Kwanini China nchi ya kidikteta ina maendeleo makubwa kuliko Kenya na Zambia?

Kwanini China nchi ya kidikteta ina maendeleo makubwa kuliko Kenya na Zambia?

Umesah

umesahau pointi moja muhimu sana. Uchumi wa Afrika unasimamiwa na mabepari. Nchi ikienda speed kimaendeleo, itapigwa tukio ili kuipunguza kasi.

Hii ndiyo sababu kubwa ya umaskini wa nchi zetu.
Uchumi wa Africa hausimamiwi na mabepari, hizo ni conspiracies tu.
Makampuni makubwa kama ya madini yanavyotenda Africa ndivyo yanavyotenda kote duniani yakipata hiyo nafasi. Tofauti ni kwamba nchi nyingine wana taasisi imara za kudhibiti mambo kama ukwepaji kodi.

Hakuna nchi ya mabepari inayolazimisha kununua V8 kwa viongozi wenu huku mkishindwa kuwapa watu huduma muhimu za miondombinu n.k, hakuna nchi ya mabepari inayowalazimisha kuwa na sera mbovu zinazozuia ukuaji wa mitaji na biashara kwa raia wenu, hakuna nchi za mabepari zinazowalazimisha muibiane kura na kuharibu uchaguzi,
 
Hakuna mahusiano yeyote kati ya maendeleo ya nchi husika na mfumo wake unao iongoza.
Na ndo maana kuna nchi zinazo ongozwa kidemokirasia ni tajiri na kuna nyingine zina uchumi wa kati na kuna nyingine ni masikini kabisa,na upande wa nchi zinazo itwa za kidkiteta ni vilevile.
Kuna mahusiano makubwa kati ya maendeleo na mfumo wa uongozi wa nchi. Kuna aina ya udikteta unakwamisha au unaharibu maendeleo, Demokrasia ni nadra kukwamisha maendeleo hata kama sio perfect kwa sababu kuna fursa ya kujikosoa na kujisahihisha kupitia mijadala na mawazo huru.
 
Kupitia Demokrasia kama nchi ina wajinga wengi wanaweza kumchagua mwendawazimu kwa uchaguzi huru na wa haki kabisa, zinaweza kupitishwa sheria za hovyo na wabunge waliochaguliwa kupitia Demokrasia.
Na hapo ndipo huwa inakuwa...

Always majority ya watu huwa sio intelligent, wajinga ni wengi kuliko wenye akili hata darasani tu, level ya mkoa hadi nchi... Na serikali zinajua kucheza na akili za wajinga wengi..
 
Kuna mahusiano makubwa kati ya maendeleo na mfumo wa uongozi wa nchi. Kuna aina ya udikteta unakwamisha au unaharibu maendeleo, Demokrasia ni nadra kukwamisha maendeleo hata kama sio perfect kwa sababu kuna fursa ya kujikosoa na kujisahihisha kupitia mijadala na mawazo huru.
Demokrasia haifanyi kazi perfectly kama nchi ina tatizo la elimu duni na rushwa. Yani cancer ya RUSHWA ndio mbaya mno na ikishaingilia mfumo hapo Demokrasia inabakia mdomoni tu. Thats a typical case of Tanzagiza.

Ili ufanisi wa demokrasia uwepo by 100% nchi inatakiwa iwe imenyooka kibunge, kimahakama na kiserikali. Sasa kama kuna kundi la raia wao sheria na adhabu haziwahusu halafu wengine a slight misconduct wanaozea jela huoni kuna shida hapo. Hata ukija upande wa fursa the same pattern goes on.
 
Hakuna mahusiano yeyote kati ya maendeleo ya nchi husika na mfumo wake unao iongoza.
Na ndo maana kuna nchi zinazo ongozwa kidemokirasia ni tajiri na kuna nyingine zina uchumi wa kati na kuna nyingine ni masikini kabisa,na upande wa nchi zinazo itwa za kidkiteta ni vilevile.

