monde arabe
JF-Expert Member
- Oct 22, 2017
- 8,781
- 13,444
Noma sana!Asante Kwanza Kwa mchango wako
Unajua kama ulivyosema Malaika walionyesha wasi wasi juu ya kuumbwa Sisi kwasababu wakiangalia uzoefu kuna miamba ilimwaga damu Sana na mabalaa
Sasa
Mungu alitaka kuwaonyesha kuwa yeye anajua anachokiumba,ndo akamfundisha Adamu majina ya kila kitu halafu akawauliza malaika wataje lkn wakashindwa ndio Adam akataja
Kwahiyo ndio akawaambia wamsujudie Kwa heshima na kuwaonyesha kwamba huyo waliye dhani ni balaa kumbe yupo vizuri
Kosa la Ibilisi na kupinga amri ya Muumba wake kwasababu ya kiburi akaambiwa pita huku
Uzoefu huohuo unaonesha wanakua hivo kwa sababu ya mapito wanayopitia au visanga wanavyoviona vikitokea.Uzoefu unaonyesha watu WA juu ndio huwa na viburi zaidi mkuu
Unakuwa moto mkubwa zaidi yani nguvu inaongezekaMkuu hiyo bonge moja adhabu
Moto jumlisha Moto unapata nini hapo?
Noma sana!kama sababu ni hii basi shetani alionewa.
ushahidi unaonyesha sababu ya binaadm kuwa bora mbele za Mungu ni ya upendeleo zaidi wala sio ya uwezo na viwango.shetani kwa daraja alilokuwepo na uwezo alio nao inaonyesha wazi kumsujudia adam ilikuwa ni kumdhalilisha.
by the way,bible inasema shetani alifanya kiburi pia lakini si kumsujudia adam,bali kujaribu kujiinua hata mbele za Mungu baada ya kupewa nguvu kubwa,cheo na vipaji,akajiona anaweza akafanya jambo[emoji23],kilichompata kikawa kimempata,akafukuzwa na kuja kukaa duniani,lakini kwa hasira akatamka kwamba hakuna jambo jema la Mungu ataruhusu lifanyike mbele yake anaona.
AstaghfirullahIla mungu alikosea sana kusema adam amsujidie iblis maana adam kaombwa na udongo dhalili wakati iblis kaumbwa kwa moto na ukitoa jambo la iblis kukataa kumsujudia adam hana jambo baya alilowahi kufanya hapa duniani wakati huyo mwanadamu ana mabaya kila kukicha na baadhi umeyataja kwa makundi ya watu wanaofanya mabaya kunzia madokata wanausalama viongozi
Nakumbuka malaika walimwambia mungu usiumbe mtu binadamu kwakuwa atakuja kuleta fitna mauvo mabaya duniani ila malaika hawakuwahi kumwambia mungu usimuumbe iblis utakuja kuona iblis hana baya ila watu ndio wabaya ila ushauri wako mzuri saana kwa jamii
Kweli kabisa mkuu na yapo matukio mengi Sana kama hayo huwatokea watuJamaa alikuwa na demu wake Mzumbe lecture akawa anamtaka binti, binti kachomoa, lecture kafatilia jamaa ndio anaemiliki, lecture akajenga bifu na jamaa, kila jamaa akipambana anakula sapu tu anakamatwa, akamfuata lecture kulikoni shida nini mbona unanikamata hali nafanya vizuri, lecture akamwambia jamaa " hatma ya maisha yako ipo mikononi mwangu" lecture anamkomoa jamaa kisa yupo na binti amtakae.
Jamaa akaona isiwe tabu akaacha Mzumbe akaenda Muhimbili kusoma udaktari, akahitimu udaktari, miaka imepita zaidi ya 10 na kitu.
