Kwa tabia hii una tofauti gani na Ibilisi?

Naam ibilis

Mungu aliumba kila kitu lkn kwakuwa yeye ndio muumbaji basi huwezi sema ana sifa mbaya

Yeye anajinasibisha na sifa sifa nzuri nzuri kabisa
Na je kila kilichopo duniani mungu aliumba yeye au matokeo ya fikra za watu
 
"Basi akawateremsha wao kutoka kwenye daraja zao kwa hadaa, na wakati walipouonja ule mti zilidhihiri tupu zao{baada ya kuwa ni zenye kusitiriwa} na wakaingilia {wakaanza} wanajifunika majani ya mti huko peponi na akawaita wao mola wao akiwaambia je! kwani sikuwakatazeni kula mti huo? na kwani sikuwaambia nyinyi hakika shetani Iblis Bin Shetan kwenu nyinyi ni adui mwenye kudhihirisha uadui?.."

Quran 7:22


uasi wa aadam alayhi ssalaam ni kwa ushawishi wa shetani unayemsifu hapa.
 
Naheshimu maoni yako mkuu

Karibu sana
Huo mfano wa CEO ndo umekosea.

Nina real life experience, nlikua kiongoz sehemu fln kwenye branch mojawapo ya barrick, yalonikuta sitosahau, lkn usijepoteza muda wako na masikini, watu wa chini ni watu wa chini tu. Bora wakuone una kiburi kuliko kuwajalu halafu haohao waje wasababishe yakutokee puani.

Nlipoteza cheo kisa huo upuuzi na sitorudia tena kujifanya najali watu wa chini, wapande ladder wenyewe wafike
 
Hili andiko lilikuja uadui wa iblis na mwanadamu pale alipoambiwa amsijidie na hapo adam yupo na hawa mm nataka adam anapuliziwa roho na iblis kuwa adui unipe hilo andiko sio unipe andiko baada ya adam kuumbwa
 
Naam ibilis

Mungu aliumba kila kitu lkn kwakuwa yeye ndio muumbaji basi huwezi sema ana sifa mbaya

Yeye anajinasibisha na sifa sifa nzuri nzuri kabisa
Jibu jepesi ni kuwa allah anaumba vitu anavyovipenda na asivyovipenda pia, ameumba mema hali ya kuwa anayapenda na ameumba maovu hali ya kuwa anayachukia na amemuumba ibliys, firauni, qaarun, haaman na umayyah ibn khalaf na wenzie na hali ya kuwa anawachukia.

Haulizwi kwa anayoyafanya kwani yeye hafanyi kitu kwa upuuzi bali anafanya mambo yake kwa hekima iliyotakasika kabisa, سبحانه و تعالى عمّا يقولون علوّا كبيرا
 
Hili andiko lilikuja uadui wa iblis na mwanadamu pale alipoambiwa amsijidie na hapo adam yupo na hawa mm nataka adam anapuliziwa roho na iblis kuwa adui unipe hilo andiko sio unipe andiko baada ya adam kuumbwa
Wakati malaika wanamwambia allah atamuumba mwanadamu atamwaga damu na kufanya ufisadi katika ardhi yeye aliwajibu mimi ninayajua yale msiyoyajua, wanawachuoni wametaja kuwa ni kuwa mnaye nyie kati yenu mwenye kiburi na muovu mno na hamumjui mpaka pale alipodhihirisha kiburi chake wakati amepewa amri ya kusujudu naye ni Iblis Bin Shetan na wala kutokudhihiri uovu wake kabla aadam hajaumbwa hakubadilishi kitu.
 
kumbe wanachuoni sio mungu kama wanchuoni hamna kitu hao sio ndio leo wanabishana na kutofautiana habari za mwezi mtume anasema usifunge siku ya iddi kuna waislam wanafunga kupitia hao wanchuoni hao wanchuoni ni fitna hawanaa wanachojua kila mtu anvuta kwake sunni anampinga shiya na ahmadiya anawapinga wote unaweza kuona wanachuoni hamna kitu kama quran haijasema iblis alimchukia adam wakat wakupuliziwa roho hayo maneno usiyatumie tena maana ukiyatumia nitakuuliza umeyatoa wapi
 
Mkuu hizi ni ngano na hekaya tu. Chanzo cha wanadamu wote siyo Adam. Kama adam alikuwa binadamu wa kwanza nipe sababu ya kwanini wengine ni weusi wengine weupe
Mwanadamu anapotumia akili yake kwenye mambo yaliyomzidi kimo, uzito na umri ndio matokeo yake haya.

