Kwa sasa sipo tayari kuolewa, nahitaji kufanya mambo yangu

Sio mpaka uzeeni mkuu mwanamke akifika 30 tu anaanza trip za kwa mwamposa na waganga wakati mwanaume huo umri ndio kwanza kuna pambazuka
 
Mkuu hapa hatuongelei whether jinsia fulani kufanya jambo fulani ni kosa au la, bali tunaongelea uwezo wa kila jinsia ku multi task na ku catch up kufanya majukumu ya mwenzie, wewe unanitajia majukumu ambayo obviously ni ya wanaume na wanawake wengi wanayafanya siku hizi

Halafu kaa ukijua wanaume wanafanya hayo majukumu kwa sababu tu kuna vitu wanatarajia wavipate toka kwa hao wanawake, mfano kufanyiwa kazi za ndani, kulelewa watoto wao, kupewa heshima na utii nk, hakuna mwanaume anayeweza kukubali kufanya hayo majukumu ikiwa hapati hivyo vitu toka kwa mwanamke wake

Sasa je mnapolinganisha na wanawake kwamba eti wao hawawezi kufanya hivyo kwani hata wakifanya wanapata nini in return, je mnawasaidia kazi za ndani, je mnawasaidia kulea watoto, je mnaweza kuwapa heshima na utii kama wanayowapa ninyi, kama hamuwezi basi hiyo ndio sababu wanawake hawawezi kujitoa kama ninyi sababu they get nothing from you in return
 
Sio mpaka uzeeni mkuu mwanamke akifika 30 tu anaanza trip za kwa mwamposa na waganga wakati mwanaume huo umri ndio kwanza kuna pambazuka
Wanawake wengi wanaenda kwa manabii si kwamba eti ni kweli wanazihitaji sana hizo ndoa bali ni ile pressure tu inayosababishwa na jamii kwamba mwanamke akifika umri fulani hajaolewa anaonekana malaya, na ndio maana hata wengi wao wakizipata hizo ndoa bado wanaenda kusumbua huko ndoani na kufanya waume zao walete malalamiko humu mitandaoni, ukitaka kujua kwamba hitaji la ndoa siyo nature ya wanawake wote duniani jiulize kwanini kwa wazungu hayo mambo ya wanawake kuhangaika kwa manabii kisa kukosa ndoa hayapo, kule hata mwanamke mwenye miaka 50 anaolewa haijalishi ana watoto au la ila hayo mambo ya kuhangaika kwa manabii yapo huku afrika tu, ambako wanawake wanaexperience some stupid gender stereotypes called 'nature'
 
Wanaume wanachokuwa wanakitafuta ni wanawake ambao kiumri ni wadogo na ndio umri sahihi wa kufanya ndoa nao.

Huko uzeeni ni kusindikizana tu kusiwe na upweke. At all these points hakuna sehemu mwanaume anahitaji zaidi ndoa ni swala la muda gani muafaka wa kuanzisha jambo fulani na sio kulihitaji kuliko fulani.
 
Inaelekea bado haujaelewa matrix ipoje. Kimsingi mwanamke ndoa kwake ni jambo automatic hawezi likimbia bali analikimbiza.
 
Mkuu wanaume ni wabinafsi sana hamna na hamjawahi kuwa na huruma, wadanganyeni hao mabinti wa 2000 ila sisi tunaelewa how the shit goes, mnaoa kwa sababu mnahitaji ndoa period..wala hakuna sababu nyingine

....
Screenshot hii comment halafu subiri miaka kumi ukiendelea na hizi hizi fikra halafu njoo uje kuisoma tena. Nakuhakikishia utajichukia.
 
Sasa majukumu ya mwanaume hali ya kuwa unaniuliza kama tunaweza kulea watoto, kupika na kazi za nyumbani, hayo ni majukumu ya kiume?

We kubali tu wanaume wanabeba majukumu kuwazidi, heshimu hilo.

Huwezi pingana na asili, kujibebesha majukumu ya kiume hamuwezi, utavunjika.
 