Siku moja akaambiwa zamu YAKO kuna mgonjwa ICU nenda kaokoe uhai wake jamaa akaenda chumbani, wakati akiendelea na matibabu akavuta kumbukumbu nyuma akaikumbuka hio sura akasema " huyu ni lecture yule alijifanyia ubaya kisa binti hatma ya maisha yake ipo mikononi mwangu" akamuomba MUNGU akapambana Sana hadi mgonjwa akakaa sawa akarejeshwa wodini, akiwa wodini akawa Akiendelea kumtibu hadi mgonjwa kumbukumbu zikarudi sawa, akiwa ni daktari wa mgonjwa. Kuna siku akamkumbusha mgonjwa ' nitazame vizuri unanikumbuka" Mwalimu hawezi mkukumbuka mwanafunzi, labda kupitia kisa au tukio. Akamkumbusha kisa cha binti na jinsi alivyomwambia chuoni " hatma ya maisha yako ipo mikononi mwangu" mgonjwa akakumbuka, daktari akamwambia sasa wewe hatma ya maisha YAKO ilikuwa mikononi mwangu ningeweza kulipa kisasi ningekudozi ufe lakini sikutaka kulipa ubaya. Mgonjwa akalia Sana na kuomba msamaha.
FUNZO maisha ni mzunguko usimtende ubaya mtu.
Asante studio. Kwa upande wangu nilivyosoma mada na maoni ya watu wengi humu, nimederive kwamba kiburi kinatokea kwenye fullness, completeness, satisfaction.
Mahali popote pale ukiwa juu yani ukiwa nafasi ya juu everywhere iwe kwa sifa za watu ama uwezo ama afya ama uchumi ama elimu ama kipaji..etc ni rahisi sana kupata kiburi. Hivyo independence ama kujiamini na kiburi kuna a very thin line.
Shetani alikataa kusujudu kwa sabbu alijiona tayari yuko level za juu. Wengi wetu kiburi tunakipata kutoka katika ile feeling ya independence. Nesi atakipata kwa sabbu anaona yeye kashazalisha wengi ama kuhudumia wengi na amepata mafanikio..wewe na shida zako leo unamletea afu yuko fresh kiafya, kiuchumi, kielimu, kiakili. Kama ana Roho wa Mungu sawa, lakin kama ndo leader wa kuzimu kashampa cheo chap tu lazima uipate pate. Hasa kama wewe ni level ya chini yake.
Similarly sehemu yoyote ile. Tunakuwa na kiburi kwa sabbu afya, akili, uchumi ,watoto, ndoa, familia ziko vizuri. So unaona ninyenyekee ili iweje?Niwe mpole ili nini labda? Nimsaidie kisa nini? Sisemi kwamba its always kiburi maana kuna muda tunahitaji mipaka baina yetu na watu lakini mipaka inapokuwa mikubwa hugeuka kuwa kiburi hasa kama unamuwekea muumba wako akupaye uzima mipaka na kutotaka kujishusha.
Na kiburi mara nyingi huondoka kwa kuserve wengine. Popote pale ukitaka uwe na mafanikio lakin usiwe na kiburi give out. Iwe ni muda wako, kipaji chako, sadaka, nguvu zako, kushiriki na wenzako katika mambo mbalimbali. Na zaidi ibada ya kweli kutoka moyoni. Itakusaidia sana kuweza kukishinda kiburi. Nimejaribu kuandika kwa mtazamo wangu, am open to more info..
"Similarly sehemu yoyote ile. Tunakuwa na kiburi kwa sabbu afya, akili, uchumi ,watoto, ndoa, familia ziko vizuri. So unaona ninyenyekee ili iweje?Niwe mpole ili nini labda? Nimsaidie kisa nini? Sisemi kwamba its always kiburi maana kuna muda tunahitaji mipaka baina yetu na watu lakini mipaka inapokuwa mikubwa hugeuka kuwa kiburi hasa kama unamuwekea muumba wako akupaye uzima mipaka na kutotaka kujishusha."
Asante Sana pamoja na mengi mazuri Sana uliyosema Mademoiselle nimependa niquote na hayo hapo.
Usiwe unanichoka mara nikutafutapo huwa napata mchango mzuri kutoka kwako.
Shukrani Sana.
