Kwanini benki hakuna vyoo/maliwato kwa ajili ya wateja?

Kwanini benki hakuna vyoo/maliwato kwa ajili ya wateja?

Swali zuri sana.

Pia wao wafanyakazi huwa wanatimiza haja zao wapi kama hizo sehemu za kutimizia haja hazipo?
Vyoo vya wafanyakazi lazima vitakuwepo ila kwa wateja nafikiri hadi uombe na unaweza hata kusachiwa na wanausalama ili wajiridhishe kuwa huwezi kuleta madhara.
 
Wafanyakazi kuna vyoo vyao mle ndani.

Vyoo vya wafanyakazi lazima vitakuwepo ila kwa wateja nafikiri hadi uombe na unaweza hata kusachiwa na wanausalama ili wajiridhishe kuwa huwezi kuleta madhara.
Kama wanahofia suala la usalama, ni bora waangalie namna ambayo wataweza kutoa huduma hiyo hata kwa kusachi kabla mtu hujaingia sehemu ya haja.

Vyoo ni muhimu sana kwa kuimarisha huduma za jamii.
 
Hata polisi hakuna vyoo vya sisi wananchi sijui kwa nini !!![emoji41]
 
Ukitaka kujutia kubanwa na haja maishani omba ufunguo wa choo cha mahakama.
 
Ivi na wale walinzi wanaokaaga nje nao huwa wanajisaidiaga wapi
 
Vyoo vipo sana kama unahitaji uliza wale askari utaonyeshwa.
 
Wewe Bank umeenda kupata huduma ya choo au kutoa na kuweka hela..!??? Na vilee Bank zipo Mjini watuu watakua wanaend tu kujisaidia hata kama hawahitaji huduma za Kibank... na vitakua Vichafu sanaaaa yani sanaa...maana watu ustaarabu zerooo
 
Back
Top Bottom