Kwanini January Makamba unakataa kutambua nguvu na juhudi za hayati Magufuli kwenye JNPP?

Kwanini January Makamba unakataa kutambua nguvu na juhudi za hayati Magufuli kwenye JNPP?

Ukweli lazima usemwe,kuna tatizo gani kutambua juhudi za hayati Magufuli kwenye mradi huu wa umeme (JNPP),hasa kwenye hotuba zenu?

Wazo lilikuwa la Mwalimu Nyerere ,akashindwa,awamu zilizofuata kuanzia ya pili mpaka ya NNE,hawakuwa na habari na mradi huo,waliupa kisogo.

Hayati Magufuli kwa nguvu kubwa na ujasiri usio na shaka akaamua kutekeleza wazo hilo.
Miongoni mwa waliohujumu juhudi hizi ni waziri wa sasa wa nishati, January Makamba kwa kisingizio cha uharibifu wa mazingira,ikapelekewa kuondolewa baraza la mawaziri.

Leo hotuba ya mkurugenzi mkuu Maharage Chande na waziri wake wamejificha kwenye kichaka cha mipasho ,hasa waziri Makamba.

Nijielekeze kwenye usanii wa waziri kutambua juhudi za watangulizi kwenye ujenzi wa bwawa hilo,katengeneza zawadi za kutambua michango ya mzee Mwinyi na Jakaya,wana mchango gani ikiwa mradi waliupa kisogo?
Makamba junior kawapa medal za kinafiki sana,hata wao wamejisikia aibu sana kupewa medal za ushiriki wao wa mradi wakati hawajashiriki hata kidogo.

Huyu kijana ndio awaza kuwa rais wa hii nchi.tuna hasara kubwa kama taifa.

Nimpongeze rais Samia kwa kujaribu kuusema ukweli kuhusu kazi kubwa ya hayati Magufuli katika kufanisha mradi huu.

Kumekuwa na ka syndicate kupoteza Juhudi za hayati Magufuli kwa kuzimeza kijumla jumla na wasiostahili .moja wapo ni hilo tukio la kinafiki la kutambua mchango wa bwawa wakati si washiriki.

Namalizia kwa kumwambia waziri Makamba na walio nyuma yake kwamba watanzania hawadanganyiki tena , Magufuli aliwafumbua macho.

Huu mchezo wa kujaza vijana mitandaoni kumdhihaki, mmeona leo jinsi likitajwa jina lake makofi na shangwe kama lote.

Nikiashiria kwamba kimwili hatuko naye ila kifikra tukonae,acheni majungu dhidi ya marehemu.
Kuna Mhudhuri humu kwa jina la Sangudi, kiunagaubaga ameandika sehemu....Taratibu wataelewa ni nini maana ya 'Uongozi' ni nini maana ya 'Ujasiri' ni nini maana ya 'Uzalendo' ...kiufupi, Ni nani hasa aliyewaletea heshima Watanzania na Waafrika kwa Ujumla katika kuchanganua na kufanya yale yanayowafaa!

-isitoshe, tumeona na kusikia jinsi nchi mbali mbali hapa Afrika na huko Ulaya wakifanya maamuzi ambayo yalikuwa yakionekana kama yanaweza kuleta mfaragano aidha baina ya nchi au watu wake. Mfano mpya ni Pale nchi ya Denmark kwa sasa kuelekeza fedha zinazotumiwa kwenye sherehe, kuelekezwa kwenye miradi yenye Chanya. Hiyo ni #MAGULIFICATION of Denmark.

mic drop.

Makamba anajua hapo alipo ni, na , zilikuwa nguvu za Hayati Raisi J.P.M katika uelewa wake wa kujali na kuongeza nguvu za Vijana katika kujenga Nchi. kwani wao ndio Nguvu ya kesho.

Aluta Continua.
 
Lakini ssh amesema wazi kuwa ujasiri na maamuzi ya awamu ya tano chini ya magufuli,

Na shangwe nyingi sana.

R.I.P magufuli
Watu ni walalamishi kinoma..

SSH kampa heshima yake kabisa kwamba JPM alisema kivyovyote lazima ujenzi uanze na akapongeza uthubutu wake.

Hawa washamba wanataka nini cha ziada kifanyike?
 
Nimeona twitter Lema nae anamponda Makamba kutowaalika PM na Makamu wa Rais kwenye hiyo shughuli, kama hii ni kweli, naona Makamba sasa anaonekana kama mtoto wa mama anayedekezwa sana.
 
Kuanzia Tuzo , Et anapewa JK , anapewa Mwinyi .... Walifanya nn? Sibora mngechomekea na JN mwanzilishi wa Wazo?.


Et wanashindwa kutaja Awamu ya JPM, badala yake wanamuingizia kwenye awamu kiujumla jumla .!!


Mkamba JR, una utoto na uswahili , wewe hufai hata kua Balozi wa nyumba kumi.


Huwezi Kumtenganisha JPM na JNHEPP , huwezi na ni mjinga pekeake tu ndo anaweza kumtenganisha, Tena ni mjinga, asokua na haya, na mnafiki, mwenye kiburi anayejiambia 'Hamna wakunigusa'.


NEC walichokuonyesha ,hakijakufunza?

Watanzania wanajua, nani ni nani kwao, hizi porojo zako, ni kutojielewa na kuendelea kunishushia Heshima ndogo ulobakiwa.


Wewe sindo ulikua kimbelembele kupiga vita Huu mradi Kwa JPM?.

Sasa yule yule ulokua unampiga Vita, unajifanya kujisahaulisha ?.



Makamba Jr. Acha Utoto !!.

Watanzania wangekuwa wanajua yeye ni nani angepora uchaguzi? Ukiishi kwa hujuma hata ukifa unalipwa hujuma.
 
Nimeona twitter Lema nae anamponda Makamba kutowaalika PM na Makamu wa Rais kwenye hiyo shughuli, kama hii ni kweli, naona Makamba sasa anaonekana kama mtoto wa mama anayedekezwa sana.
Itakua kweli , huyu jamaa Kwa Sasa ni mtoto pendwa .

Alafu ana ujanja ujanja Fulani ivi ambao Kwa Sisi akili kubwa, tunamuona mjinga.


Anamtanguliza Samia mbele, yeye anakua nyuma
 
Back
Top Bottom