Until_The_End
JF-Expert Member
- Nov 21, 2020
- 1,456
- 2,202
Huo ni uongo. Tukiwa duniani kila kitu kina mwisho haijalishi kimetoka wapi.Mitume na Manabii kazi yao haina kusitaafu wala kupumzika ni jukumu la milele mpaka Bwana atakapochukua Roho yake. Wote hao uliowataja nguvu zao za kiroho wamezitoa kwa yule mkuu wa kuzimu yule Joka mkuu audanganyaye ulimwengu. Kwa vile mikataba ya yule Joka mkuu ni ya muda/kipindi fulani ndiyo maana wanachuja lengo ile nguvu apewe mwingine katika mazingira mengine ili kumkomoa Bwana muumba kwa kuangamiza waja wake.
Chochote kitokacho kwa Joka mkuu hakiwezi kudumu milele iwe utajiri, umaarufu, uponyaji, unabii hata umaskini maana asili ya ile nguvu siyo ya milele, aliye wa milele ni Bwana muumba, chochote akitoacho yeye kitadumu maisha yako yote. Ndiyo maana utaona manabii na mitume wote wa Bwana, Upako wao ulikoma pale walipotwaliwa hakuna aliyepoteza mvuto akiwa bado yuko hai, hata wafalme waliopata Ukuu kwa jina la Bwana ukuu wao ulidumu maisha yao yote hata wale waliomkosea Bwana kama Sauli na Daudi hakuwaondolea ufalme wao wakiwa hai bali alisubili watwaliwe ndo baraka zake zikome.
Refer:
Nabii Eliya aliishiwa upako hadi akamwomba Mungu ni bora amuue tu, Mungu alitaka kushusha upako wa Musa baada ya Israeli kuzingua, Musa akamwambia 'usitutoe hapa uso wako usipokwenda nasi' Mfalme Sauli na Daudi walikuwa wanashindwa vita upako wao ulipokuwa unapungua............kwa hiyo mifano ipo mingi.