Kwanini ktk maisha ya ndoa watoto wakishafanikiwa humjali mama yao kuliko baba yao?

Biologically watoto wanakua na BOND kubwa zaidi na mama kuliko baba..... mtoto anatumia muda mwingi na mama kuliko baba

Kitamaduni haswa za bongo mwanamke ni kama kiumbe dhaifu mbele ya mwanaume.... kwa muktadha huo watoto wanakua so protective kwa mama zao
 
Tatizo Mnatoa hela ya matumizi gizani, mnawakabidhi wake zenu. Wake zenu wanawaaminisha watoto kuwa wao ndiyo wanatoa hizo hela na siyo baba
Hii si sababu kubwa, na inaweza kuwa si sababu pia. Ukweli ni kwamba, Baba ni cheo ni Nafasi ambayo inamuhitaji kuwajibika kama baba, si kwa sababu tuu umemzalisha mwanamke unajitapa kila mahali nina watoto watano, n.k Swali la msingi je unawajibika katika nafasi yako? Hata kwa kidogo Mungu anachokibariki? Je, unapata nafasi ya kukaa na watoto wako walau mara moja kwa wiki kuzungumza nao kutaniana nao, n.k
Wamama wengi hasa wale maika ile , wamejitahidi sanaa sanaa ku-play part zao vizuri mno. Ndiyo maana unaona wanaonekana kupendelewa. Wakina baba tujitahidi sanaa kutunza familia na kuonyesha mapenzi ya kweli kwa familia zetu. Siku ya mwisho , Mungu hatakuuliza ulikuwa tajiri kiasi gani? Swali litalenga uliweza vipi kuwajibika kwa familia yako? Kazini kwako? Kwa cheo ulichopewa, kanisani kwako/msikitini kwako? n.k
 
Watu wametofautiana sio wote wanaofanya hivyo, kama mtoto wa kiume unafocus kwa mama tu kuzidi baba we ni ndezi.
Kuna wakina baba, walijeruhi mioyo ya watoto wao kipindi wapo wadogo na hata ukubwani. Moyo wa mtu ukijeruhiwa unahitaji counselling ili angalau kuuponya. Mahusiano ya baba na mtoto ni muhimu sana kabla ya kuja kumlaumu mtoto hapo baadae. Upendo wa Mtoto kwa mzazi si wa kulazimisha ni kitu kipo tuu automatically, si cha kujifunza shuleni wala kanisani. Mimi nitaendelea kuihimiza jamii kila mtu achukue hatua, jua kuwa baba si kuzalisha tuu bali ni pamoja na kuwalea watoto kwa namna ya upendo unaostahili, tusijeruhi mioyo ya watoto, ni ngumu mtoto kusahau matendo ya wazazi wake , narudia tena ni ngumu sanaaa!!
 
Watu wametofautiana sio wote wanaofanya hivyo, kama mtoto wa kiume unafocus kwa mama tu kuzidi baba we ni ndezi.
Kama kila kitu kipo sawa basi hakuna mtu anayemchukia mzazi mmoja wapo

Lakini kiuhalisia binadamu wote wana bond kubwa zaidi na mama zao kwasababu za kibaiolojia
 
Jitahidi upate watoto wakike kama unataka kujaliwa mjali Binti Yako sure ata ukiachana na mke wako mtoto wako wakike hawezi kukusahau wa kiume anakusahau akiowa
 
Hili nina ushahidi nalo ni fact
 
Umemaliza kila kitu Demi sijawahi kuelewa ni kwa nini sehem kubwa ya jamii yetu wanapenda kuanza/kutaka kutatua tatizo kuanzia juu kwenda chini. Unakuta mtu anajua kutia mimba tuu na kujitia eti ni provider wa ugali ndondo akidhani hilo pekee ndio familia yake inahitaji. Tujifunze kuwa kila kitu ni uwekezaji sizungumizii pesa hapa 🙂.
 
Kama mwanamme usizeeke na watoto wa tumbo moja!!

Zeeka na watoto was matumbo tofauti hata manne na wote kwa nyakati tofuti wape mahitaji!!

Mtoto anekulia nyumbani haoni umuhim was baba Hadi pale anapomkosa!!

Mtoto was nje anaona umuhimu was baba hasta ukimtembelea na kumpa ten anaona wewe ni baba bora!!

Ni uzembe wa Hali ya juu kuzeeka ukiwa na watoto was mama mmoja huna wengine!!

Kina mama hawasemi mazuri ya waume zao zaidi ya maneno ya kizandiki na ya kishenzi!!Hilo nimeona na kusikia hapa kwangu japo Bado wadogo!!

Hasta uwatunze vipi mwanamke anaanza kuwaondoa watoto mikononi mwako!!

Pia ni vema kujiwekea akiba binafsi plus usizekee kwa mke mkubwa ulieanza name maisha Bali mdogo ambae bado anakihitaji kimaisha!!!

Chukua hiyo mkuu!!
 
Watoto hawatakumbuka pesa ulizowahi kuwa nazo. Mara nyingi wanakumbuka uwepo wako hasa kwenye matukio muhimu. Wazazi tunafeli sana hapa
 
Sasa unataka Wamchukue baba kwao aanze kuunguruma? Hujui fahati wawili hawakai zizi moja?

Madingi wengine wanafujo, anaweza hamishia sheria za kwake hapo kwako ukaishi kama uko gerezani.

Just kidding 😂
 
Mr Spider we umejuaje kama huyo mungu atauliza hayo maswali?🤣🤣
 
Wewe uliishi vipi na wazazi wako. Tupe experience yako na kwa sasa nini kinatokea?
 
Tatizo Mnatoa hela ya matumizi gizani, mnawakabidhi wake zenu. Wake zenu wanawaaminisha watoto kuwa wao ndiyo wanatoa hizo hela na siyo baba
Sometimes its not about money, its your precence, umetenga muda wa kukaa na kubond na watoto wako mara ngapi? Au ndio kutoka kumi na moja kurudi saa tano

Watoto wakilala wapo na mama, wakiamka.mama yupo, weekend wapo home na mama, baba upo busy kutauta, automatically wanajenga mapenzi makubwa na mama kwa.sababu ya uwepo wake wakati mwingi

Muda wao kwa watoto una thamani kubwa sana, tutafute pesa lakini tutenge muda wa kukaa na watoto
 
Kuna Uzi jamaa alishauri humu kama mwanaume pambania familia Yako ila usijisahau kwa maana jiwekee akiba ya uzeeni ili hizo chokochoko zikianza unakaa pembeni unajilia ki akiba chako mdogo mdogo huku unasubilia umauti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…