Hellow!
Wadau kama inavyosomeka hapo juu,
Kwanza ifahamike kwamba biashara ya bank ni biashara inayotolewa leseni yake na BOT kutoa huduma zake kwa umma kama zilivyo biashara nyinginezo
Kwa kua biashara hii inahusisha huduma za kuvuta subra kwa muda mrefu pamoja na foleni za hapa na pale,
kwa mfano nipo bank fulani ya hapa jijini Dar es salaam toka saa 8 mpaka saa kumi huduma bado haijakamilika nilikua nimebanwa na mkojo nachezesha miguu mpaka nahisi kushtukiwa ila naambiwa kupata huduma za choo (vya kulipia) ni kilomita 2 hadi 3 kutoka mahali nilipo
Nimejaribu kuulizia kama vipo vyoo vya staff ili nizame tu hivyo hivyo ila wazee wamenibania kabisa hata baada ya kuona hali yangu
Ili kuulinda utu na afya yangu niliamua kuzunguka nyuma ya jengo la bank nikaachia vyombo kumbe security wameniona
Pamoja na kwamba tulizozana kwa muda mfupi ila nashukuru sasa najiona mwepesiiii
Nitoe rai kwa wizara ya fedha kupitia benki kuu watoe wito kwa mabenk yote nchini kuwajali wateja wake kwa kuwaletea karibu huduma hii muhimu (ya vyoo) hasa ukizingatia kwamba huduma za kibenk ni mchakato wenye kuchukua muda mrefu kibongobongo
Nawasilisha....