Taifa lolote linapata maendeleo kwa sababu ya uwajibikaji wa viongozi na jamii ya watu wa nchi hiyo,sasa huku Africa kuanzia viongozi mpaka kwa raia uwajibikaji ni zero.

Ukitaka kujua kuwa waafrica ni jamii ya hovyo ww nenda vyuoni ambavyo ndo vinategemewa kuzalisha viongozi na watumishi wa uma uone mambo yanayo fanyika.
Yaani tunataka tuzalishe viongozi bora kutoka kwenye jamii iliyo oza.
Uozo unaanzia juu😁! Iko hivyo duniani kote...Huwezi kuongoza watu ukataka wawe wasafi ikiwa wewe ni mchafu tayari.
 
Miluzi mingi humpoteza mbwa,kwenye demokrasia watu wanapata muda wa kukosoa kila kitu! Kuna kijiji nilikulia miaka ya tisini kile kijiji kilikuwa kisafi Sana wanakijiji waliishi Kwa ushirikiano Sana,barabara walitengeneza wenyewe Kwa kujitolea,hapo ndio Kiongozi alipatikana Kwa kuangalia mtu anayejitoa Sana kwenye KAZI za kijamii! Ulikuwa kuiangalia mtaa unaweza ona mbele hata kilometer 5 usione hata karatasi! Badae nikaenda baada ya miaka 15 dooh salala! Kijiji kichqfu balaa madiwani wanasema tunashindwa kuwafosi watu kwenye KAZI za maendeleo watakunyima kura
Utamfosi vipi mtu ambaye humlishi😂??? Serikali haiwajali zaidi ya kuwagonga tozo huo muda wa kusimamia vijiji utatoka wapi?
 
"Popote umwonapo mtu mweusi ujue Kuna tatizo,kwa sababu mtu mweusi mwenyewe ni tatizo"P.W.Botha

China ni taifa la tofauti sana na mataifa ya Afrika,katika nyanja zote za kimaisha.Serikali ya China haicheki na watu wazembe hata kidogo na inawalipa mishahara na posho.
 
Attachments

  • 20241031_101347.jpg
    20241031_101347.jpg
    117.5 KB · Views: 1
Miluzi mingi humpoteza mbwa,kwenye demokrasia watu wanapata muda wa kukosoa kila kitu! Kuna kijiji nilikulia miaka ya tisini kile kijiji kilikuwa kisafi Sana wanakijiji waliishi Kwa ushirikiano Sana,barabara walitengeneza wenyewe Kwa kujitolea,hapo ndio Kiongozi alipatikana Kwa kuangalia mtu anayejitoa Sana kwenye KAZI za kijamii! Ulikuwa kuiangalia mtaa unaweza ona mbele hata kilometer 5 usione hata karatasi! Badae nikaenda baada ya miaka 15 dooh salala! Kijiji kichqfu balaa madiwani wanasema tunashindwa kuwafosi watu kwenye KAZI za maendeleo watakunyima kura
Kukosoa hakujawahi kuzuia maendeleo, wakosoaji hawawalazimishi watawala kufuata ajenda zao kwa sababu hawana dola. Hicho kijiji viongozi walichoshindwa kusimamia usafi na mipango ya kijiji ni kwa sababu ya ujinga.
Mbona Moshi wameweza kusimamia usafi kwa muda mrefu??
 
Siku zote wanao shindwa kutimiza majukumu yao Sawa Sawa hutafuta wa kumpa lawama juu ya failure zao.

Leo hii useme chama kama UDP,CUF nk sababu ya kukosa serikali ya CCM basi wanazuia maendeleo how ? Na wakati huo huo bajeti ya kununua magari ya kifahari ya Tamisemi ni kubwa kuliko baadhi ya wizara.
Hawa wafuasi wa CCM wanadhani kila mtu ni mpumbavu.
 
Na hapo ndipo huwa inakuwa...