Ukitazama hao wanaume wote ni wana uwezo wa kifedha halafu wanataka kuoa mabinti wadogo huku wao umri ukiwa umekwenda, unajua sifa ya binti aliye katika umri mdogo kwa mwanaume mtu mzima? [emoji848]
 
Punguza maigizo ya maisha ya watu wa nchi za Magharibi we Dada halafu inaonekana una chuki na Wanaume au walishawahi kukutenda?
 
πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚
Aisee inabidi utafute msaada wa kiroho na msaada wa kisaikolojia
 
She doesn't want to be controlled
 
"Kwa sasa sipo tayari kuolewa nahitaji kufanya mambo yangu"

Hayo maneno wanaambiwa wwnaune wasio na pesa
Niwe na Tsh ngapi nisiambiwe haya maneno ? (Kiasi gani cha pesa).

Huyo anaeiniambia hivyo anakuwa katika hali gani ya kiuchumi ?.


Ninashauku ya kuambiwa hivyo, ila nikuhakikishie tu huku uswahilini kwetu hio kauli hutamkwa na binti asiejitambua tu.

Tumezoea vizinga vyetu elfu mbili mbili mwisho elfu tano. Labda huko kwenu ulipo UKWASI.
 
Ndio hata kwa wanawake pia ni suala la muda gani muafaka wa kuanzisha jambo fulani na si kwamba wanalihitaji zaidi kuliko wanaume, ninyi wenyewe ni mashahidi mara ngapi mnalalamika kwamba mkiwa vijana huwa mnawatongoza mabinti kwa lengo la kuwaoa ila ni wao ndio hukataa, sasa kwa mantiki hiyo nani anayeanza kuhitaji ndoa mapema kwanini ninyi muanze kuwaza ndoa mkiwa vijana ilihali wanawake ni hadi watumike ndio waanze kuwaza ndoa
Inaelekea bado haujaelewa matrix ipoje. Kimsingi mwanamke ndoa kwake ni jambo automatic hawezi likimbia bali analikimbiza.
Ni jambo automatic kwa kuangalia jamii gani mkuu lazima tuangalie hali ikoje kwa wanawake wote dunia nzima, acheni kuongelea wanawake wa kiafrika ambao wote tunajua wazi na kipi kinachowapelekea wao kuwa na pressure ya kuhitaji ndoa, kuna nchi huko magharibi nimesikia wanawake wameanza kugoma kuzaa hadi viongozi wa kisiasa imebidi waingilie kati na kuwabembeleza wazae akiwemo Dikteta Kim Jong Un wa North Korea sasa hili linatakiwa liwape picha halisi ya wapi tunaelekea
Screenshot hii comment halafu subiri miaka kumi ukiendelea na hizi hizi fikra halafu njoo uje kuisoma tena. Nakuhakikishia utajichukia.
Kama bado nitakuwa hai hata iwe miaka mingapi mbele siku mkiona nimebadili hii mitazamo yangu, basi nawaombeni mnikamate mniwahishe hospitali yoyote ya wagonjwa wenye matatizo ya akili, inaweza ikafika wakati nikaacha tu kuhangaika kushusha magazeti kama hivi kuhusu hizi mada za mapenzi na mahusiano lakini kamwe misimamo yangu haiwezi badilika
Ukitazama hao wanaume wote ni wana uwezo wa kifedha halafu wanataka kuoa mabinti wadogo huku wao umri ukiwa umekwenda, unajua sifa ya binti aliye katika umri mdogo kwa mwanaume mtu mzima? [emoji848]
Hapa nimeongelea umuhimu na uhitaji wenu wa ndoa sijaongelea nani anamuoa nani katika umri gani, kitendo cha kuoa tu haijalishi mnaoa mabinti au wazee wenzenu bado kinaonesha uhitaji wenu wa ndoa hata kama mna pesa, hivi unaweza ukafananisha uzee wa mwanamke asiye na ndoa na uzee wa mwanaume asiye na ndoa nani anayeteseka zaidi ya mwenzake
 
Ndio hiyo ndio ilikuwa hoja yangu kwamba kati ya wanaume na wanawake, ni kina nani wanaoweza ku multi task na ku catch up kufanya majukumu ya mwenzake, bila kuhitaji msaada toka kwa jinsia nyingine

