Kwanini benki hakuna vyoo/maliwato kwa ajili ya wateja?

Kwanini benki hakuna vyoo/maliwato kwa ajili ya wateja?

Banki ni sehem ambayo hutakiwi kukaa muda mrefu... ikizidi sana ni dakika tano sasa hiyo haja anaitoa wapi ndani ya dakika tano? ukikaa sana pia si vizuri kiulinzi.
Mkuu bank ya wapi hiyo ya kukaa dk5 ukapata huduma ukaondoka?

Branches nyingi ni msoto kuanzia kwenye huduma za Atm hadi humo ndani balaa la kuunga bogi.

Benki ya wapi ya huduma fasta nama hiyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Banki ni sehem ambayo hutakiwi kukaa muda mrefu... ikizidi sana ni dakika tano sasa hiyo haja anaitoa wapi ndani ya dakika tano? ukikaa sana pia si vizuri kiulinzi.
Mkuu acha utani basi,miaka ya2008,2009 nikiwa nafanya biashara zangu wilayani Kahama,nilikuwa nikienda benki naweza kaa foleni kwa dakika 40 hadi saa nzima hasa tarehe za mishahara,harafu wewe unasema dk 5?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa alivyotaja Huduma hizo nimeelewa kua inatumiwa na wenye hela, sasa swali ni kuanzia shilingi ngapi? faida na hasara za kutumia account hizo
hapo sawa, nadhani atakuja kukueleza kwa ufasaha
 
Hapo mbagala nilisha ahirisha huduma sababu ya ubabe wa walinzi, nilikua nasoma account numbers kutoka kwenye simu jamaa linaniambia huruhusiwi kutumia simu tukabishana sana ikabidi tu nisepe kwa maudhi yao. Ile bank yenye rangi za chama pendwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Walinzi wanazingua sana, ma branch manager wangelijua hili wasingewaruhusu kabisa, tunakeleka saaana
 
Ni kweli kabisa nilishawahi kukutana na tatizo hilo Bank mbona nilikatisha huduma !! Hivi ni kwanini hawana vyoo ??

Sent using Jamii Forums mobile app
inabidi tuwe tunamaliza haja zetu kwanza majumbani ndio tunaenda maana hakuna namna, tunaenda kama wateja ila tukifika tunahisiwa vibaya nakugeuka wezi watarajiwa
 
Vyoo vipo kwenye kila jengo
Shida watz wakijisikiaga haja huwa wanaona noma kuuliza!

Ova
 
Banki ni sehem ambayo hutakiwi kukaa muda mrefu... ikizidi sana ni dakika tano sasa hiyo haja anaitoa wapi ndani ya dakika tano? ukikaa sana pia si vizuri kiulinzi.
Kama una tumbo la kuharisha je? Watoa huduma wa bank wapo taratibu kuliko unavyo dhani

Choo kina umuhimu wake sehemu yoyote pale.
 
Hellow!

Wadau kama inavyosomeka hapo juu,

Kwanza ifahamike kwamba biashara ya bank ni biashara inayotolewa leseni yake na BOT kutoa huduma zake kwa umma kama zilivyo biashara nyinginezo

Kwa kua biashara hii inahusisha huduma za kuvuta subra kwa muda mrefu pamoja na foleni za hapa na pale,

kwa mfano nipo bank fulani ya hapa jijini Dar es salaam toka saa 8 mpaka saa kumi huduma bado haijakamilika nilikua nimebanwa na mkojo nachezesha miguu mpaka nahisi kushtukiwa ila naambiwa kupata huduma za choo (vya kulipia) ni kilomita 2 hadi 3 kutoka mahali nilipo

Nimejaribu kuulizia kama vipo vyoo vya staff ili nizame tu hivyo hivyo ila wazee wamenibania kabisa hata baada ya kuona hali yangu

Ili kuulinda utu na afya yangu niliamua kuzunguka nyuma ya jengo la bank nikaachia vyombo kumbe security wameniona

Pamoja na kwamba tulizozana kwa muda mfupi ila nashukuru sasa najiona mwepesiiii

Nitoe rai kwa wizara ya fedha kupitia benki kuu watoe wito kwa mabenk yote nchini kuwajali wateja wake kwa kuwaletea karibu huduma hii muhimu (ya vyoo) hasa ukizingatia kwamba huduma za kibenk ni mchakato wenye kuchukua muda mrefu kibongobongo

Nawasilisha....
 
FURSA HIYO KWA WAFANYA BIASHARA MAANA BENKI SIO RAHISI KIHIIVYOO
 
Back
Top Bottom