Naaam ujumbe murua kabisa huu
Nilikuwa busy kiasi halafu usiwazungumzie wanachuoni wetu kama wanafunzi fulani wa day care, hao ni watu waheshimiwa na warithi wa mitume kwasababu mitume hawajarithisha dirham wala dinar bali wamerithisha elimu, na wapokezi wa hiyo elimu ni wanawachuoni wabobezi kwenye elimu hata allah جلّ و على akauunganisha ushahidi wake na wa malaika na wanawachuoni kuonesha hadhi yao na nafasi mbele zake.kumbe wanachuoni sio mungu kama wanchuoni hamna kitu hao sio ndio leo wanabishana na kutofautiana habari za mwezi mtume anasema usifunge siku ya iddi kuna waislam wanafunga kupitia hao wanchuoni hao wanchuoni ni fitna hawanaa wanachojua kila mtu anvuta kwake sunni anampinga shiya na ahmadiya anawapinga wote unaweza kuona wanachuoni hamna kitu kama quran haijasema iblis alimchukia adam wakat wakupuliziwa roho hayo maneno usiyatumie tena maana ukiyatumia nitakuuliza umeyatoa wapi
Hakuna nia kwenye kujiita jina baya namna hiyo sisi tumekatazwa kuitana majina mabaya kwenye quran.Ukisoma vizuri kitabu cha ARBAIN HADITHY NNAWAY kuna hadihi inasema mtume anasema INNAMAL AMALU BI NIYYAT hakika kila tendo kwa niya na mtu hunuiya anayofanya maana ni kwamba angalia nia ya mtu wengi wenu nyinyi waislam na wakristo ni majina tu matendo yenu zero wazinifu wao wasengenyi wao wezi wao wanafki wao sasa kuna tofauti gani kati ya iblis na waislam au wakristo wa sasa
Yeye ameumbwa kwa ndimi za moto, na aya nyingine imekuja kwa joto la moto lisilo na moshi linalounguza.Aliumbwa na moto alafu akapewa adhabu ya kwenda motoni kwake hiyo ni adhabu kweli?
Allah hana sifa mbaya, sifa zake zote ni za ukamilifu na ni nzuri na majina yake ni katika sifa zake.Mungu ana sifa zote uazozijua ziwe mbaya au nzuri
Sio kilichopo duniani bali yeye ameumba kila kitu ambacho sio yeye, kila kisichokuwa allah basi ni kilimwengu au kwa lugha nyingine kila kisichokuwa yeye basi kimeumbwa na yeye.Na je kila kilichopo duniani mungu aliumba yeye au matokeo ya fikra za watu
Ibliys hakuonewa bali alifanya kiburi cha hali ya juu mbele ya mola wake, malaika wabora na watukufu walikubali kumsujudia aadam yeye ni nani akatae wakati ni jini tu miongoni mwa majini? ukiwa na kiburi na husda umechukua sehemu katika tabia za ibliys na ukiwa mwepesi wa kuomba msamaha na maghfirah umechukua sehemu katika tabia za baba yako aadam alayhi ssalaam.kama sababu ni hii basi shetani alionewa.
ushahidi unaonyesha sababu ya binaadm kuwa bora mbele za Mungu ni ya upendeleo zaidi wala sio ya uwezo na viwango.shetani kwa daraja alilokuwepo na uwezo alio nao inaonyesha wazi kumsujudia adam ilikuwa ni kumdhalilisha.
by the way,bible inasema shetani alifanya kiburi pia lakini si kumsujudia adam,bali kujaribu kujiinua hata mbele za Mungu baada ya kupewa nguvu kubwa,cheo na vipaji,akajiona anaweza akafanya jambo[emoji23],kilichompata kikawa kimempata,akafukuzwa na kuja kukaa duniani,lakini kwa hasira akatamka kwamba hakuna jambo jema la Mungu ataruhusu lifanyike mbele yake anaona.
Mkuu kuna faida kutoka katika hadithi ya abuu hurayrah kwamba mtume swala na salaam ziwe juu yake amesema:Mkuu kama ulivyosema na kutoa mfano hapo huyu shwaini hajaonewa wewe mwenyewe umetoa mfano katika Biblia jinsi alivyo haribu
Anastahili kupita huku huyo.