Kwanini mitume na manabii huishiwa upako baada ya muda? Je, hizi pako zao ni za kweli au za mchongo?

Mitume na Manabii kazi yao haina kusitaafu wala kupumzika ni jukumu la milele mpaka Bwana atakapochukua Roho yake. Wote hao uliowataja nguvu zao za kiroho wamezitoa kwa yule mkuu wa kuzimu yule Joka mkuu audanganyaye ulimwengu. Kwa vile mikataba ya yule Joka mkuu ni ya muda/kipindi fulani ndiyo maana wanachuja lengo ile nguvu apewe mwingine katika mazingira mengine ili kumkomoa Bwana muumba kwa kuangamiza waja wake.

Chochote kitokacho kwa Joka mkuu hakiwezi kudumu milele iwe utajiri, umaarufu, uponyaji, unabii hata umaskini maana asili ya ile nguvu siyo ya milele, aliye wa milele ni Bwana muumba, chochote akitoacho yeye kitadumu maisha yako yote. Ndiyo maana utaona manabii na mitume wote wa Bwana, Upako wao ulikoma pale walipotwaliwa hakuna aliyepoteza mvuto akiwa bado yuko hai, hata wafalme waliopata Ukuu kwa jina la Bwana ukuu wao ulidumu maisha yao yote hata wale waliomkosea Bwana kama Sauli na Daudi hakuwaondolea ufalme wao wakiwa hai bali alisubili watwaliwe ndo baraka zake zikome.
Huo ni uongo. Tukiwa duniani kila kitu kina mwisho haijalishi kimetoka wapi.

Refer:
Nabii Eliya aliishiwa upako hadi akamwomba Mungu ni bora amuue tu, Mungu alitaka kushusha upako wa Musa baada ya Israeli kuzingua, Musa akamwambia 'usitutoe hapa uso wako usipokwenda nasi' Mfalme Sauli na Daudi walikuwa wanashindwa vita upako wao ulipokuwa unapungua............kwa hiyo mifano ipo mingi.
 
Gwajima anaombea wafuasi wake ulinzi kiimani wkt huo yy kiunoni ameficha gun[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Yeye anazungumzia nguvu wewe unaongelea pesa. Pesa wanazo je nguvu za mwanzo bado zipo?
Kila siku na kila wilaya naona misukule inarudishwa, wanaosema ni ya michongo sawa, wanatimiza andiko, Baba Ibrahimu alimwambia tajiri (yule aliyekufa na Lazaro, akitaka mmoja wa wafu aende kuwahubiri ndugu zake), Ibrahimu anasema" .... hata mtu akifufuka kutoka kwa wafu, hawatashawishwa"

Ni nguvu gani nyingine tunataka kuiona?
 
Mzee wa upako aliamia kuwa mlevi, mwingira kazaa na mke wa mzungu, gwaji boy kakutwa na kahaba, kakobe kaficha fedha kwenye majaba pia kawakataa wadhamini wa kanisa kwama hawana chao kanisa la kwake. Kesi kasinda mahakamani kwa kanisa ni mali yake. Mwamposa waumini wake walikanyagana na kuangamia yeye kabeba fuko la hela kapanda ndege kia kukimbiza hela dar. Suguye kanisa limefungwa na serikali halina usajili. Mwamposa kajenga hotel kubwa Mbeya shida iko wapi kapiga hela kwa wajinga kawauzia mafuta, maji ya chumvi nk. Geodavie wake za watu wanamkoma. Mwamini Yesu peke yake usiabudu wapiga hela, hao ni binadamu kama wewe. Mungu ni wawote na anamsikia kila anayemwamini na sio kupitia kwa binadamu mwenzako. Mathayo 4:10
Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.
Mnakubaki wake zenu wanakuwa wajinga. Wanakwendabkupikia, kufulia na kuwa hawara wa hao knaowaita "manabii na mitume". Mungu alishaonya kabla. Mathayo 24:24
Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.

Mathayo 24:25
Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele.

Manabii wanahitajika kwa ajili ya nini ambacho hakijaandikws kwenye biblia. Nabii anatabiri mpira wa Yanga na Simba. Nabii wanatabiri kwamba umelogwa kama waganga wa kienyeji. Ama kweli watu wamepungukiwa na maarifa ya kiimani. Isaya 5:13
Kwa sababu hiyo watu wangu wamechukuliwa mateka, kwa kukosa kuwa na maarifa; na watu wao wenye cheo wana njaa, na wengi wao waona kiu sana.
Watu wamekataa maarifa ya Mungu shetani kupitia kwa mawakala wake amewapiga upofu na hawaoni. Wana kiu na njaa ya maarifa ya Mungu na wasipojitambua watapotea milele.
[emoji120] [emoji120]
 
Hapo utajua ni mambo tu ya "kalumanzila" ni mikataba inayofifia. Ukiona watu wapo juani wanakusikiliza ujue Kuna nguvu inayowasukuma katika ulimwengu wa roho.
 
