Kwa vichwa vilivyopo Wizara ya Fedha sasa, Tanzania itakuwa mbali sana kiuchumi kufikia 2030

Kwa vichwa vilivyopo Wizara ya Fedha sasa, Tanzania itakuwa mbali sana kiuchumi kufikia 2030

Viwanda vipo na vinaendelea kujengwa ila sio vya kutosha..

Lite ungejua sekta ya manufacturing inavyobeba uchumi Kwa Sasa hata usingeongea
Hapana , hatumanufacture dhahabu Wala minerals yoyote utasemaje inajenga uchumi?
Kama ingekuwa inajenga uchumi, tungekuwa na tax cuts mpaka sasa ila hakuna tax cuts na Kodi inaongezeka.
 
Angalia tunachoexport manufacturing goods compared kama tungekuwa tunaexport manufactured gold na raw minerals zingine.
Tungekuwa mbali mno
 

Attachments

  • Screenshot_20230326-214739.jpg
    Screenshot_20230326-214739.jpg
    22.2 KB · Views: 4
Duh tatizo ni mifumo mibovu tu ndio maana tunawaona wako poa ila kwangu siafiki kabisa kama wako juu kwa uelewa wa uchumi
Tatizo hatufanyi utafiti kwa wataalam wetu na shida kubwa kulamba asali itatucost sana, kila kitu kusifia hata pasipo na mpango
 
Nimefanya utafiti kidogo juu ya habari mbalimbali zinazoandikwa juu ya Tanzania kiuchumi kwa kipindi cha miezi 3 sasa. Kusema kweli hakuna habari mbaya utakayoikuta juu ya Tanzania kiuchumi. Wachambuzi wote wa nje na ndani ya Afrika wanaisema vizuri sana Tanzania. Sio kwenye uwekezaji sio kwenye ukuaji wa uchumi.

Nikaja eneo la pili kujiuliza kwa nini haya yanatokea sasa? Nimekuja kugundua pale Wizara ya Fedha, Rais kaweka watu makini sana ambao kwa maoni yangu bila shaka hawa ndo wanasababisha haya yote yatokee

Rished Bade, Lawrence Mafuru na sasa Nehemia Mchechu watakuja vikwa nishani kama sio 2029 basi 2030.

Wanafanya Mwigulu Nchemba aonekane Waziri wa Fedha mahiri sana kwa Afrika Mashariki na kati kwa sasa.

Walioshauri hawa financial gurus wawekwe kwenye mfumo wa serikali wa uchumi wanastahili pongezi sana.

Kwa hali hii, kuna kila sababu ya kusema Samia anaweza kuja kuwa Rais bora kabisa kuwahi kutokea Tanzania. Hali ya kiuchumi ya nchi inaenda vizuri sana kwa kweli!
Kuna pale TIC pia, kuna vichwa pale
 
Naunga mkono hoja
P
Hapo Kakaangu Paschal Mayala nitakupinga. Bila nchi kujitosheleza kwa chakula kwanza, hakuna maendeleo. Leo hii wananchi wako site huku wanalia hawana uwezo wa kununua chakula maana chote kinaenda nje, maendeleo yanatoka wapi? Pili, bila nchi kutengeneza home purchasing power (ambayo siioni ikitengenezwa) hakuna kwenda popote ila tunaweza kujidanganya kuwa tunaenda.
 
Sure, ngoja tuone...ingawa nataman hao manguli mmoja angepewa kuongoza Shirika letu la ndege...ni kama hamna kichwa cha biashara pia pale...Mama apaangalie pale
ATCL pale kuna haja ya kuletwa Dr Ramadhan Dau au achukuliwe mmoja kutoka makampuni ya Simu yaliyopo hapa Tanzania
 
Hapo Kakaangu Paschal Mayala nitakupinga. Bila nchi kujitosheleza kwa chakula kwanza, hakuna maendeleo. Leo hii wananchi wako site huku wanalia hawana uwezo wa kununua chakula maana chote kinaenda nje, maendeleo yanatoka wapi? Pili, bila nchi kutengeneza home purchasing power (ambayo siioni ikitengenezwa) hakuna kwenda popote ila tunaweza kujidanganya kuwa tunaenda.
Kwani Tanzania Ina shida ya Chakula?
 
Back
Top Bottom