Kwanini Graduates wengi hawapendi kazi zenye kipato kidogo?

umeanza vizuriii ila kwa ulichosomea subiri hadi sensa ya 2032…
 
kwa mawazo yangu siyo kwamba wamedharau pasipokuwa na sababu ya msingi ila wametumia elimu yao kutazama kilichopo mbele. Kumbuka kuna garama ambazo watakumbana nazo kama wakianza hizo kazi mfano nauli ,chakula,mawasiliano n.k hivo wanaweza jikuta hata huo mshahara usitoshe kukidhi hizo garama. Hapo bado kuna kodi kama mshahara utakuwa umefikia kiwango cha kukatwa kodi, bima ya afya, ada ya chama cha wafanyakazi,marejesho ya mkopo wa elimu kwa wale waliokopa.Na ukirudi kwenye familia zetu za kimaskini ndugu nao wataanza kukuomba bila fahamu kiwango kidogo unachopata na ukiwanyima ndiyo mwanzo wa kukwaruzana na ndugu.Ni kweli exposure inasaidia lakini garama za maisha zipo juu ndiyo sababu hasa. Mtu anaona bora akiwa nyumbani anaepuka garama kama hizo.Unajisikiaje unaenda kazini halafu mwisho wa mwezi mshahara wote unaishia kwenye nauli unabaki huna hata senti. Fikiria kwa mtu aliyeko Dar anaishi mbagala nauli 500/=mpaka mjini na kurudi 500/= jumla 1000/=. kwa siku 30 ni kama 30000/=. sasa hiyo ni nauli tu.
 
Jua kwamba kipato kidogo kinazaa kikubwa kulingana na juhudi zako. Walioajiriwa jaribu kugawa unachopata kwa mwezi kwa 30, uone unapata ngapi kwa siku. Utagundua ni kidogo ila ni ule uhakika wa maisha unaopata.
 
Kuna kazi watu wanalipwa iyo pesa lakini madili yako kibao. Mpk mfanyakazi aendi kutoa salary yake baada y miezi 3.
 
Kwasababu wanaangalia sana bongo movie kipindi cha likizo
 
Mentality tuliyojengewa Toka vizazi na vizazi kua ukisoma baasi sharti upate Kazi ya tai shingoni

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Mentality unayo wewe. Muda unaotumika masomoni ni mrefu na pindi MTU anapohitimu tayari majukumu yameshamkaba. So lazim apate mshahara unaoendana na mahitaji kwa hasa ya kifamilia.
 
Kuna kazi watu wanalipwa iyo pesa lakini madili yako kibao. Mpk mfanyakazi aendi kutoa salary yake baada y miezi 3.
ni mpaka ubahatike ofisi ambazo wanakupa muda wa kujiendeleza na madili au issue zingine. Kuna ofisi unaweza fikiria upo jela ukitoka tu kidogo ushatafutwa na mikwala kibao na sababu wanajua uhaba wa kazi ndiyo kabisaaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…