Kwa unyenyekevu mkubwa, naombeni msaada wa mawazo kuhusu huyu binti

Vipi kuhusu mwanamke asiye na mtoto akitaka kuolewa na mwanaume mwenye mtoto au watoto?
 
Vipi kuhusu mwanamke asiye na mtoto akitaka kuolewa na mwanaume mwenye mtoto au watoto?
Ni ngumu kupata amani ya moyo kwenye ndoa ambayo mwenzio tayari ana mtoto na mtu mwingine......

Ule muunganiko wa wazazi wawili waliochanganya damu na kuzaliwa kiumbe ni wa kudumu......hauvunjiki kwa matusi wanayotukanana wala meseji chafu wanazotumiana.......

Kuingia kwenye muunganiko wa ndoa na mtu wa namna hiyo ujue umejiingiza kwenye vita ambayo hautakaa ushinde maisha yako yote kwa maana hiyo NDOA baada ya kuwa ni ya watu wawili inakuwa ya watu watatu.......kitu ambacho kamwe moyo wako hautakaa uridhie.......
 
Tumia akili sana kufanya maamuzi hapa kijana.... Ukikurupuka tu kwa ushawishi wa kichwa cha chini (mihemko ya kihisia) na moyo vikakushawishi bila kushirikisha akili yako yote utakuja kujuta baadae...
 
Hapa ninakuelewa kabisa mkuu, nipo kwenye mahusiano ambayo mwanaume ana mtoto, yale mawasiliano yake na mama mtoto wake huwa yananikwaza sana
 
Hapa ninakuelewa kabisa mkuu, nipo kwenye mahusiano ambayo mwanaume ana mtoto, yale mawasiliano yake na mama mtoto wake huwa yananikwaza sana
Waungwana wanasema
Ukipanda gari na ukagundua haliendi unapokusudia kwenda basi fanya hima ushuke kituo kinachofuata.....kadri unavyochelewa kushuka na gari inavyosonga mbele ndio unavyozidi kuwa na mbali na kituo kikuu cha kuchukua basi sahihi la unapotaka kwenda.......na ndio gharama ya kurudi kituoni inazidi kuwa kubwa.........

Think big , take control of your destiny
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…