Wakati tunasoma kijijini, majirani walikuwa wanamshauri mzee kwamba kwa nini anahangaika kusomesha watoto sekondari, kwa nini asituegemeze kwenye kilimo, mbona kinalipa? Mzee aliwajibu kuwa, alikuta babu yake analima, akamuona baba yake analima na ueye akaingia kulima, lakini haoni mabadiliko. So ameamua kusomesha watoto ili wajaribu kupata experience ya tofauti.
Nikirudi kwenye mada, wazazi tulio wengi tunesoma Kayumba. Tunajua raha na karaha zake, fursa na changamoto zake. Tunapojitutumua kuwapeleka huko English mediums, tunataka wapate experience, japo kidogo, tofauti na Kayumba.
Pili, kuchelewa kumlipia mtoto ada sio kushindwa. Ni suala la muda tu. Changamoto hazikimbiwi. Akisolve, mtoto akapokelewa shule, ndo kushinda changamoto huko.
Mwisho kabisa, dunia inabadilika. Msomeshe mtoto kulingana na mahitaji yake ya baadae, sio kwa mahitaji yako.