Kwa unyenyekevu mkubwa, naombeni msaada wa mawazo kuhusu huyu binti

Kwa unyenyekevu mkubwa, naombeni msaada wa mawazo kuhusu huyu binti

Mimi binafsi simshauri kijana ambaye amejitunza, akashindana na matamanio ya nafsi huku akijenga maisha yake na amefikia hatua ya kuoa kwa maana ya uwezo wa kuyabeba majukumu.....na ni ndo yake ya kwanza....kuoa mwanamke ambaye ana mtoto......

Ndoa hasa ya kwanza ni ya kufurahia na kula raha za ndoa na sio kuhangaika na malezi moja kwa moja......lakini wanawake wenye watoto wao wanakuwa na ndimi mbili juu ya mahusiano Yao na wazazi wenza....ambapo Kwa mwanzo lazima ampake matope......

Kwa kweli mimi naona kuoa mwanamke mwenye unahitajika uwe na moyo mgumu wenye uwezo wa kuyavumilia hata yale yasiyo ya kawaida
Vipi kuhusu mwanamke asiye na mtoto akitaka kuolewa na mwanaume mwenye mtoto au watoto?
 
Vipi kuhusu mwanamke asiye na mtoto akitaka kuolewa na mwanaume mwenye mtoto au watoto?
Ni ngumu kupata amani ya moyo kwenye ndoa ambayo mwenzio tayari ana mtoto na mtu mwingine......

Ule muunganiko wa wazazi wawili waliochanganya damu na kuzaliwa kiumbe ni wa kudumu......hauvunjiki kwa matusi wanayotukanana wala meseji chafu wanazotumiana.......

Kuingia kwenye muunganiko wa ndoa na mtu wa namna hiyo ujue umejiingiza kwenye vita ambayo hautakaa ushinde maisha yako yote kwa maana hiyo NDOA baada ya kuwa ni ya watu wawili inakuwa ya watu watatu.......kitu ambacho kamwe moyo wako hautakaa uridhie.......
 
Habari wanaJf,
Kuna binti nipo nae kwenye mahusiano yakususua karibu mwaka wa pili huu. Huyu binti kipindi anasoma chuo kwa bahati/nzuri akapata ujauzito na kufanikiwa kupata mtoto. Mwanzo alikuwa anaogopa kuniambia kama ana mtoto ila akaja akaniambia ukweli.

Sasa kamaliza chuo anataka kuja kwangu na mimi Mungu kabariki nimefanikiwa kujenga nyumba yakuishi, mm sina shida sana na mtoto wake japo inavyoonekna mm ndio ninatakiwa kubeba majukumu kama shule n.k japo bado mdogo sana.
Kuhusu baba yake yupo mkoa mwingine na anavyodai huwa hahusiki sana na matumizi ya mtoto japo huwa anatoa kidogo.Shida inakuja majirani, ndugu na jamaa wanajua mm bado sina mtoto na mwimbo wa kila siku kuwa naoa lini!

Wakuu nimekuwa nasoma nyuzi za single mother kila mara humu ila hili lipo kwangu safari hii, naombe msaada kwa solve hilo suala[emoji1431][emoji1431]
Tumia akili sana kufanya maamuzi hapa kijana.... Ukikurupuka tu kwa ushawishi wa kichwa cha chini (mihemko ya kihisia) na moyo vikakushawishi bila kushirikisha akili yako yote utakuja kujuta baadae...
 
Ni ngumu kupata amani ya moyo kwenye ndoa ambayo mwenzio tayari ana mtoto na mtu mwingine......

Ule muunganiko wa wazazi wawili waliochanganya damu na kuzaliwa kiumbe ni wa kudumu......hauvunjiki kwa matusi wanayotukanana wala meseji chafu wanazotumiana.......

Kuingia kwenye muunganiko wa ndoa na mtu wa namna hiyo ujue umejiingiza kwenye vita ambayo hautakaa ushinde maisha yako yote kwa maana hiyo NDOA baada ya kuwa ni ya watu wawili inakuwa ya watu watatu.......kitu ambacho kamwe moyo wako hautakaa uridhie.......
Hapa ninakuelewa kabisa mkuu, nipo kwenye mahusiano ambayo mwanaume ana mtoto, yale mawasiliano yake na mama mtoto wake huwa yananikwaza sana
 
Hapa ninakuelewa kabisa mkuu, nipo kwenye mahusiano ambayo mwanaume ana mtoto, yale mawasiliano yake na mama mtoto wake huwa yananikwaza sana
Waungwana wanasema
Ukipanda gari na ukagundua haliendi unapokusudia kwenda basi fanya hima ushuke kituo kinachofuata.....kadri unavyochelewa kushuka na gari inavyosonga mbele ndio unavyozidi kuwa na mbali na kituo kikuu cha kuchukua basi sahihi la unapotaka kwenda.......na ndio gharama ya kurudi kituoni inazidi kuwa kubwa.........

Think big , take control of your destiny
 
Back
Top Bottom