Jambo wadau?​

Naingia kwenye mada moja kwa moja pasipo kuwachosha na maneno mengi. Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikifuatilia upako wa manabii na mitume jinsi wanavyoanza huduma zao kwa pako za hali ya juu sana lakini baada ya muda zile pako huanza kufifia taratibu na kuisha kabisa. Nabaki najiuliza maswali kadhaa yasiyokuwa na majibu:
  1. Kwanini pako za hawa manabii zinapanda na kushuka ghafla kiasi hiki?
  2. Je, hizi pako ni za kweli au ni za mchongo?
  3. Kama ni za kweli kwanini zinaisha na kama ni za mchongo kwanini zikiisha wasirudi tena kuchukua nyingine kule wanakozitoa?
Yaani najiuliza maswali mengi bila majibu. Ndipo nikaamua kuanzisha huu uzi kwa kuwa humu JF kuna wabobevu wa masuala ya theology akina Mshana Jr wanaweza kutusaidia kujibu baadhi ya maswali haya.

Hebu jaribu kufikiria nguvu za upako alizokuwa nazo Askofu Kakobe enzi zile anafungua kanisa lake la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) halafu ulinganishe na hali aliyo nayo sasa hivi utagundua kuna kitu hakiko sawa. Si huyu tu bali walikuwepo Mitume na Manabii wengi hapa nchini wakiwemo Mzee wa Upako, Mch Antony Lusekelo ukiangalia jinsi alivyokuwa akikusanya mtiti na mabasi yake kila kona ya nchi halafu leo ukienda kule kanisani kwake unakuta mabasi yote yamepaki unabaki unashangaa. Hapa lazima kuna tatizo sio bure.

Ukitoka kwa hawa wawili njoo kwa Mtume Mwingira na Mtume Gwajima ujiulize zile nguvu walizokuwa nazo zamani zilipotelea wapi hadi sasa wamebaki na waumini wa kuungaunga. Tatizo ni nini hasa?

Manabii na mitume waliovuma siku za nyuma na kupotea kimuujiza ni wengi lakini nimetoa mifano ya hawa wachache kama msingi wa kujenga hoja yangu. Sasa hivi Mtume Mwamposa ndiye yupo juu lakini naye atakuja kuporomoka baada ya muda mfupi.

Njooni wajuzi wote tujadiliane hili jambo mpaka tupate jawabu la pamoja.

Nawasilisha.​
Pumbafu sana wewe biblia inakupa tadhari kuwa watakuja watu watajiina manabii na mitume watawapotosha wengi lakini wakiristo amuamini pamoja na kubeba kitabu hicho kwapani kila mala pumbafu pumbafu
 
Mitume aina ya Mwamposa wana tabia kama hii; wamefanikiwa kuwateka wanawake wanawapiga hela bila huruma.

Waliitwa na Mungu
Wakapofushwa na pesa pamoja na umaarufu wakaacha wito mkuu wa kuwahubiri watu kuwaandaa kwa unyakuo.
Mungu akawaacha katika njia zao za upotevu. Mostly wanadubiriwa jehanamu
 
HAKUNA MTUME MJINI..
MNADANGANYWA KWA KUTOYAJUA MAANDIKO.
 
Waliitwa na Mungu
Wakapofushwa na pesa pamoja na umaarufu wakaacha wito mkuu wa kuwahubiri watu kuwaandaa kwa unyakuo.
Mungu akawaacha katika njia zao za upotevu. Mostly wanadubiriwa jehanamu
Hakuna mtume mjini, mtume hanaga kanisa
 
Hapo utajua ni mambo tu ya "kalumanzila" ni mikataba inayofifia. Ukiona watu wapo juani wanakusikiliza ujue Kuna nguvu inayowasukuma katika ulimwengu wa roho.
Hakuna mtume mjini
Hakuna mtume mwenye kanisa...ukisikia mtu mjini kimbia ufe
 
Nliendaga Tanga kanisani kwake na mgonjwa wangu pale tukataka kuelezea shida yetu tukaambiwa tutoe laki kadhaa , duh hatukuwa nazo ikabidi tuwe wapole.

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
Sasa jamani kwa ''mtu wa mungu'' unaelezea tena shida? Mimi nilidhani huwa wanaombea na mtu anaponywa? Anyways wajinga ndiyo waliwao.
 
Jambo wadau?

