuu, Chalinze kuna kata nilifika nilikuta vijiji vina wakwere wakristo wa kutosha...
 
Udini usiwekwe hapo mkuu, Chalinze kuna kata nilifika nilikuta vijiji vina wakwere wakristo wa kutosha...
Sasa hio Chalinze ni Wapi haujui kule Wamishionari walipachika Misalaba yao kabla hata ya Uhuru, unataja wakwere haujui unaizungumzia Bagamoyo haujui Bagamoyo ndio kuna Kanisa kongwe kuliko yote Nchini
 
Utapia mlo sio kukosa chakula tu.

Unakuta mtu amerundika magumia mia yaahindi ndani ila familia ina utapia mlo. Hii husababishwa na mambo mengi ikiwemo.
1. Uandaaji wa chakula.
2. Mda wa kula - Mikoa ya Bara Mingi wazazi wako busy na kazi hadi wanasahau kuwapa watoto chakula kwa mda sahihi
3. Usafi.

Hizo ni baadhi tu.
Kwa ukanda wetu Chakula si shida,,,watu wanakula na vyakula bei nafuu sana...

Hapo hiyo utapiamlo bara labda iwe Kaskazini na Kanda ya kati....

Kuna Msafwa au Mnyakyusa kishikonda.
 
Sasa hio Chalinze ni Wapi haujui kule Wamishionari walipachika Misalaba yao kabla hata ya Uhuru, unataja wakwere haujui unaizungumzia Bagamoyo haujui Bagamoyo ndio kuna Kanisa kongwe kuliko yote Nchini
Ndiyo mana nkasema ishu siyo dini ila Mazoea ya wakazi husika...

Mana mfano Kagera ina ardhi nzuri,ipo mpakani,ina maji...ila ni Maskini wa kutupa,,kumbuka Kagera ina Wakristu wengi sana..makadinali wote wa Tanzania wametokea huko.
 
Ndiyo mana nkasema ishu siyo dini ila Mazoea ya wakazi husika...

Mana mfano Kagera ina ardhi nzuri,ipo mpakani,ina maji...ila ni Maskini wa kutupa,,kumbuka Kagera ina Wakristu wengi sana..makadinali wote wa Tanzania wametokea huko.
Nasemaje wewe haujanielewa nimesema kwamba mleta mada anapogusa Lindi asisahau Lindi 90% ni Waislamu wakristu ni wa kuhesabu kwa hio hapo aliposema hawana ukarimu wachoyo wana midafu Ila unapiga kazi hupewi hata dafu na wana minazi kibao, nikamwambia hapo unagusa ndugu zetu katika Imani sio kabila lao wala Mkoa wao
 
Wanaandikisha. Rate ya kumaliza form four ni ndogo na waliomaliza shule nzima inaweza kula yai (division zero)! Ndo maana nikasema hawapendi kusoma. Yaani ni nadra kukuta cheti cha form four kilichonyooka. Haimaanishi hawapo kabisa;
Shule zipo ndo maana mimi nimesoma huko! Kumbuka shule ya advance inachukua wanafunzi kutoka popote!
Shule za Arusha somo moja walimu wamezidi,shule za pwani, Lindi mtwara Kuna upungufu wa walimu,nani alaumiwe hapo!?
 
Kilimo, Migodi,Biashara,Ufugaji,Uvuvi....
Fika Kahama, Tunduma, Ilala, Kyela,Z.Victoria...utaona wachapa kazi.
Ilala wachapa kazi!?..kumbe hata bila kutumia nguvu ni kuchapa kazi!?... mtwara na Lindi hawana korosho!?..hawavui!...hakuna mgodi ruangwa!?hakulimwi karanga huko!?
 
Shule za Arusha somo moja walimu wamezidi,shule za pwani, Lindi mtwara Kuna upungufu wa walimu,nani alaumiwe hapo!?
Walimu wanatoka mikoa yote kwani wao hawawapi nafasi walikua Wazawa wa huko huko kwao?
 