Hapa suala siyo kupingana na asili wala kujibebesha majukumu ya kiume bali suala ni wanaume kuanza kukimbia majukumu yao, kwahiyo mlitaka wanawake waendelee kuwabembeleza ninyi kufanya majukumu yenu, kana kwamba wao hawana akili na uwezo wa kujifanyia hayo majukumu

Ni majukumu gani hayo ambao mnayabeba kutuzidi hebu yaweke hapa, au ndio utaleta habari za vita na kupambana na majambazi sijui ujinga gani, kana kwamba nayo ni sehemu ya maisha ya kila siku au kwamba wanaume wote lazima wapitie hayo
 
Punguza maigizo ya maisha ya watu wa nchi za Magharibi we Dada halafu inaonekana una chuki na Wanaume au walishawahi kukutenda?
Mjomba kwani watu wa magharibi siyo watu wewe hapo ulipo umewazidi nini watu wa magharibi, mnataka tutolee mifano ya wanawake wa kiafrika tu ilihali sisi tunaangalia hali halisi kwa wanawake wote duniani, mkiambiwa ukweli mnakimbilia kudai eti tunawachukia wanaume je hawa wanaume wenzio wanaoshinda wanadhalilisha wanawake mbona huwaulizi kama wana chuki na wanawake
πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚
Aisee inabidi utafute msaada wa kiroho na msaada wa kisaikolojia
Mnaohitaji msaada ni ninyi wanaume ambao bado mnalazimisha kuishi kwenye fantasy badala ya kuja kwenye reality, seriously most african men need a reality check sababu ni kama bado hamtaki kukubali kwamba wanawake ndio wameshabadilika hivyo, mtaendelea kuwatukana na kuwatishia ndoa sijui ujinga gani ila wenyewe hawajali ndio kwanza wanazidisha maovu halafu mwisho wa siku ninyi ndio mnaishia kuumia kihisia kwa kukosa wake wema mnaowataka
 
Kwa kweli ukahaba/prostitution ni janga kubwa sana, tendo la ndoa limebinafsishwa watu wamepewa uhuru wa kufanya ngono na kuuza na kununua ngono wanavyojisikia, hata wakiingia ktk ndoa mambo yanaendelea yale yale, sometimes walioolewa wana madanga/clients kuliko wasiiolewa.
 
Nimeshakujibu kwa maelezo na mifano kuhusiana na swali lako sasa sijui katika maelezo yangu hujapata la kukusaidia, ama umekaza kichwa hutaki kufungua kichwa na kukubali ukweli mchungu, kama umekaza kichwa hapa hatuwezi kuelewana hata nielezee vipi hauwezi kunielewa.

Mwanaume ana uwezo mkubwa kufanya majukumu ya mwanamke kuliko ambavyo mwanamke angefanya majukumu ya mwanaume hata wakibadilishana, hili halina ubishi hata wanawake wenzako watakiri juu ya hili, ndio maana nimetoa mifano mingi tu ya kueleweka.

Kama unataka kuelewa utaelewa kama upo hapa kwa ajili ya kubisha basi nitakua natwanga maji kwenye kinu, hata niandike kitabu hutonielewa na hauna huo utayari.

Kingine tunatokea background tofauti katika malezi, utofauti katika jamii n.k.

Inawezekana unapotoka hujashuhudia mwanaume akipika, kuosha vyombo, kufua na kazi nyingi za nyumbani.

Familia ninayotokea mzee wangu alikuwa anafanya kazi zote nyumbani kipindi nipo mdogo, kuanzia kupika hadi kufua, usafi nyumbani na kila kitu kwa miaka hadi naanza kujitambua.

Mimi hakuna kazi ya nyumbani itanishinda, hata kupika biryani napika na sioni huo ugumu wowote ambao unasemwa kufanya kazi za nyumbani.

Wanaume wengi hizo kazi za nyumbani wanafanya sana tu, kuna zile familia unakuta kuna watoto wa kiume tupu utakuta wanafanya kazi zote za nyumbani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…