Kwa utendaji kazi uliotukuka wa Rais Samia naanza kuziona dalili za upinzani kutafuta visingizio vya kumkimbia na kumkwepa katika Uchaguzi Mkuu ujao

Mobutu Sesseko alikuwa na vyama zaidi ya 30 pale Zaire ambavyo vilikuwa ni mali zake na vikiwa kwenye payroll yake, kila uchaguzi alishinda kwa zaidi ya 90%.

Mabeberu wa Ulaya hawakumpigia kelele maana walizawadiwa kila wakitakacho kwenye ardhi ya Zaire kwa mpumbavu mmoja Mobutu na circle yake wafurahie maisha, walifurahia kweli na kulewa sana.
Haya yote aliyafanya Mobuto akiwa amewaweka rehani ndugu zake weusi wa Zaire.
Leo hii Mobutu hayupo ameshaoza huko ardhini tena amekufa kifala kabisa na kuzikwa Moroco alikotibiwa maana alivyokuwa mjinga alishindwa hata kujenga hospitali na madaktari wanaoweza kumtibu akiumwa huko Zaire.
Mobutu amewaacha ndugu zake waZaire masikini na kwenye hali kubwa ya sintofahamu kwa sababu ya ujinga wake.

Waatanzania wengi ni masikini sana na umasikini wao kwa kiasi kikubwa chanzo chake ni maamuzi mabovu mabovu ya wanasiasa, Leo hii huwezi kusema eti hakuna mshindani ilihali Taifa limejaa watu masikini kila kona, Taifa vijana kwa mamilioni hawana ajira, Taifa hospitalini hakuna madawa na watu wanakufa kwa magonjwa yakipumbavu kabisa, Taifa watu hawalipwi mafao yao, Taifa hata mfuko wa bima ya Taifa tumeshindwa kuuendesha (NHIF), Taifa ambalo mifumo imejaa wezi wa mali za umma, Taifa ambalo matumizi ya serikali ni makubwa huku watu masikini, Taifa ambalo wahitimu mavyuoni wameathiriwa na mfumo mbovu wa elimu, Taifa ambalo kodi na tozo ni mzigo kwa mwananchi. nk nk,
 
Ndugu zangu hivyo ndivyo hali halisi ilivyo, kwasasa upinzani umefika hatua hauelewi ushike lipi na uache lipi, uongee nini na usimame na lipi, ubebe lipi na uache lipi, utembee na lipi na usimame na lipi.

Imefika hatua hata kuaminiana wao kwa wao wameacha, maana kila mtu anahisi mwenzie anadalili za kusaliti chama na kwenda kumuunga mkono Mh. Rais wetu mpendwa, hapa unaweza kurejea habari za Mch. Peter Msigwa namna alivyo tukanwa na vitoto vidogo kiumri kisa tu kusimamia mtizamo wake katika kuiunga mkono serikali juu ya suala la Loliondo.

Ndugu zangu kwa sasa hata wenyewe hawaoni wakuweza kushindana na Mh. Rais Samia maana kila waliyemuona awali kuwa ndio kamanda wa kuongoza mapambano, wanakuta amerudi mstari wa nyuma akiunga juhudi za Mh. Rais na hata kama ni kukosoa anakosoa kwa kushauri baadhi ya maeneo kwa heshima na staha, jambo linalozidi kuwa changanya na kuwalaza na viatu vijana wa upinzani.

Hii yote ni kwa kuwa Mh. Rais kafanikiwa kugusa kila eneo kiutendaji, watanzania wana matumaini makubwa sana na Mh. Rais kwa kuwa wanaona juhudi zake katika kujenga nchi yetu, wanaona namna kila mtu, kila kundi na kila eneo linavyoguswa kiutendaji. Hakuna anayeachwa nyuma wala kutengwa au kubaguliwa, wote wanapata huduma sawa.