Mkuu,Arusha wanaongoza kwa kuzalisha Mazao ya Maua hapa nchini.. Meru na Arusha mjini.

Arusha wana mifugo ya kutosha...Monduli na Longido
Arusha wana utalii wa kutosha.....

Na hapo hapo kumbuka Arusha kuna sehemu ni kame, lakini wamjiongeza.

Sasa uje ,Lindi yetu....dah
😅😅😅Acha utani maua hayo mashamba ya wazungu ,Sasa huoni kila jamii na utamaduni wake.

Arusha unaifikia Mombasa kwa maendeleo!? Jaribu kutembea Sasa Dar wanalima nn?
 
Ilala wachapa kazi!?..kumbe hata bila kutumia nguvu ni kuchapa kazi!?... mtwara na Lindi hawana korosho!?..hawavui!...hakuna mgodi ruangwa!?hakulimwi karanga huko!?
Hahaha mdau kalenga Lindi sio Mtwara Mtwara haipo hapo kule watu wanapiga kazi atakua hajatembea akaona
 
Mkuu katika nchi yangu hii, mimi nishafika Mikoa takribani 25,hapa nakupa data za kujionea kabisa...View attachment 2960178
Katika hiyo mikoa mitano ya mwisho, Pwani na Kagera mna matatizo kwakweli, kwa maana wote mna Ardhi ya kutosha na yenye rutuba masoko yapo, wasomi ila dah...

Singida,Dodoma na Tabora ni kame ,yani kame kwelikweli...ndiyo mana hata haishangazi kuwaona hapo.
Utakua huijui pwani,pwani in rutuba gani na imejaa mchanga kasoro kisarawe ina mfinyanzi!?
 
Lete facts mkuu.
Kama umasikini hata Dar ni masikini sana. Dar ina umasikini kwanza ambao haujaisha ndio unataka Pwani ilingane na Dar kimaendeleo?
Haya Pwani wavivu, Singida, Rukwa, Kigoma nako ni nini kimewapata?

Halafu usiongee sana, Wasukuma wanahamia kwa wingi Pwani. Wanadhani wakazi ni wavivu. Wakifika mtu mmoja analima heka nyingi akidhani ni rahisi kutunza shamba. Wanagundua ardhi na majira ya Pwani si kama kwao usukumani. Pwani inapokea mvua nyingi, palizi ni nyingi, magugu yanaota after 2 weeks hata upulize dawa gani. Ndipo wanajifunza kulima kwa akili badala ya nguvu.

Haya tuambie, watu wa Mbeya wangefanya nini Pwani?
Umenena haswa
 
Mapori Pwani unashangaa leo?
Kigamboni juzi tu ilikua mapori mpaka Kibada.
Mbezi, Mabwepande, Kibamba,Mpigi Magohe, Magole huko Kitunda ndani ndani, Pugu miaka ya karibuni bado yalikua mapori. Sasa kama Dar bado ina mapori Pwani inasalimika vipi?

Impact ya uvivu wa Pwani inaonekana wapi? Humo unamosema mapori unaona minazi, mikorosho, miembe na michungwa ina maana watu waliima wakapanda. Hebu tufanye ziara hadi Mkuranga tuone msitu usio na mazao hayo ya kudumu.
Kumiliki mashamba ya minazi, mikorosho, miembe, miwa, michungwa ni dalili ya uvivu. Huhitaji kwenda shamba mara Kwa mara. Utashinda kucheza BAO tu.
 
Hata kwa Uvuvi, bado sana, hakuna hata Wilaya moja Pwani inayofikia Mwanza kwa uvuvi....
Yani usijifichie huko,wakati Mkuranga,Kisarawe,Kibiti na majority ya Chalinze ni mbali na bahari...

Mkoa ni mapori ,watu hawalimi,,kutwa Ngoma.
Mkuu kwa taarifa tu wilaya ya Mkuranga imepakana na bahari ya Hindi kwa upande wa Mashariki.

Tarafa ya Kisiju Pwani, Mkuranga zote zimepakana na bahari.

Fanya tafiti kidogo
 
Back
Top Bottom