Kwahili la Mabasi kusafiri Usiku, nampongeza Mbunge Tulia Ackson

Kama tuna wasiwasi na vyombo vya ulinzi haviwezi kumlinda msafiri na mali yake na akafika salama safari yake basi hawafai kuwepo, tunaposafiri masaa 24 wajipange highway patrol, na vituo vya ukaguzi viwepo muda wote ili kudhibiti pia magendo na biashara haramu kufanyika kwa mwanza wa kusafiri usiku,
 
Hakika kabisa ndugu yangu
 
Kuna changamoto ya uendeshaji wa hovyo usiku hasa kwa malori.

Usiku malori yanatimua mbio kiasi kwamba wenye magari madogo wanaweza kusukumizwa mtaroni, imenikuta hii alafu jamaa hakusimama wala nini nashukuru Mungu nilinusurika ila gari iliharibika so nilikesha pale kuhangaikia matengenezo
 
Zambia, Botswana, zimbabwe, Swaziland, Namibia, Msumbiji, DRC , Angola, na Baba lao SA. Wewe bahati ushafika kote huko umevuruga hivi ukiona vyuma wanavyokokota barabarani unaweza kudhani sisi ndio hatuna bandari
Nawaona ndugu zangu kama tumerogwa hapo Botswana ukiliona Ford Ranger au Toyota GD harafu lipo kituo cha polisi dogo kalipaki akitoka anatambaa nalo home wewe hata upite na gari gani hashangai wala hata kukagua chochote ulichobeba ndani zaidi onyesha document utembee Tz sasa unalipia gari kodi kubwa harafu wanakuja kukuuliza hii Tv vip au rice cooker mpaka unawaambia Wazee tumerogwa nini mbona tuna Roho za kupenda vitu visiingie Tanzania?
 
Halafu hua kodi za Tanzania maajabu matupu Haiwezekani Rwanda simu iwe bei rahisi kuliko Tanzania yaani watu wanatoka Tanzania kwenda Rwanda kununua simu bei rahisi tena hawana habari ya fake hadi tunatia huruma
Simu Watanzania wanafata SA kwa sababu hawa jamaa kodi kwenye simu sio kubwa Bongo sasa kitu cha kawaida kodi kubwa kinapelekea watu wake kutumia vitu vya hovyo hovyo wakiamini ni bora kumbe hata hizo simu bora hazina bei hiyo ni vile Serikali haijali watu wake tupo busy tunahangaika na used ya Dubai,China na SA kumbe kukiwa na kodi rafiki maduka ya simu bora yataanzishwa nyumbani...
 
Unapopishana na lori usiku mwenye gari ndogo punguza sana mwendo na unatakiwa utanue bara bara hasa kwa wale wanaojihami kwa kuwasha hadi zile taa za juu...madereva wa malori hata mchana wanalala nimeona ajali ya Arusha exp hapo Dodoma bus lilifatwa upande wake..
 
watu watabinuka hapa waje walaumiwe ofisi ya majanaga ya waziri mkuu kwa kutotoa msaada haraka.

wenzenu wanaangalia biashara zao wanatoa mawazi haya.

wengine wanaangalia takwimu,kitaalamu wanaona ni heri usiku zisiwepo.
 
Halafu hua kodi za Tanzania maajabu matupu Haiwezekani Rwanda simu iwe bei rahisi kuliko Tanzania yaani watu wanatoka Tanzania kwenda Rwanda kununua simu bei rahisi tena hawana habari ya fake hadi tunatia huruma

Nishaenda Kigali mara 3 eeh banae hawana vitu copy hata mtumba wa kuvaa tu ni kuwango sema bei uki-convert faranga yao ni kubwa kuliko Tsh. Ila wapo smart mno cha ajabu ni gari aina ya noah ndo sijawahi iona huko!
 
Enzi zile Sirari Nairobi bus za Otange Nyamira na Akamba kutekwa ilikuwa kawaida sana tuliwahi tekwa tukaambiwa shuka uchi kila ulichonacho weka kwa mfuko kumbe bana watekaji wanagawana majukum wawili ndani na mitutu 1 nje mlangoni na mfuko mkubwa ukishuka tu unaweka kwenye mfuko kila ulicho nacho wengine wapo wawili ni maelekezo lala chini kichwa iangalie chini Eeh sitosahau hiyo siku jamaa ye hadi nguo kaweka kwa mfuko tumerudi ndani mwenzetu yupo uchi mama kampatia kanga mwingine kampa kitenge basi bana tumetoka pale kufika Bomet tunaenda kureport polisi polisi anasema geuza gari twende penye hiyo place wakora wamechukua hizo vitu nilishangaa sana turudi kufanya nn? [emoji16] Mwanangu acha tu kutwekwa kusikie na walet ndo ukawa mwisho wangu kuitumia hadi leo hii [emoji112]
 
Hongera Betina.
 
Kabla yayote, Magari yoteya Abiria na Malori yawekew speed lemit, kama wanavo fanya South Africa. Hapo sasa safari zausiku zinaweza ruhsiwa!
 
Ni wachawi tu ndio mambo yao ni usiku, nguvu zao ni za giza.

Safari za usiku ni safari za kutoana kafara kwa nchi yetu, bado tupo nyuma sana kwa safari za usiku.
Mawazo ya kijima kabisa haya, imagine sasa hivi unatoka Mpanda mpaka Dar barabara ni lami, unataka watu wasisafiri usiku? Halafu unataka uwe uchumi wa kati au uchumi wa juu?? Thubutuuu!!!
 
Tujiandae na kulia sana
Ajali nyingi mchana Usiku itakuwaje
Wakati wa kuwekewa mawe barabarani/Kitonga ni nyakati za Usiku
Watakaoteseka ni wamama wazee na watoto
Hii nchi inazidi kurudi nyuma…
Mawazo ya kimasikini sana haya, narudia miaka ya 80 kuja 90 ma Bus yalikuwa yanasafiri usiku, alfajiri unaingia Dar unafanya mishe zako weee ikifika saa 10 jioni uko Kisutu au pale Mnazi mmoja unachukua bus unarudi zako mkoani. Hii pia ilisaidia anayerudi mkoani akifika asubuhi kama anaenda wilayani anakuta usafiri anaunganisha. Huwezi kuwa na jamii iliyoendelea inayofanya kazi asubuhi mpaka saa 9 au saa 10 tuu, no way.
 
Watu wenye mawazo kama haya mimi huwaita vikwazo vya maendeleo. Badala ya kuruhusu bus zisafiri usiku ili kuona changamoto na kuzitatua, bado mna mawazo ya mzee Mwinyi ya miaka hiyoo wakati network ya barabara nchini yenye lami was maybe 30%... 60 yrs unawaza kusafiri usiku siyo salama?? Really??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…