Kila mtu anapata huduma sawa,kila mtu anasikilizwa, kila mtu anathaminiwa,kila mtu anaona anayo nafasi ya kuchangia ujenzi wa Taifa hili na kila mtu anaona anaweza kutimiza Ndoto na malengo yake katika nchi hii kwa kuwa fursa zipo wazi kwa kila mtu mwenye kuzitaka.

Sasa hapa ndioo mtihani mkubwa walionao upinzani kwa sasa katika kuweza kusimamisha mgombea kiti cha Urais maana hawaelewi watamsimamisha nani? Kwa sera na ajenda zipi, hawaelewi watawashawishi kipi watanzania, maana Mh. Rais amefanya kazi zilizogusa maisha ya watanzania hasa wanyonge wasio na sauti.

Wameona namna Mh. Rais alivyo shapu kuchukua hatua katika kumsaidia mwananchi pale panapojitokeza tatizo la kidhalula kama alivyo fanya kutoa Ruzuku katika kilimo na nishati ya mafuta, kiukweli kasi hii ya Mh. Rais imewaweka pabaya sana kisiasa.

Ushauri wangu kwao ,kwa kuwa wameonyesha kukubali utendaji kazi wa mh Rais Basi hawana budi Kuendelea kumuunga mkono Mh. Rais wetu, waendelee kutoa ushauri watakapoona panafaa kwa lugha ya heshima na staha.

Maana mama ni msikivu na mnyenyekevu anayemjali na kumsikiliza kila mtu, kwa sasa mama amekaa katika mioyo ya watanzania. Watanzania walitaka maendeleo na mtumishi mnyenyekevu atakayewasikiliza, sasa amepatikana Mh. Rais Samia anatekeleza kwa vitendo ndoto za watanzania.

Kazi iendeleee.
Kazi iendelee ya kusifu sifu na kumpamba mtu hata kama hafai,ccm bonge la machizi.
 
Haikuchaguliwa bali ilipitishwa na dikteta Magufuri akishirikiana na Mahera pamoja na Ndugai.
Wewe wasema hayo lakini wananchi ndio walio toa Ridhaa kwa CCM kuwatumikia, Ndio maana unaona namna wanavyoendelea kuiamini CCM
 
I think you need some mental checkup,

Honest sikuji lkn I think your has some mental illness
Nakwambia hivi upinzani kwa Sasa hauna Sera Wala ajenda za kwenda kuwashawishi watanzania, Sasa hivi wapinzani wachachee wamebaki kudandia vimatukio vipitavyo Kama ukungu
 
Ukiona mgonjwa mahututi ICU, ameamka, akaomba chakula, mkapiga stori vizuri, jua ya kuwa ANAAGA!!!!

CCM Ipo ktk hatua za mwisho za uhai wake.

KANU ktk hatua za mwisho za uhai wake walitamka kuwa Wana miaka 100 mbele ya kutawala, mwaka uliofuata kikafa.

Tusubiri.
Ccm siyo kanu ,CCM Ina misingi yake ambayo hakuna awezaye kuitikisa hapa nchini, hayupo na hatakuwepo
 
Kazi iendelee ya kusifu sifu na kumpamba mtu hata kama hafai,ccm bonge la machizi.
CCM Ni chama kilichobeba matumaini ya watanzania, Ni chama kiongozi, Ni chama chenye Sera na ajenda zinazogusa maisha ya watanzania, ndio maana mtu akifika ofisi ya CCM anakuwa na Imani ya kupata suluhisho la kero yake
 
Nakwambia hivi upinzani kwa Sasa hauna Sera Wala ajenda za kwenda kuwashawishi watanzania, Sasa hivi wapinzani wachachee wamebaki kudandia vimatukio vipitavyo Kama ukungu
Bwana Mwashambwa uteuzi tuu ndio unakufanya unaandishi vyote hivi.

Ivi uoni hata hii double taxation inayozumbua watu ase .
Kodi unalipa PAYE anakuja mtu anakata tena hata hiyo kidogo ulichobakisha
 
Kazi uliyotumwa unaifanya vizuri manake huangalii hoja zaidi ya kukomaa na ulichotumwa, inasound good
 
Back
Top Bottom