Kwanini huwa tunalipia kodi ya pango la ardhi wakati ardhi tumeikuta ipo bure? Why?

Kwanini huwa tunalipia kodi ya pango la ardhi wakati ardhi tumeikuta ipo bure? Why?

Mimi nafikiri watu wengi wameshindwa kukuelewa logic yako nini wanakurupuka kujibu,kuna wengine wamekariri notsi za darasani.
Nijuavyo mimi serikali inapaswa kudai kodi mahali walipopaendeleza ili kufidia gharama zao na kuendelea kupatunza mahali hapo.
Kwa mfano Soko,Kivuko,bandari au huduma yoyote wanayoisimamia directly mfano kusambaza maji,umeme.
Sasa hoja ya mtoa mada ni hivi"Ardhi ni yake alinunua,nyumba alijenga mwenyewe bila support ya mtu yeyote ni kwa nini alipishwe kodi?
Wewe ndio huelewi, tangu umezaliwa umeikuta Ardhi ni Mali ya serikali.

Usipoelewa vitu vidogo kama hivi basi repoti ya CAG ndio wala usiangaike hata kusoma.

Ukiona kitu chochote kina expire date ujuwe si chako cha milele.

Ardhi ni kama driving licence tu, mamlaka wakitaka Leseni yao wanaichukuwa.
 
Mada nzuri sana na nimependa wachagiaji wamechangia kwa busara bila matusi wala lugha za kukera,

Nimebaki njia panda kulingana na maoni ya wadau,
1. Ardhi isilipiwe sababu tumeikuta ni kitu cha Asili kama ambavyo hatulipii hewa

2. Ardhi inalipiwa sababu umekua mmiliki na ukiwa mmiliki ni wazi inakuletea faida na chochote kikupacho faida basi kilipiwe kodi,

Lakini kwanini nilipie ardhi kila mwaka wakati kinachonipa faida ni jengo na tayari jengo nalipia kila mwezi?
Kinachokupa faida ni biashara iliyomo ndani ya jengo! Hivyo kodi inalipwa kwenye biashara husika!
Ardhi ni vazi sasa unalipiaje kodi vazi la lazima?
 
Kwa ufupi,
1. Kodi lazima ilipwe kwa mfalme. Hiyo ni tanguy zama hizo.
2. Kumpa mtu umiliki kamili (absolute ownership) wa ardhi ambaye hana uwezo wa kuilinda kisheria, kiusalama, kijeshi nk. ni hatari kwa mstakabali mzima wa taifa lolote. Ukisema ardhi, maana yake ni nyumbani, maana yake ni nchi. Sasa vitus kama hivi haviwezi kuachwa vivi hivi.
3. Sheria inatambua kuwa ardhi ni Mali ya umma. Ikimaanisha mimi na wewe na yule, lakini usimamizi amepewa Rais. Hivyo haki ya kumiliki na kutumia kisheria iko sawa kwa wote, lakini kwa kufuata taratibu zilizowekwa.
1.Kwa nini mfalme atoze kodi ya pango la ardhi wakati ardhi huyo mfalme ameikuta?
2. Mfalme ni binadamu au taasisi aliyoiunda ambayo imepewa ardhi na mungu kama ilivyo kwa wananchi wake, kwanini mfalme atoze kodi kwenye ardhi ambayo wote tumeipata bure?.
 
1.Kwa nini mfalme atoze kodi ya pango la ardhi wakati ardhi huyo mfalme ameikuta?
2. Mfalme ni binadamu au taasisi aliyoiunda ambayo imepewa ardhi na mungu kama ilivyo kwa wananchi wake, kwanini mfalme atoze kodi kwenye ardhi ambayo wote tumeipata bure?.
Ndo hapo sasa! Tumechezewa mno!
 
Kama ardhi ni Mali ya uma Kwa Nini mtu akikuuzia eneo labda Kwa milioni 5 serikali kama yenye dhamqna Inachukua 10% tu?maana yake serikali ni dalali sio mwenyewe.
 
Kama ardhi ni Mali ya uma Kwa Nini mtu akikuuzua eneo labda Kwa milioni 5 serikali kama yenye thamqna Inachukua 10% tu?maana yake serikali ni dakali sio mwenyewe.
Sijui kama somo limeeleweka!
Yaani Ardhi ni natural at existing! Swali; kwanini serikali itoze kodi kila mwaka?
 