Mkuu babu yako huwezi kumjua mpaka utambulishwe na wanaomfahamu hata kama una akili za namna gani, vilevile habari za kale huwezi kuzijua mpaka usome historia sahihi hata kama una akili kubwa kiasi gani, mwisho mtu wa nyuma ya ukuta wako huwezi kumjua mpaka utoke ukachungulie hata kama una akili za namna gani, sasa nakujibu.

"Enyi watu! hakika sisi tumewaumba kutokana na mwanaume mmoja na mwanamke mmoja, na tumekufanyeni kuwa ni mataifa na makabila mbalimbali ili mpate kujuana, hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu mbele za allah ni yule mchamungu zaidi kwenu, hakika allah ni mwenye elimu, mwenye khabari zote."

Qur'an 49:13
 
Usidhani umetoa hoja nzito, kwani quran ndio ushahidi pekee si kuna hadithi za mtume muhammad? haufahamu wewe kuwa ibliys alikuwa anamchezea aadam akimuingilia mdomoni na kutokea kwenye tupu yake ya nyuma wakati huo hajapuliziwa roho ameumbwa tu kwa udongo na ameachwa akiwa maiti?.

Sasa nakuuliza kwani kuna faida gani kujua alikuwa muovu kabla ya kupuliziwa roho aadam na baada yaani ndio nini, kuna faida gani?.
 
kama sababu ni hii basi shetani alionewa.
ushahidi unaonyesha sababu ya binaadm kuwa bora mbele za Mungu ni ya upendeleo zaidi wala sio ya uwezo na viwango.shetani kwa daraja alilokuwepo na uwezo alio nao inaonyesha wazi kumsujudia adam ilikuwa ni kumdhalilisha.

by the way,bible inasema shetani alifanya kiburi pia lakini si kumsujudia adam,bali kujaribu kujiinua hata mbele za Mungu baada ya kupewa nguvu kubwa,cheo na vipaji,akajiona anaweza akafanya jambo[emoji23],kilichompata kikawa kimempata,akafukuzwa na kuja kukaa duniani,lakini kwa hasira akatamka kwamba hakuna jambo jema la Mungu ataruhusu lifanyike mbele yake anaona.
 
Kwanza pole Sana mkuu Kwa huo mtihani

Hata nami nilitaka kurogwa Kwa kuwasaidia hao wakulungwa

Lakini

Tukiwahukumu wote tutakuwa tunakosea,naamini kuna wengine ambao sio wabaya kiasi Hicho

Ila

Uzoefu unaonyesha watu WA juu ndio huwa na viburi zaidi mkuu
 
Mkuu kama ulivyosema na kutoa mfano hapo huyu shwaini hajaonewa wewe mwenyewe umetoa mfano katika Biblia jinsi alivyo haribu

Anastahili kupita huku huyo.
 
Shukran kwa ukumbusho akhy, Allah akulipe kheri.

Mtume Swalla llahu allaihi wasallam- alipoulizwa ni nini kibri akasema:-
" Ni kuikataa haqi(kweli) na kuwadharau watu".

Tuzitakase nafsi zetu na maradhi haya ya moyo, yaliyokuwa mabaya kabisa, na Mwanadamu anatakabari kwa kipi hasa!

Allah subhaanahu wataa'la anasema:-

"Wala usitembee katika ardhi kwa maringo. Hakika wewe huwezi kuipasua ardhi wala kufikia urefu wa milima."(7:37).
 
Manesi wengi wa leba ni mawakala wa kuzimu ni maajenti, ndugu YAKO akiingia leba tafuta Mchungaji kabisa na mfunge Ili kukilinda kiumbe chake kisicho na hatia plus mama wa mtoto. Yaani huko hospital ndipo ibilisi amejaa, kila hospital ina mkuu wa pepo anaemiliki anga hilo. Hospital ni njiapanda ya kifo. Life and death.
Roho ya ukatili ya manesi wanapewa na boss wao shetani.
 
Swadakta Al akhy

Shukrani Kwa neno zuri toka Kwa mtukufu WA daraja
 
Dawa ya kiburi ni kaburi, thus waislamu na wakatoliki wanaagizwa kusafisha makaburi. Hii kitu uondoa roho ya kiburi na kujiona wewe si lolote.
Madhehebu mengine ukizika umezika hakuna kurudi nyuma
 
Swadakt mkuu

Umesema kweli kabisa watu ambao tungetarajia wawe faraja kwetu wamegeuka kuwa maibilisi wakubwa
 
Noma sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…