Danga lao matawi ya juu hawawezi danga Kwa wapiga debe au watu wa chini wewe na ulofa wako huwezi wapataHamisa Mobetto kasoma Kayumba kuanzia Msingi na sekondari kasoma shule ya kata.
Hao kina Paula wamesoma hizo English Mediums lakini wanadanga. Huna hoja mkuu
"connection" inamata sana sasa hv ,Ila amini kuwa future haitokuwa na dili sn, sababu utakuwa na connection ila position hamna ,itabaki unajuana na mkuu wa mkoa, waziri na mfanyabishara mkubwa but still itakuwa ngumu kupiga hatua itakayokidhi nafsi yakoUsitegemee mwanao asome senti kayumba afu aje awe na connection nzuri baadae ( hapa tunaangalia badae na sio sasa).
Kama una uwezo wa kufanya hivyo fanya maana sio kwaajili yako bali ni kwaajili yake, yaani kwaajili ya maisha yake ya badae.
umesoma alichoandika au umekurupushwa usingizini kuogopa watoto kuondolewa shule hizo!!!?Wenye Hela hawalalamiki na Wala hawahitaji mleta mada lofa awasemee
Ni kweli kabisa ndugu yangu, mimi binafsi sambamba na mtoto wangu kuanza darasa la kwanza nimenunua shamba na kupanda miti ya mbao.imefikia hatua sasa ubora wa elimu anayopewa mtoto unapimwa kwa yeye kuongea kiingereza fasaha akiwa na baba yake au mama yake wakiwa matembezi weekend.
maarifa na uelewa wa mambo sio kipaumbele.
ndio sababu akina matumbotumbo mmewaona wameanza kuwaandaa watoto wao kwenye stream za uongozi kupitia ccm chipukizi,miaka 10 ijayo haitakuwa tena unajua kiingereza kiasi gani tukupe kazi(hazitakuwepo).itakuwa umejifunza nini shuleni kuja kupambana na masumbwi ya maisha???
anayewekeza $$ kwenye elimu ya mwanaye,asisahau kumuandalia na walau kiwanja\biashara au shamba atakaloanzia.
Tafuta pesa ww acha ujingaUmeongea kwa hasira ila ndo ukweli wenyewe
Af wenye hela hawana muda wa kusoma soma huku jf ...... wapo busy sana aiseee ila hawa jamaa wakukurupuka sasa .... wanavimba sana....🤣🤣🤣🤣 wenye hela hawafoki
Mwanafalalsafa mmoja akishawahi Sema dalili za mkulima Maskini ukiifika msimu wa kilimo badala ya kulima anaongelea wengine ohh wanalimaje ohh wanatakiwa walime hivi wenzie wanalima na trekta yeye na jembe la mkono mwenye trekta anaendelea kuwa tajiri sababu akilima na trekta Hana muda wa kuongelea mlima Kwa jembe la mkono yeye kazi tukila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.
Haya bhana mkuu mm yangu ni hayoHakuna connection yoyote shule za English Medium mkuu Narudia tena hakuna.
Bora hata Kayumba atatengeneza network ya watu wengi.
Mtoto anatakiwa apate maarifa yatakayo mfanya atafutwe na watu.
Hongera Kwa kupanda miti lakini hiyo haitoshi sababu miti Ina ushindani sana zamani mti ndio Kila kitu Sasa hivi Kuna viti vya plastic meza za plastic nguzo za simenti ,kuezeka nyumba Kwa chuma nk na Kuna kampeni Dunia Nzima za watunza mazingira za kuzuia ukataji miti hovyo ulichofanya kuzuri Tena mno kama Hali itabaki hivi hivi bila kubadilika miaka hiyo ijayo utavuna pesa nyingi mno na mkakati mzuriNi kweli kabisa ndugu yangu, mimi binafsi sambamba na mtoto wangu kuanza darasa la kwanza nimenunua shamba na kupanda miti ya mbao.
Toka mwaka huu wa 2024 mpaka 2034 atakuwa amemaliza elimu ya pili kama sera mpya ya elimu itapita.
Hio miaka kumi ijayo kama nikijaliwa kuitunza vizuri hio miti natumaini kabisa itakuwa mwanzo wake mzuri kuanza maisha hata kama hatajaliwa kwenda elimu za juu.
