Kwa Wazazi ambao watoto wenu bado hawajapokelewa shule za English Mediums kwa sababu bado hamjalipa ada, pitieni hapa

Kwa Wazazi ambao watoto wenu bado hawajapokelewa shule za English Mediums kwa sababu bado hamjalipa ada, pitieni hapa

Hamisa Mobetto kasoma Kayumba kuanzia Msingi na sekondari kasoma shule ya kata.

Hao kina Paula wamesoma hizo English Mediums lakini wanadanga. Huna hoja mkuu
Danga lao matawi ya juu hawawezi danga Kwa wapiga debe au watu wa chini wewe na ulofa wako huwezi wapata
 
Usitegemee mwanao asome senti kayumba afu aje awe na connection nzuri baadae ( hapa tunaangalia badae na sio sasa).

Kama una uwezo wa kufanya hivyo fanya maana sio kwaajili yako bali ni kwaajili yake, yaani kwaajili ya maisha yake ya badae.
"connection" inamata sana sasa hv ,Ila amini kuwa future haitokuwa na dili sn, sababu utakuwa na connection ila position hamna ,itabaki unajuana na mkuu wa mkoa, waziri na mfanyabishara mkubwa but still itakuwa ngumu kupiga hatua itakayokidhi nafsi yako

La muhimu ni pesa unayotumia Kwa mtt kwajili ya Ada na kwenda tour, "Wekeza" , wapi? Kwenye ardhi na mifugo, sababu nowadays vyeti si ishu tena ila connection ni ishu , so kinachofata ni connection itakuwa si ishu tena but what you possess ....
 
imefikia hatua sasa ubora wa elimu anayopewa mtoto unapimwa kwa yeye kuongea kiingereza fasaha akiwa na baba yake au mama yake wakiwa matembezi weekend.

maarifa na uelewa wa mambo sio kipaumbele.

ndio sababu akina matumbotumbo mmewaona wameanza kuwaandaa watoto wao kwenye stream za uongozi kupitia ccm chipukizi,miaka 10 ijayo haitakuwa tena unajua kiingereza kiasi gani tukupe kazi(hazitakuwepo).itakuwa umejifunza nini shuleni kuja kupambana na masumbwi ya maisha???

anayewekeza $$ kwenye elimu ya mwanaye,asisahau kumuandalia na walau kiwanja\biashara au shamba atakaloanzia.
Ni kweli kabisa ndugu yangu, mimi binafsi sambamba na mtoto wangu kuanza darasa la kwanza nimenunua shamba na kupanda miti ya mbao.
Toka mwaka huu wa 2024 mpaka 2034 atakuwa amemaliza elimu ya pili kama sera mpya ya elimu itapita.

Hio miaka kumi ijayo kama nikijaliwa kuitunza vizuri hio miti natumaini kabisa itakuwa mwanzo wake mzuri kuanza maisha hata kama hatajaliwa kwenda elimu za juu.
 
kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.
Mwanafalalsafa mmoja akishawahi Sema dalili za mkulima Maskini ukiifika msimu wa kilimo badala ya kulima anaongelea wengine ohh wanalimaje ohh wanatakiwa walime hivi wenzie wanalima na trekta yeye na jembe la mkono mwenye trekta anaendelea kuwa tajiri sababu akilima na trekta Hana muda wa kuongelea mlima Kwa jembe la mkono yeye kazi tu


Ndiyo Haya mlima jembe la mkono mwisho wa siku lofa Hana Hela za kupeleka mtoto shule za bei kubwa anaanza kujitia Tena mshauri wa mwenye pesa asomeshe wapi.Apambane na Hali yake .Maisha ni kama shamba Kila mtu alime lake ahangaike na shamba lake
 
Hakuna connection yoyote shule za English Medium mkuu Narudia tena hakuna.


Bora hata Kayumba atatengeneza network ya watu wengi.

Mtoto anatakiwa apate maarifa yatakayo mfanya atafutwe na watu.
Haya bhana mkuu mm yangu ni hayo
 
Sawa ela ngumu ila ukweli usemwe
Ubora wa elimu ya msingi kati ya public na private ni tofauti kabisa!
Nna wadogo zangu wanasoma kayumba darasa la 2 na wengine wanasoma private darasa hilo la 2 ila ukiwauliza vitu wale wa kayumba ni kama hawajawahi kabisa kwenda shule yani hawaelewi
Imagine darasani mwalimu anapewa wanafunzi 100+ wakati private wakizidi sana class ni 30,huwezi kulinganisha hawa walimu 2 kwenye ufatiliaji wa wanafunzi!
Ni heri mtoto asome private elimu ya msingi then sekondari ndo umpeleke government as anakua kashapata msingi mzuri
Suala la kujiuliza kama huko public pazuri mbona hatuoni mtoto wa kiongozi yeyote akisoma ili tupate uhakika elimu huko ni bora?
 