Always majority ya watu huwa sio intelligent, wajinga ni wengi kuliko wenye akili hata darasani tu, level ya mkoa hadi nchi... Na serikali zinajua kucheza na akili za wajinga wengi..
Sio kweli, nchi nyingi za Ulaya zina raia wengi wenye akili na imefanya demokrasia kushamiri. Pia kadri nchi inavyopata maendeleo ndivyo raia wake wengi wanaelimika na kutaka demokrasia zaidi, hata kama maendeleo yalipatikana chini ya udikteta, ndio maana unaona Korea Kusini, Singapore, Malysia na Indonesia zimefuata mkondo wa demokrasia.
 
Twende huku
 
Uozo unaanzia juu😁! Iko hivyo duniani kote...Huwezi kuongoza watu ukataka wawe wasafi ikiwa wewe ni mchafu tayari.
Kwani hao viongozi walioko juu wanatoka mbinguni mkuu?siwanatoka miongoni mwa jamii yetu?

Tatizo la waafrica Sio uongozi bali ni mfumo wa kifkira kwenye jamii yetu ,na ndio maana mtu utamkuta anapiga kelele kuhusu ufisadi lakini akipewa nafasi ya uongozi badala ya kuondoa huo ufisadi alio kuwa anaupigia kelele yeye ndo anaenda kuwa fisadi mara 10 ya aliye mtangulia.
Sasa hivi mfano chadema akachukua nchi nakuhakikishia hakuna chochote kitakacho badilika ndani ya nchi hii.
 
Demokrasia ni utawala bora.

Sasa ki vipi utawala bora usiwe kichochezi cha maendeleo katika nchi ?
Ondoa akili za kiform two hizo

Bado tu umekalili mambo uliyofundishwa huko shuleni badala kuyahusishanisha na uhalisia hili ujue ulichofundishwa ni sahihi au sio sahihi???

Eti demokrasia ni utawala Bora.. yaan hata Aibu huoni kutamka kauli kama hii mbele ya critical thinkers waliopo hapa jamvini?
 
Wewe ni critical thinker ?

Kama demokrasia sio utawala bora ni nini sasa ?
 
Wewe ni critical thinker ?

Kama demokrasia sio utawala bora ni nini sasa ?
Demokrasia inategemea kwa kiasi kikubwa factors 3 zifuatazo hili iweze kuleta positive impacts

1). Historia na asili ya watu wa jamii husika, kwa watu ambao wamezoea kutawaliwa kwa mtindo wa kifalme, mfano kama waarabu leo hii ukiwapelekea demokrasia hawawezi kuwa katika chain ile ile ya maendeleo, lazima watayumba.

2). Ufahamu/elimu na ethics, hili hiyo demokrasia yako iwe applicable kwa urahisi ni lazima watu wawe na ufahamu wa kutosha na pia vile vile watakaochaguliwa wawe na Nia ya dhati, Sasa kwa afrika hapa ni raia wangapi wanaojua demokrasia ni kitu gani? Na viongozi wangapi waadilifu tulionao?

3).Uchumi wa jamii husika, demokrasia Ina thrive kwenye jamii ambayo tayari wameshafika level Fulani hivi ya kiuchumi, yaani hawana Tena njaa, Sasa hapa kwetu kwanzia wapiga kura tu wenyewe Wana njaa kama nini wanajua kabisa kiongozi Fulani ni fisadi lakini wakihongwa hela ya chumvi tu wanaenda kumpigia kura huyo huyo.. Sasa hapo maendeleo yataletwa na hiyo demokrasia saa ngapi??

Kimsingi Demokrasia sio main indicator ya utawala Bora, na neno utawala Bora likoo too subjective.

Nachoona Wewe Bado umekalili terminologies za Civics ya Form Two na umekuwa nazo mpaka leo hii, hujataka kabisa hata ku-unlearn hili kupata uhalisia na undani wa hicho ulichofundishwa huko shuleni.
 
Back
Top Bottom