Hujaelewa mada.
Tofautisha kati ya kodi na mauziano.
Mauziano ya ardhi huwa ni makabidhiano ya ardhi kutoka kwa mmiliki wa mwanzo aliyewahi kwenda kwa mmiliki mpya(aliyechelewa kuipata) na malipo hufanyika mara moja tu.
Lakini kodi ni tozo kwa mmiliki wa ardhi na ambayo hujirudia mara kwa mara na hii ndio hoja ya mtoa mada
Tanzania hakuna mtu anamiliki ardhi. Wote tumekodisha kwa serikali.
 
Sijui kama somo limeeleweka!
Yaani Ardhi ni natural at existing! Swali; kwanini serikali itoze kodi kila mwaka?
Swali limeeleweka ni kwamba serikali inalipisha udalali kwa manufaa Yao ili baadaye CAG awahoji.
 
Tanzania hakuna mtu anamiliki ardhi. Wote tumekodisha kwa serikali.
Ndio ni kwa mujibu wa hao wakusanya kodi ndio waliitunga hiyo sheria,lakini bado swali la mtoa mada litabaki palepale ni kwa nini iwe hivyo wakati ardhi yote iliumbwa na Mungu ili binadamu waitumie?
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Aliyewahi kuichukua ndio anahesabika ni mmiliki kisha yeye ataamua kummilikisha mtu mwingine kwa malipo fulani,hiyo ndio asili yake ilikoanzia.
Bila hivyo ingekuwa vurugu ingekuwa kiwanja kimoja wanajazana watu 100.
Na kumbuka si wamiliki wote wa ardhi walinunua kwa pesa,wengine waliwahi tu mapori wakajimilikisha
Mbona hewa hatuuziani lakini hakuna vurugu ushawahi kusikia sehemu watu 100 wanagombaniana kuvuta hewa basi Kama hewa kaumba Mungu hatugombaniani kila mtu ni yeye tu na ukubwa wa pua yake kwanini hio ardhi kuwe na kuuziana na umiliki

Hili la kununua mbona huja hoji unahoji la kodi
 
Ni kwa sababu unapotumia ardhi unamnyima mwingine fursa ya kuitumia hiyo ardhi.

Usingeweka wewe nyumba juu ya hiyo ardhi ningeweka mimi
 
Tanzania hakuna mtu anamiliki ardhi. Wote tumekodisha kwa serikali.
Kwa nini tukodishwe na Serikali wakati Ardhi tumeikuta na Kama ilivyo hewa ndio urithi wa mwanadamu?
Kama tunakiri kuwa wakoloni walitwaa ardhi zetu, wakagawa vipande na kuweka Serikali zao, zikajiendesha kwa kodi za dhulma kama hii, kwa nini Serekali yetu inaendeleza ukoloni ule ule kwa watu wake?
 
Ni kwa sababu unapotumia ardhi unamnyima mwingine fursa ya kuitumia hiyo ardhi.

Usingeweka wewe nyumba juu ya hiyo ardhi ningeweka mimi
Kwani hewa unapovuta wewe, mwingine anakosaje?

Kwanini umuwaze mtu mwingine asiyeishi hapo badala ya kuwaza hiyo ardhi pia imenufaisha wanayoitumia!

Haya unapochukua kodi ya ardhi huyo mwingine atapata ardhi ya kufidiwa?
 
Kwa nini wadhibiti matumizi ya ardhi wakati iliumbwa ili tuitumie kwa kujinafasi?Maana dunia ndio hii hii moja hatuna dunia nyingine ya kwenda
Kudhibiti nilikuwa na maana ya kusimamia kwa ajili ya manufaa ya wote.
 
Ulaya ndio matumizi ya kodi huonekana ndugu.
Kama hata panadol ya bure hospitalini hakuna utajihesabia kuna matumizi sahihi ya kodi.
Ulaya Huduma za Afya ni bure tena ni huduma bora na si bora huduma.
Tungekuwa na proper budgeting madini tu tuliyonayo na bandari vingetosha kufanya kila kitu lakini cha ajabu haieleweki hizo pesa wanazitumia vipi hadi zinaisha wanakuja kutembeza bakuli kwa walalahoi mitaani.
Sipendi kuzama kwenye siasa ila kutokana na comment yako imenifanya nifunguke
... wewe sasa una-diverge; hoja hapa ni sahihi kulipa kodi ya ardhi? Kwamba kuna misuse ya kodi hiyo ni topic nyingine kabisa! Let's be focused vinginevyo mjadala huu utakuwa hauna mwelekeo unaoeleweka.
 
Back
Top Bottom