Hapa Kama una hela peleka Norway,Sweden, Finland,uk and usa Kama unataka uhakika wa connection Mana namuona jamaa mmoja my Ethiopia Ana date na binti wa Obama Kama kweli ndicho utafutacho.Hajielwi ulofa na ubahiki mbaya sana
Mtoto anasoma na watoto wa viongozi wakubwa serikalini, bungeni na Mahakama na WA wa wanyabiashara wakubwa na wanasiasa wakubwa nk wanaoajiri na kutoa fursa
Baadaye ndio hao huanza kupiga yowe kuwa ohh sababu mtoto Hana connection
Future is uncertain and it's beyond our reach and you won't touch it. Kama Ni konekesheni Ni kujipendekeza na kuwasifia wengine ama kumfungia riziwani kamba za kiatu utapewa uwaziri ama ukuu wa wilaya,ukiwa na sura nzuri mbona u dc unaupata jamani ,kila mtu Ana perception yake ,yaaani we differ our thoughts, beliefs like how we differ our physical featuresJirani yangu alisoma Tanganyika international school,,,Ile shule husoma watoto ambao wazazi wao hutoka mataifa mbalimbali huja kufanyakazi Tz.Huyo jirani yangu Kwa Sasa ni dalali WA vyumba mjini.🤣
Jirani angu mwingine alisoma st Mary's school,,,Kwa Sasa ni mwinilisti haya makanisa ya mwendokasi.
Jirani WA tatu alisoma Uganda,,,,Kwa Sasa hajulikani anachofanya(Hana kazi)
Umasikini unakusumbua. Huwezi ukawa na hela afu mtoto umwache akasome huku amekaa chini Huo ni ubwegeAmini nakwambia, hapa duniani kuna watu ambao wanahitaji kitu kimoja tu. Nacho ni mtu wa kuwaambia " hakuna tatizo kabisa endapo utafanya hivyo " au " usiogope"
Miongoni mwa watu hao ni kundi la wazazi wanao struggle kuwalipia watoto wao ada kwenye shule za kulipia za kiingereza.
Watoto mpaka sasa hivi hawajapokelewa wamebaki nyumbani huku wenzao wapo shuleni wana furahia maisha ya utoto shuleni. Mzazi kichwa kinaelekea kupasuka kwa sababu ambazo kimsingi hazina kichwa wala miguu.
Amini nakwambai , it is very much okay kumhamishia mtoto wako kwenye shule ya Kayumba.
Hakuna tatizo lolote kama utafanya hivyo. Wengi wanafanya hivyo kwa wingi sasa hivi and it is very much okay.
Usi babaishwe na hoja dhaifu kwamba " Tunalipa pesa nyingi kwa sababu tunathamini future za watoto wetu" . Hakuna lolote kwa sababu👇
Kuna tofauti kubwa sana kati ya kununua kitu kwa bei ya juu VS kununua kitu chenye thamani ya juu.
Kununua kitu kwa bei ya juu = Kupigwa.
Wewe kununua kitu kwa bei ya juu haimaanishi kwamba kitu hicho kina thamani ya juu. Ila maana yake ni kwamba muuzaji amekushawishi wewe uamini kwamba kitu hicho bei yake ni ya juu. Wewe kulipa kwa bei ya juu tafsiri yake ni kwamba umeingia kwenye mfumo wa muuzaji wala haimaanishi kwamba kitu hicho kina thamani hiyo.
Unaponunua IPhone kwa sh. Milioni 3 haimaanishi kwamba thamani ya IPhone ni sh milioni 3 ila ina maanisha kwamba muuzaji amekushawishi uamini kwamba thamani ya I phone ni sh milioni 3.
Inawezekana gharama za uzalishaji kwa kila iPhone moja ikawa dola moja au hata chini ya hapo ila wewe unauziwa milioni 3. Na huo unaweza kuwa ndio ukweli wenyewe kwa sababu kwa mabepari , business is when you buy an item for 50 Cent and sell it for 2000 usd. Capitalism is all about minimizing the cost of production in order to maximize the profit. Capitalism is always characterized by unequal exchange.
Hata hayo mamilioni unayo lipa unapigwa tu mkuu ( bwege mtozeni) wala haimaanishi ndio thamani ya anachopewa mtoto wako shuleni.
So ushauri wangu kwako bado hujachelewa. Peleka mtoto wako Kayumba. Utakuja kunishukuru sana.
Mwambie abadilishe mtazamo wake. Mpe nyuzi zangu asome atawarudisha watoto wake Kayumba without a doubtKuna jamaa nimekutana nae ananiambia majukumu yamemuandama ada anadaiwa zaidi ya 3M kwa watoto watatu tena hapo bado haijaisha analipa kwa installment ili wapokelewe tu shulen
jamaa hadi anaogopa kurudi nyumbani