Kwanini January Makamba unakataa kutambua nguvu na juhudi za hayati Magufuli kwenye JNPP?

Najuta kuwa part ya this generation...,

walamba asali wapo pale ku-justify ulambaji wao sisi huku so called thinkers tupo kupigana vijembe na wanaomkashifu marehemu na wengine wanaomtetea (yaani tupo busy na kujadili watu na matukio)...

Afadhali ningekuwa generation ya hunters and gatherers huenda sasa hivi ningekuwa nimevaa zangu rubega huku nikitafuta tafuta matunda baada ya kutoka kuwinda swala....
 
Sasa si Samia kamtaja Magufuli, Makamba kawataja wengine.

Au unataka kila mtu arudie majina yaleyale?
 
Kibri tu .lakini Nchi hii inavituko sana yaani Yule alikataa Miradi usianzishwe ndo amepewa jukumu la kusimamia mradi
 
Una picha ya huyo msaliti
 
yule mhutu alikuwa mtu mwovu kupindukia, hata shetani mwenyewe inabidi aingie darasani kwanza kuweza kuukariri uovu wake.
Nikimkuta ahera naenda mwenyewe Motoni nafikiri kutakuwa raha huko
 
Kibri tu .lakini Nchi hii inavituko sana yaani Yule alikataa Miradi usianzishwe ndo amepewa jukumu la kusimamia mradi
Baada ya kuona utafanikiwa sasa kajipachika kuwemo kwa history,aibu sana
 
Maisha hayo yapo kabisa sema wewe unang'ang'ania kuishi sehem ambayo sio level yako
 
sema weww hudanganyiki, usijaribu kuchanganya watanzania wote,
 
Tupua basi hata kapicha?!
 
Hili ni tatizo kubwa la siasa za TZ zimejikita kuhangaika na haiba za wanasiasa kuliko kutazama mfumo kwa ujumla unafanikiwa au la.

Hao wastaafu wawili Kikwete na Mwinyi wanaongelewa kama hawakufanya lolote la maana!, Mwinyi aliipokea nchi wakati hazina ikiwa inanuka vumbi tupu, yaani ni sawa na mtu anayekung'uta pochi akiwa hana hata senti moja. Na taratibu akaanza kubadilisha hali za maisha ya mtu mmoja mmoja.

Mzee Kikwete hali kadhalika, amepambana mpaka MOI ikajengwa, amepambana mpaka leo watu wa Dar wanasafiri kwa mwendo kasi. Amepambana sana kuanzisha miradi mingi iliyokuja kuendelezwa na JPM.

Kumpamba JPM huku wakipondwa marais wengine ni kutowatendea haki hawa wazee, pia ni ushamba kumsifu sana mmojawao wakati utaratibu ni ule ule wa kuachiana vijiti, kumpa ushujaa wa ajabu wakati kuna mengine aliyapokea kutoka kwa Kikwete na yeye aliyapokea kutoka kwa Mkapa ni muendelezo ule ule wa mawazo ya kibinafsi na ya kishamba pia.
 
Nafasi ipo...Unaweza kuvaa rubega na kuwa hunter kama huwezi kulamba asali na hutaki kuwapiga vijembe wanaomkashifu marehemu.
 
Maisha hayo yapo kabisa sema wewe unang'ang'ania kuishi sehem ambayo sio level yako
Unajua maana ya kipindi cha hunters and gatherers ?

Ni kwamba kipindi hicho as a human that was the best one can.. kupambana na mazingira ni kujitafutia chakula na kukimbia threat (simba n.k.) hivyo mababu zetu they did the best they could at the time...

Sasa hivi karne ya Sayansi na Teknolojia we can achieve a lot as a group ila ndio hivyo tena tunashikana uchawi na kuendekeza uzandiki....

Kwahio as part of generations bora ningekuwa hao mababu zetu at au at best generation ya Pioneers sio hii generation ya walafi na wazandiki....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…