Ukweli lazima usemwe,kuna tatizo gani kutambua juhudi za hayati Magufuli kwenye mradi huu wa umeme (JNPP),hasa kwenye hotuba zenu?
Wazo lilikuwa la Mwalimu Nyerere ,akashindwa,awamu zilizofuata kuanzia ya pili mpaka ya NNE,hawakuwa na habari na mradi huo,waliupa kisogo.
Hayati Magufuli kwa nguvu kubwa na ujasiri usio na shaka akaamua kutekeleza wazo hilo.
Miongoni mwa waliohujumu juhudi hizi ni waziri wa sasa wa nishati, January Makamba kwa kisingizio cha uharibifu wa mazingira,ikapelekewa kuondolewa baraza la mawaziri.
Leo hotuba ya mkurugenzi mkuu Maharage Chande na waziri wake wamejificha kwenye kichaka cha mipasho ,hasa waziri Makamba.
Nijielekeze kwenye usanii wa waziri kutambua juhudi za watangulizi kwenye ujenzi wa bwawa hilo,katengeneza zawadi za kutambua michango ya mzee Mwinyi na Jakaya,wana mchango gani ikiwa mradi waliupa kisogo?
Makamba junior kawapa medal za kinafiki sana,hata wao wamejisikia aibu sana kupewa medal za ushiriki wao wa mradi wakati hawajashiriki hata kidogo.
Huyu kijana ndio awaza kuwa rais wa hii nchi.tuna hasara kubwa kama taifa.
Nimpongeze rais Samia kwa kujaribu kuusema ukweli kuhusu kazi kubwa ya hayati Magufuli katika kufanisha mradi huu.
Kumekuwa na ka syndicate kupoteza Juhudi za hayati Magufuli kwa kuzimeza kijumla jumla na wasiostahili .moja wapo ni hilo tukio la kinafiki la kutambua mchango wa bwawa wakati si washiriki.
Namalizia kwa kumwambia waziri Makamba na walio nyuma yake kwamba watanzania hawadanganyiki tena , Magufuli aliwafumbua macho.
Huu mchezo wa kujaza vijana mitandaoni kumdhihaki, mmeona leo jinsi likitajwa jina lake makofi na shangwe kama lote.
Nikiashiria kwamba kimwili hatuko naye ila kifikra tukonae,acheni majungu dhidi ya marehemu.