Ni kweli kabisa ndugu yangu, mimi binafsi sambamba na mtoto wangu kuanza darasa la kwanza nimenunua shamba na kupanda miti ya mbao.
Toka mwaka huu wa 2024 mpaka 2034 atakuwa amemaliza elimu ya pili kama sera mpya ya elimu itapita.

Hio miaka kumi ijayo kama nikijaliwa kuitunza vizuri hio miti natumaini kabisa itakuwa mwanzo wake mzuri kuanza maisha hata kama hatajaliwa kwenda elimu za juu.
Hongera Kwa kupanda miti lakini hiyo haitoshi sababu miti Ina ushindani sana zamani mti ndio Kila kitu Sasa hivi Kuna viti vya plastic meza za plastic nguzo za simenti ,kuezeka nyumba Kwa chuma nk na Kuna kampeni Dunia Nzima za watunza mazingira za kuzuia ukataji miti hovyo ulichofanya kuzuri Tena mno kama Hali itabaki hivi hivi bila kubadilika miaka hiyo ijayo utavuna pesa nyingi mno na mkakati mzuri

Lakini Kuna msemo usiweke mayai yote kikapu kimoja kikianguka yanabomoka yote

Wekeza pia Kwa kusomesha shule nzuri kukikwama huku mtoto anaibukia kwingine
Otherwise nakupongeza lakini isiwe option pekee tafadhali
 
Jiulize kwanini viongozi wote nasisitiza viongozi wote HAWAPELEKI watoto wao SAINT KAYUMBA?

tuseme wao wanapesa nyingi?
Au tuseme HAWAZIAMINI SAINT KAYUMBA?
AU tuseme wanafuata mkumbo?

Kuna kitu hakiko sawa sehemu!. Kama ingekuwa sharti na 01 ili uweze kuwa KIONGOZI WA UMMA basi mtoto wako ASOME SAINT KAYUMBA . Naamini hizi shule zingebadilika na kila mmoja angeona fahari kupeleka mtoto huko.

Jitahidini wale wote wenye walau kiasi kidogo cha fedha komaeni mpaka kieleweke mtoto ajisikie KUTHAMINIWA na moyo wako uwe na AMANI.
 
Hajielwi ulofa na ubahiki mbaya sana
Mtoto anasoma na watoto wa viongozi wakubwa serikalini, bungeni na Mahakama na WA wa wanyabiashara wakubwa na wanasiasa wakubwa nk wanaoajiri na kutoa fursa

Baadaye ndio hao huanza kupiga yowe kuwa ohh sababu mtoto Hana connection
Hapa Kama una hela peleka Norway,Sweden, Finland,uk and usa Kama unataka uhakika wa connection Mana namuona jamaa mmoja my Ethiopia Ana date na binti wa Obama Kama kweli ndicho utafutacho.
Ila hapa hapa bongo sioni tofauti ishu kubwa unasukumwa na EGO yaani kununua sigara ya Bei mbaya hakukufanyi uwe tajiri Ni Ile low self esteem and low self image unadhani kuwa ukimiliki iPhone na wewe utakuwa matawi Ila uhalisia nafsi yako inakuambia.
Kuna mdau akasema labda Kama umempeleka ambazo anasoma na watt wa mabalozi wa nje za above $10k kwa mwaka hapo sawa Ila below sijui 17M tzs bado unapigwa.
So mwanao anaenda kutafuta elimu ama konekesheni,yaani Kama Ni konekesheni sio lazima ahangaike huko anaweza akawa mpambepambe na Kama ana sura nzuri mbona atapewa u dc, u rc ama unasemaje??



Kikubwa kila mtu afanye kulingana na uwezo wake Mana watu hatulingani uwezo na sio ukose Raha kutumia kibatani mbele ya mwenzako mwenye smartphone.
Mfano unaweza ukawa na chombo Cha usafiri wenzako Wana magari.


Kuteseka mtu anajitesa mwenyewe what I know to live a happy life is accepting reality,and not trying to control uncontrollable,
Don't do comparison with others since this will steal your happiness and inner peace,
Do what your you're capable of na sio kulazimisha uwezo nje ya your young modulus.
Pia tusipangiane maisha kila mtu huwa ana k yake ambayo humsimumua automatically bila ya kuambiwa ama kushawishiwa.
Accept differences hata ulaya wapo wanaopanga mstari kupokea hela ya chakula Cha msaada ama coupon.

