Nimetembea kote Tanzania hii Mpaka kigoma nimefika ila asee usijiloge mikoa ya kusini ni hatari Sana kama ni mtu unayetegemea majamaa wakuletee maendeleo..
Watu wa huku wanakatisha tamaa Balaa yaani hata ukisema uwasaidie inakula kwako ila nafuu kidogo Mtwara Dangote amekuja kuchangamsha na Tanga kidogo kuna mchanganyiko wa watu sio kama singida au dodoma unaalikwa kiroho Safi ila sio Lindi Kwa wamwera aisee huku sio poa Dunia ya Lindi hakuna kabisa ukarimu unaenda kijijini kufanya kazi sehemu mtu hakupi hata dafu na ana minazi kibao sio kama mbinga au songea Kule utafaidi sana kibaya zaidi hakuna watu wa kufuga mifugo hakuna mtu anafuga hakuna nyama nyoma na kachumbari yaani ni shida.
Na kwanini mikoa iliyo nyuma wasipewe ma RC wachapakazi kama makonda, mtaka, chalamila.. Nashangaa mikoa mzuri kama Arusha wanapelekwa viongozi wazuri wa kuliamsha.
Swala LA mikoa ya kusini, ni tamaduni na Mila, hawasathamini elimu,jamii haina msukumo wa elimu, kule ni unyago tu,
Mama ntilie wa kagera, anawaza Sana elimu ya mwanae, anajisghulisha sana kuhakikisha mtoto wake anafikia kiwango kikubwa cha elimu kadri uwezo wake utaksvyoruhusu, ansjisikia vibaya kuona watoto wa jirani wamefaulu wake wamefeli!
Jamii inakuwa na mshawasha kujua mtoto wa nani kafaulu, nani kafeli!
Kusini hakuna hiyo!uende shule poa, usiende poa, kule ni unyago tu, binti akipata mimba sio kesi! Binti asiporudi hm usiku,kaya inaona afueni mdomo mmoja umepata mwenzie, sehemu ya kula na kulala!
Tatizo LA kusini, ni by design wanasiasa wanapendelea wananchi wabaki maskini ili wawatawale kirahisi,
Juzi,nimeona clip wananchi wa singida wakisukuma V8 la waziri mbunge wao Mwigulu, umaskini wao umefikia kiwango kikubwa wanaona kugusa V8 ni, kama ufahari, kila MTU anapigania kuligusa!
Hakuna mwananchi anayeishi kwenye mitaa ya masaki, oysterbay, ambaye anaweza kupoteza muda wake kufanya ule upuuzi