Kwanini huwa tunalipia kodi ya pango la ardhi wakati ardhi tumeikuta ipo bure? Why?

Wazo zuri ila wapangaji ndio walipaji wakuu kweny kununua LUKU.
Yaani mwenye nyumba anachukua. Chake na mweny nchi anachukua humo humo
 
Hiyo miundombinu mbona tunailipia? Ingekuwa mtu akijenga anasogezewa Huduma zote BURE sawa lakini huduma zote tunauziwa ni BIASHARA!
Ndo maana nikasema kimsingi hatuipati.

Barabara
Madaraja
Taa za barabarani
Mifereji
Je tunavipata hivyo?
 
Ndio hivyo ukisoma universal law na ukaielewa hupati tabu,
 
Na hapo ujanja ni wewe kujichomeka Serikalini
 
Kwa mujibu wa Sheria, Hakuna Ardhi iliyokaa bure tu, Ardhi ni mali ya umma na msimamizi mkuu ni Rais, wewe unakuwa umepewa tu hati ya kuimiliki kwa miaka kadhaa lakini lazima uendelee kulipa kodi kwa msimamizi mkuu (Rais)
Halafu hili suala la ardhi yote kumilikiwa na Raisi ni bongo tu.

Hapo Kenya ardhi ni Mali binafsi hivyo kurahisisha maendeleo na muendelezo wake.

Kifupi ukifatilia historia ya Kodi haikuanza miaka mingi na raia walichangia serikari kipindi Cha Vita.

Kodi ilianzishwa ili kutozaa matajiri ila Serikari ilivyoanza kuonja fedha taratibu wakaiweka kwa jamii nzima.

Sasa kutokana na mlundikano wa Kodi tumekuwa State Slaves.

Hii kutozwa Kodi mara mbili kwenye kitu kile kile inakera kwa kweli(Double Taxation)
Fikiria unalipa Kodi ya ardhi na jengo kwenye kiwanja kile kile.
 
Hewa haiuzwi wala kununuliwa , ardhi inauzwa na kununuliwa , lazima itozwe kodi mana ipo ndani ya mipaka ya kimamlaka
 
Ngoja tusubiri ufafanuzi kutoka kwa wasomi
Hili halihitaji usomi, ni kujuwa tu sheria za Ardhi.

Ardhi yote ni Mali ya serikali, tena zamani ilisomeka kama Mali ya Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania.
.unalipa kodi ya Ardhi kwa sababu serikali imekupangisha kwa miaka 33 au 100 na siyo milele.

Serikali ikiwa na Mipango yake inachukuwa Ardhi yake kwa kuthaminisha na kukulipa fidia, hata uwe umejenga nini, sanasana utalipwa pesa na kupewa Ardhi nyingine.
 
Ndo maana nikasema kimsingi hatuipati.

Barabara
Madaraja
Taa za barabarani
Mifereji
Je tunavipata hivyo?
Road licence tunakatwa kwenye mafuta!
Kadri unavyosafili ndivyo unalipia zaidi;
Mwaka Jana nilipiga hesabu mafuta niliyonunua kwa mwaka asilimia niliyokatwa kwenye road license inafikia laki 7!
Hii inachangia ujenzi wa barabaranj, madaraja, taa na mifereji, hapo hujaweka Tarula parking fees!
 

Ni wizi mtupu ,wachumi ndiyo walivyofikiria "kubwinu mbwinu" za kuongezea mapato serikalini yaani haina tofauti na ule wizi wa Service charge TANESCO ambao Late JPM aliuondoa.

Kwa viwanja vilivyopimwa unalipia kila mwaka kodi Ardhi na Pia Kila mwezi unakatwa kodi ya jengo kupitia Tanesco yaani ni WEEZY WEEZY.
 
Ardhi ni mali ya serikali kwa mujibu wa sheria za ardhi. Shangaa hata makaburi uhamishwa wakitaka kupitisha barabara hapo au kujenga majengo hapo. Bora tu serikali imiliki ardhi vinginevyo ingekuwa ni vurugu tupu kwa wababe kunyang'anya wenzao ardhi wanazojenga na kulima. Ardhi ina mali nyingi kama madini mabepari wanaitaka, utageuzwa kabwela pepari likimiliki ardhi
 
Hiyo sheria kwanini isingewekwa na kwenye hewa!?
Yaani walitungia sheria kitu ambacho siyo man made! (Siyo cha kwako unakitungiaje sheria kujimilikisha?)

Yaani unalitungia sheria jua, mwezi, ardhi, hewa hii si sawa hata kidogo! Wakaiboreshe!
 
Yesu alishamaliza huu utata siku nyingi, aliwaambia ya Kaizari mpeni Kaizari.

Wengi hawajui Yesu alikuwa analipa kodi, kwahiyo Hakuna kiumbe yoyote wa kushindana na mfumo huu, huu siyo mfumo kristo, huu ni mfumo Babylon.
 
Yesu alishamaliza huu utata siku nyingi, aliwaambia ya Kaizari mpeni Kaizari.

Wengi hawajui Yesu alikuwa analipa kodi, kwahiyo Hakuna kiumbe yoyote wa kushindana na mfumo huu, huu siyo mfumo kristo, huu ni mfumo Babylon.
Kwanini hewa isitozwe kodi?
 
It sucks but taxes are necessary wether we want them or not..You never really own land..You rent it from the Government forever.

Huu ndio mfumo wa Kiutawala Kiongozi Dunia nzima..Point yako imeeleweka but You have to understand where the money is going. Property taxes are the ONLY way that the city/town makes money. So no property taxes=no police, no schools, shitty roads, ect.
 
Ni sawa na Wasaudia walivokuta mafuta ya bure kwny ardhi yao afu useme wayagawe bure,I doesn't make any sense
 
Hiyo sheria kwanini isingewekwa na kwenye hewa!?
Yaani walitungia sheria kitu ambacho siyo man made! (Siyo cha kwako unakitungiaje sheria kujimilikisha?)

Yaani unalitungia sheria jua, mwezi, ardhi, hewa hii si sawa hata kidogo! Wakaiboreshe!
Yesu alishindwa kuwajibu Wayahudi swali hili hili, akawaambia ya Kaizari mpeni Kaizari.

Kumbuka Yesu alikuwa analipa kodi na kuna watu wanaamini Yesu ni Mungu, Imagine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…