Kwanini huwa tunalipia kodi ya pango la ardhi wakati ardhi tumeikuta ipo bure? Why?

Tokea zinaanzishwa, serikali ni vikundi vya waporaji ambao wanakutoza kodi na kusingizia ni kwa manufaa yako.
 
Hili nilishawah lifikiria nikawaza labda kwa vile wakina nyerere waliipata hii nchi kutoka kwa wakoloni hvyo tunalipia nguvu kazi iliyotumika kuipata kutoka kwa mkoloni
 
Sio wamiliki wote wa ardhi walinunua,wewe unanunua ardhi kwa sababu umechelewa kuja kuitafuta kwa hiyo unampa fidia tu mtu aliyeiwahi na kuitunza kwa ajili yako
... na hapo ndipo point ilipo; ardhi ni scarce resource ndio maana sio kila mtu anayo. Wale wachache waliyo nayo wailipie kwa maendeleo ya wote including wasiokua nayo.
 
Mapori bado yako mengi ndugu nenda Namtumbo huko hata bure unapata,sema tunalipishwa kwa sababu wengi tunakuja kurundika mjini kwenye kasehemu kadogo
 
Hewa hatulipii,maji pia hatulipii bali tunacholipia pale ni huduma ya kusafishiwa na kusogezewa karibu.
Nenda kachote maji ya mtoni au kisimani kama kuna mtu atakudai pesa
Tazama post #33
 
Mambo mengine mtu ukiwaza unaona kabisa maisha ni mepesi kimtindo lakini kuna baadhi ya wanadam wenye dhamana ya uongozi ndiyo waliyoyafanya maisha yawe magumu!

Tumeumbwa ardhi ilikuwapo, tumepata Uhuru, ardhi ilikuwapo milele hadi milele yote!

Sasa kwanini tunalipia kodi ya pango la ardhi wakati tayali ipo BURE?
Huduma zingine za kijamii tunazolipia naelewa ni sawa zinazalishwa viwandani hivyo ni mhimu kulipia!
Sasa hili la kodi ya pango ya ardhi kwanini tulipie wakati tumekuja duniani ili tuishi kwenye ardhi halisi BURE?
yaani kwa lugha nyepesi Ardhi ipo kundi moja na hewa! Kama tunalipia kodi ya ardhi kwanini tusilipie na kodi ya hewa?

Naomba kueleweshwa! Vinginevyo naomba serikali ifute hii TOZO ya ARDHI ya ardhi mara moja!r
Ardhi Haipaswi kabisa kutozwa kodi TUMEPEWA BURE ! WACHA TUISHI NAYO BURE!
Wacha kupenda vya bure, unafikiri barabara unazoziona na lami zinakuja bure?
 
Mapori bado yako mengi ndugu nenda Namtumbo huko hata bure unapata,sema tunalipishwa kwa sababu wengi tunakuja kurundika mjini kwenye kasehemu kadogo
Location matters! Pale mnapogombea thamani iko juu wachache wanaomiliki hawana budi kulipia kodi kwa faida ya wengi.
 
Thamani imekuja juu baada ya watu wengi kurundikana,Sinza na kinondoni zamani ilikuwa mapori pia.
So hata Namtumbo watu wengi wakipakimbilia na kujenga patakuwa juu na thamani itapanda
 
May be hujanielewa,mimi namuunga mkono mtoa mada,hoja yake iko sahihi na ina mantiki
... sidhani kama hoja ya mleta mada iko sahihi sana. Iko hivi, kipande cha ardhi pale katikati ya jiji la Dar, Posta Mpya mathalani ni hazina kila mtu angetamani kukimiliki; why? Kwa sababu kina faida! Kinaingiza pesa. Chochote kinachoingiza pesa kodi ni lazima.
 
Kwani hiyo kodi ya jengo wametangaza inalipishwa Posta na kariakoo?
 
Thamani imekuja juu baada ya watu wengi kurundikana,Sinza na kinondoni zamani ilikuwa mapori pia.
So hata Namtumbo watu wengi wakipakimbilia na kujenga patakuwa juu na thamani itapanda
Now you're talking! Thamani ikipanda maana yake ardhi hiyo inakuingizia pesa! So, hoja ya kulipia kodi inakuwa valid.
 
Mambo mengine mtu ukiwaza unaona kabisa maisha ni mepesi kimtindo lakini kuna baadhi ya wanadam wenye dhamana ya uongozi ndiyo waliyoyafanya maisha yawe magumu!

Tumeumbwa ardhi ilikuwapo, tumepata Uhuru, ardhi ilikuwapo milele hadi milele yote!

Sasa kwanini tunalipia kodi ya pango la ardhi wakati tayali ipo BURE?
Huduma zingine za kijamii tunazolipia naelewa ni sawa zinazalishwa viwandani hivyo ni mhimu kulipia!
Sasa hili la kodi ya pango ya ardhi kwanini tulipie wakati tumekuja duniani ili tuishi kwenye ardhi halisi BURE?
yaani kwa lugha nyepesi Ardhi ipo kundi moja na hewa! Kama tunalipia kodi ya ardhi kwanini tusilipie na kodi ya hewa?

Naomba kueleweshwa! Vinginevyo naomba serikali ifute hii TOZO ya ARDHI ya ardhi mara moja!r
Ardhi Haipaswi kabisa kutozwa kodi TUMEPEWA BURE ! WACHA TUISHI NAYO BURE!
Hewa hatulipishwi kwasababu hakuna hatari ya kupungua na kusababisha wengine wakose.
Ardhi ni tofauti kidogo, ukichukua sehemu ya ardhi umeshawazuia wengine wasiitumie na hivyo kutengeneza uhaba wa kiasi fulani.
Nadhani wamelenga udhibiti zaidi kuliko mapato, hayo malipo kiduchu unayolipa ni kwa ajili ya operating expenses ya huo udhibiti.
 
Hewa hatulipishwi kwasababu hakuna hatari ya kupungua na kusababisha wengine wakose.
Ardhi ni tofauti kidogo, ukichukua sehemu ya ardhi umeshawazuia wengine wasiitumie na hivyo kutengeneza uhaba wa kiasi fulani.
Kwa hiyo kodi ikikusanywa ndio itasaidia ardhi kuongezeka na kupewa hao waliokosa ardhi?
 
Kwani hiyo kodi ya jengo wametangaza inalipishwa Posta na kariakoo?
... hata kwa mifano huelewi? Kila kipande cha ardhi kina thamani yake kutegemea kiko wapi na kodi inatofautiana based on those factors.
 
Bado hujanishawishi,kwa mfano mimi niko na nyumba maeneo karibu na Goba na siingizi hata shilingi 100 je hapo watanipa excuse ya kutolipa kodi?
 
Back
Top Bottom