Naingia kwenye mada moja kwa moja pasipo kuwachosha na maneno mengi. Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikifuatilia upako wa manabii na mitume jinsi wanavyoanza huduma zao kwa pako za hali ya juu sana lakini baada ya muda zile pako huanza kufifia taratibu na kuisha kabisa. Nabaki najiuliza maswali kadhaa yasiyokuwa na majibu:
  1. Kwanini pako za hawa manabii zinapanda na kushuka ghafla kiasi hiki?​
  2. Je, hizi pako ni za kweli au ni za mchongo?​
  3. Kama ni za kweli kwanini zinaisha na kama ni za mchongo kwanini zikiisha wasirudi tena kuchukua nyingine kule wanakozitoa?​
Yaani najiuliza maswali mengi bila majibu. Ndipo nikaamua kuanzisha huu uzi kwa kuwa humu JF kuna wabobevu wa masuala ya theology akina Mshana Jr wanaweza kutusaidia kujibu baadhi ya maswali haya.

Hebu jaribu kufikiria nguvu za upako alizokuwa nazo Askofu Kakobe enzi zile anafungua kanisa lake la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) halafu ulinganishe na hali aliyo nayo sasa hivi utagundua kuna kitu hakiko sawa. Si huyu tu bali walikuwepo Mitume na Manabii wengi hapa nchini wakiwemo Mzee wa Upako, Mch Antony Lusekelo ukiangalia jinsi alivyokuwa akikusanya mtiti na mabasi yake kila kona ya nchi halafu leo ukienda kule kanisani kwake unakuta mabasi yote yamepaki unabaki unashangaa. Hapa lazima kuna tatizo sio bure.

Ukitoka kwa hawa wawili njoo kwa Mtume Mwingira na Mtume Gwajima ujiulize zile nguvu walizokuwa nazo zamani zilipotelea wapi hadi sasa wamebaki na waumini wa kuungaunga. Tatizo ni nini hasa?

Manabii na mitume waliovuma siku za nyuma na kupotea kimuujiza ni wengi lakini nimetoa mifano ya hawa wachache kama msingi wa kujenga hoja yangu. Sasa hivi Mtume Mwamposa ndiye yupo juu lakini naye atakuja kuporomoka baada ya muda mfupi.

Njooni wajuzi wote tujadiliane hili jambo mpaka tupate jawabu la pamoja.

Nawasilisha.

Swali zuri sana! 👍
 
Huo ni uongo. Tukiwa duniani kila kitu kina mwisho haijalishi kimetoka wapi.

Refer:
hamna ki2 kinachomaliza upako kama,uzinzi,ushirikina{shirki} natamaa ya kuupenda ulimwengu!!!!''''{yaani kuna wa2 wanauona ulimwegu ndio pepo yao}
 
Hivi watumishi kama vile Kiboko ya Wachawi ukiwatazama kwa undani kuna nabii pale kweli au mpigaji tu?
 
Mzee wa upako aliamia kuwa mlevi, mwingira kazaa na mke wa mzungu, gwaji boy kakutwa na kahaba, kakobe kaficha fedha kwenye majaba pia kawakataa wadhamini wa kanisa kwama hawana chao kanisa la kwake. Kesi kasinda mahakamani kwa kanisa ni mali yake. Mwamposa waumini wake walikanyagana na kuangamia yeye kabeba fuko la hela kapanda ndege kia kukimbiza hela dar. Suguye kanisa limefungwa na serikali halina usajili. Mwamposa kajenga hotel kubwa Mbeya shida iko wapi kapiga hela kwa wajinga kawauzia mafuta, maji ya chumvi nk. Geodavie wake za watu wanamkoma. Mwamini Yesu peke yake usiabudu wapiga hela, hao ni binadamu kama wewe. Mungu ni wawote na anamsikia kila anayemwamini na sio kupitia kwa binadamu mwenzako. Mathayo 4:10
Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.
Mnakubaki wake zenu wanakuwa wajinga. Wanakwendabkupikia, kufulia na kuwa hawara wa hao knaowaita "manabii na mitume". Mungu alishaonya kabla. Mathayo 24:24
Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.

Mathayo 24:25
Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele.

Manabii wanahitajika kwa ajili ya nini ambacho hakijaandikws kwenye biblia. Nabii anatabiri mpira wa Yanga na Simba. Nabii wanatabiri kwamba umelogwa kama waganga wa kienyeji. Ama kweli watu wamepungukiwa na maarifa ya kiimani. Isaya 5:13
Kwa sababu hiyo watu wangu wamechukuliwa mateka, kwa kukosa kuwa na maarifa; na watu wao wenye cheo wana njaa, na wengi wao waona kiu sana.
Watu wamekataa maarifa ya Mungu shetani kupitia kwa mawakala wake amewapiga upofu na hawaoni. Wana kiu na njaa ya maarifa ya Mungu na wasipojitambua watapotea milele.
Mkuu umemaliza kila kitu, siongezi chochote. Ubarikiwe sana kwa ufunuo huu.
 
Back
Top Bottom