Ni raia wa Marekani huyu. Si ajabu anaweza kuwa ni agent wao pia....
Marekani sasa inatishwa sana na uwepo wa China barani Afrika na inahaha mno kupata mahali pa kujishikiza ili kupindua meza japo kwa kuchelewa. Kutokana na mabadiliko ya kasi ya tabia nchi, kuna uwezekano mkubwa kwamba nafasi ya Afrika kama mzalishaji mkuu wa raslimali ghafi na hasa zinazohusu nishati safi na salama itazidi kuongezeka. Tanzania tuna Helium, gesi asili na Uraniamu ya kutosha. Kwa hivyo huyu mama ni mtu wa muhimu sana kwa Wamarekani si kwa Tanzania tu bali hata nchi jirani.
Nimemuona Kigogo anashangaa eti katoa wapi dola milioni 1.7 za kununua mjengo Maryland na kupeleka familia nzima visiwa vya Caribbean kutumbua kwa siku 10+. Dola milioni 2 kwa mtu kama huyu si vijisenti tu kama vya Chenge?
Hana shida huyu. Atarudi kukaa zake Maryland na kazi yake aliyokuwa amepewa si ajabu atakuwa keshaimaliza. Kama unabisha kamuulize hata Magufuli atakwambia....
View attachment 2376533