We're living in our own mind and not in big houses and bungalows or in our luxury cars
 
Jirani yangu alisoma Tanganyika international school,,,Ile shule husoma watoto ambao wazazi wao hutoka mataifa mbalimbali huja kufanyakazi Tz.Huyo jirani yangu Kwa Sasa ni dalali WA vyumba mjini.🤣

Jirani angu mwingine alisoma st Mary's school,,,Kwa Sasa ni mwinilisti haya makanisa ya mwendokasi.

Jirani WA tatu alisoma Uganda,,,,Kwa Sasa hajulikani anachofanya(Hana kazi)
Future is uncertain and it's beyond our reach and you won't touch it. Kama Ni konekesheni Ni kujipendekeza na kuwasifia wengine ama kumfungia riziwani kamba za kiatu utapewa uwaziri ama ukuu wa wilaya,ukiwa na sura nzuri mbona u dc unaupata jamani ,kila mtu Ana perception yake ,yaaani we differ our thoughts, beliefs like how we differ our physical features
 
Amini nakwambia, hapa duniani kuna watu ambao wanahitaji kitu kimoja tu. Nacho ni mtu wa kuwaambia " hakuna tatizo kabisa endapo utafanya hivyo " au " usiogope"

Miongoni mwa watu hao ni kundi la wazazi wanao struggle kuwalipia watoto wao ada kwenye shule za kulipia za kiingereza.

Watoto mpaka sasa hivi hawajapokelewa wamebaki nyumbani huku wenzao wapo shuleni wana furahia maisha ya utoto shuleni. Mzazi kichwa kinaelekea kupasuka kwa sababu ambazo kimsingi hazina kichwa wala miguu.

Amini nakwambai , it is very much okay kumhamishia mtoto wako kwenye shule ya Kayumba.

Hakuna tatizo lolote kama utafanya hivyo. Wengi wanafanya hivyo kwa wingi sasa hivi and it is very much okay.

Usi babaishwe na hoja dhaifu kwamba " Tunalipa pesa nyingi kwa sababu tunathamini future za watoto wetu" . Hakuna lolote kwa sababu👇

Kuna tofauti kubwa sana kati ya kununua kitu kwa bei ya juu VS kununua kitu chenye thamani ya juu.


Kununua kitu kwa bei ya juu = Kupigwa.

Wewe kununua kitu kwa bei ya juu haimaanishi kwamba kitu hicho kina thamani ya juu. Ila maana yake ni kwamba muuzaji amekushawishi wewe uamini kwamba kitu hicho bei yake ni ya juu. Wewe kulipa kwa bei ya juu tafsiri yake ni kwamba umeingia kwenye mfumo wa muuzaji wala haimaanishi kwamba kitu hicho kina thamani hiyo.

Unaponunua IPhone kwa sh. Milioni 3 haimaanishi kwamba thamani ya IPhone ni sh milioni 3 ila ina maanisha kwamba muuzaji amekushawishi uamini kwamba thamani ya I phone ni sh milioni 3.

Inawezekana gharama za uzalishaji kwa kila iPhone moja ikawa dola moja au hata chini ya hapo ila wewe unauziwa milioni 3. Na huo unaweza kuwa ndio ukweli wenyewe kwa sababu kwa mabepari , business is when you buy an item for 50 Cent and sell it for 2000 usd. Capitalism is all about minimizing the cost of production in order to maximize the profit. Capitalism is always characterized by unequal exchange.

Hata hayo mamilioni unayo lipa unapigwa tu mkuu ( bwege mtozeni) wala haimaanishi ndio thamani ya anachopewa mtoto wako shuleni.

So ushauri wangu kwako bado hujachelewa. Peleka mtoto wako Kayumba. Utakuja kunishukuru sana.
Umasikini unakusumbua. Huwezi ukawa na hela afu mtoto umwache akasome huku amekaa chini Huo ni ubwege
 
Kuna jamaa nimekutana nae ananiambia majukumu yamemuandama ada anadaiwa zaidi ya 3M kwa watoto watatu tena hapo bado haijaisha analipa kwa installment ili wapokelewe tu shulen

jamaa hadi anaogopa kurudi nyumbani
Mwambie abadilishe mtazamo wake. Mpe nyuzi zangu asome atawarudisha watoto wake Kayumba without a doubt
 
Back
Top Bottom